Monday, August 16, 2010

Si Malaria, si Ukimwi......NI SARATANI

Photo credit:Kick Cancer-Community Campaign
Ugonjwa wa saratani leo umetajwa kuwa unaoongoza kwa kusababisha vifo na pia kuongoza katika gharama za uchumi na hivyo kudidimiza uchumi duniani.
Katika taarifa inayotegemea kutolewa katika Mkutano wa dunia wa kudidimiza saratani utakaofanyika huko China wiki hii, imeelezwa kuwa licha ya SARATANI inagharimu maisha na gharama kuliko UKIMWI, Malaria na magonjwa mengine yaambukizwayo toka mtu mmoja hadi mwingine. Imeelezwa kuwa ugonjwa huu umegharimu takriban asilimia 1.5 ya GDP ya dunia kwa mwaka 2008, sawa na kiasi cha dola bilioni 895.
Shirika la Afya Duniani (WHO) lilitabiri kuhusu uwezekano wa ugonjwa wa saratani kuupiku ule wa moyo kwa kusababisha vifo mwaka huu. Takribani watu milioni 7.6 walikufa kwa saratani mwaka 2008 na zaidi ya watu milioni 12.4 hugundulika kuwa na maradhi hayo kila mwaka
NIWAZALO HAPA ni kuwa
Kwanini tusiwaze ni yapi yasababishayo magonjwa ya saratani?
Je! Maendeleo tunayoyakimbiza na kuyashindania, yana faida kuliko hasara?

Kwa sisi "nchi za mapokeo", tunapima vipi kila kiingiacho KUMLINDA MLAJI na athari za muda mrefu?
Je! Hatuna namna ya kuwianisha maendeleo na hasara ama madhara yatokanayo nayo?

NAWAZA KWA SAUTI TUUU
Waweza soma taarifa kamili kuhusu ripoti hiyo kuhusu saratani, bofya HAPA

5 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Kwa kweli inasikitisha sana kila mara usomapo katika magazeti na pia kusikia katika habari ya kwamba hili gonjwa limeshika nafasi ya kwanza sasa. Ni maswali mazuri uloyauliza kwa kweli Hivi kwa nini kusitokee mtu ajue chanzo chake ni nini???

emu-three said...

Kwa uoni wangu rahisi nahisi ni vyakula tunavyokula, vingi vimetokana na madawa ya viwandani, siunajua tena ili vyakula visioze au kuharibika lazima wachanganye na madawa, ambayo mengine ni sumu.
Vyakula vingine vina mafuta sana na bado watu tunakula kwa wingi, kuna sukari, chumvi, basi ilimradi tunajiua wenyewe bila kujijua, achilia mbli wavuta sigara, wanywa pombe kali nk.
Kwa ujumla maisha yetu yanakabaliwa na vikwazo vingi ambavyo tunajitengenezea sisi wenyewe, hasa kutoka viwandani.
Yote hayo mwisho wa siku yanaharibu mwili wetu kwa magonjwa kama hayo, kansa, kifua kikuu nk

malkiory said...

Ndugu Mubelwa, Saratani ipo kwenye kundi la magonjwa yanayotokana na tabia za maisha kwa kitaalamu yanaitwa lifestyle diseases, hili kundi la ugonjwa linaumiza vichwa hasa mataifa yaliyoendelea.

Wakati hali iko hivyo kwenye mataifa yaliyoendelea kwa upande wa mataifa masikini mbaya zaidi kwani bado tunapambana na magonjwa ya kuambukiza/Communicable diseases pamoja na haya yanatokona na lifestyle wakati kwa wenzetu wa mataifa matajiri msamiati huwa magonjwa ya kuambukiza unabaki historia.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

nikiwa mtanzania ninayeishi tanzania na hasa kanda ya ziwa, naamini ugonjwa wa kimataifa na ulioshindikana hapa ni MARALIA! ni ugonjwa hatari kwa mtizamo wangu na hivyo nahaha kuilinda familia yangu pendwa.

ila kansa inasababishwa kwa kiasi kikubwa na ulaji holela na ulimbukeni fulani hivi. mimi nilihama mji wa DAr nilipoona nataka kuzaa na kulea ila wanangu wanyonye madhiwa ya mama kwa muda mrefu then wale kitu nachuro.

mimi mwenyewe mlo wangu ni wa kiasili. tunapenda kubugia kila kitu mbele yetu utadhini mwili ni jalala, ni hatari hii!

harafu sasa kuhusu usasa, nawenywe ni soo, vyakula, hali ya hewa (AC) nk

tumieni tu wakuu ila lazima tubague vyakula

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Kamala una pointi. Kansa sasa ni ugongwa unaoibukia kwa kasi Afrika na mimi nadhani kwamba ni matokeo ya tabia yetu hii ya kuiga mambo hovyo hovyo - na hasa hili wimbi la kula vyakula vya kwenye masupamaketi, pombe kila siku, nyama zinazotokana na wanyama waliokuzwa kisayansi n.k.

Mwili kweli si jalala na inabidi tulitambue hili.