Sunday, October 10, 2010

Waliwaza, wamewaza, wanawaza na watamuwaza vipi MUNGU?

Kama nilivyoandika katika "toleo" la jana, yapo matukio ambayo kupona kwake kwategemea MUNGU pekee. Matukio ambayo mwanadamu hana "nguvu" wala msaada wowote zaidi ya kusubiri MABAKI ya kile kinachotendeka. Lakini nguvu za MUNGU zafanya yote.
Binafsi nimeshuhudia baadhi ya mambo ambayo wakati mwingine yakufanya uwaze kama kuna ustahili wa kuwa ulivyo ama kwa mwingine kuendelea kuwa alivyo. Nimesoma na kuona watoto waliookoka katika ajali mbaya tena bila michubuko, na mengine mengi. Yote haya (pamoja na yangu binafsi) hunifanya nirejee kwenye swali hilo hapo juu. Sasa kwa leo, tuwaangalie hawa ambao walichukua / wanaendelea kuchukua taswira ya vyombo vya habari kuhusu kupona kwao

Mtazame mwanajeshi huyu ambaye akiwa katika hatua za mwisho za kuhakikisha ndege ya kivita iko katika hali nzuri kuondoka, "alinyonywa" ndani ya injini na kutokea upande wa pili akiwa mzima. Zana za kujikinga zote ziliharibika na hata shati kuchanika lakini hakumung'unyuliwa. Huu ni zaidi ya muujiza kwani kwa sisi na wale wanaoshughulika na masuala ya anga wanatambua namna ambavyo majaribio ya injini hizi hutumia ndege kama bata mzinga ambao wanapopita mbele na kutokea nyuma huwa ni kama nyama iliyosagwa. Huyu kaka alikuwa na umbo kuubwa kulinganisha na ndege hao lakini akatoka mzima.
Unadhani alimuwa, amemuwaza, anamuwaza, na atamuza vipi MUNGU maishani mwake? Mtazame hapa chini...

Na pia tuyarejee maisha ya ndugu zetu wa Chile ambao kwa muda wote walionekana kuwa na matumaini makubwa. Kwa hakika ni kwa kuwa hawakuwa na namna nyingine ya kufanya zaidi ya KUKUBALI HALI.
Tazama maisha yao huko machimboni. Na ni kwa kukaa muda wote huo, kuvunja rekodi ya kukwama machimboni kwa muda mrefu na sasa tumaini la kuvunja rekodi ya uokozi ulio mgumu zaidi kufanyika machimboni, ninawaza hawa ndugu zangu waliwaza, wamewaza, wanawaza na watamuwaza vipi MUNGU aliyewatunza na kuwaokoa katika hili?
HIVI NDIVYO ILIVYOKUWA WAKATI WALIPOFIKIWA.

Na kazi mpya ya kuwatoa ndio inaanza kama waelezavyo Karl Penhaul na Chad Myers wa CNN


***"Waliwaza nini ni kipengele cha kuelimishana tukifurahia. Hiki kitakuwa kikikuletea habari za kweli na kushangaza kuhusu watu ambao wamefanya yale ambayo unaweza kujiuliza kuwa WALIWAZA NINI? wakati wanatenda haya.
Kitakuwa na habari fupifupi kutoka ulimwenguni kote. Kwa habari zaidi kuhusu kipengele hiki
BOFYA HAPA"***

3 comments:

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

ninachakoina hapa ni woga wako juu ya kifu kwamba Mungu anaokoa juu ya kifo ila hujui tu kwamba ili tuamie kw huyu Mungu na kuishi naye milele kufa ni hatua muhimu sana! na kuishi wakati mwingine ni hasara bora kufa tu

ila sasa sijui kama hajapaswa kufa hufi tu hata kama unaishi lakini umekufa!

Albert Kissima said...

Nami ninawaza watu waliohusika katika matukio haya nao wanawaza nini?

Pamoja na kuwa sifahamu injini ya ndege inafanye kazi, lkn tukio hili naweza kulifananisha na mtu aliyetumbukizwa kwenye tanuru la moto au kwenye mafuta ya kupikia yanayochemka halafu baada ya mda fulani akatolewa na bado akawa mzima mwenye uhai na bila kuungua sehemu yoyote ya mwili. Kwani, kama jinsi bata mzinga anavyosagwa, basi na huyu mwanajeshi ingekuwa vivyo hivyo. Ni jambo ambalo akili ya kawaida haiwezi kulielezea. Zaidi ya imani sijui kama kuna namna yoyote nyingine ya kuelezea matukio haya hususani hili la mwanajeshi.

Jeff said...

Kama ulivyosema,matukio ya kustaabisha yapo mengi.Nafurahi kusikia kwamba "kona" hii itayavalia njuga masuala kama hayo.Kila nionapo au kusikia kuhusu "miujiza"fulani huketi chini na kutafakari na kujikumbusha kwamba,siku zote,yupo ambaye aliye juu yetu sote.Kuna nguvu zishindazo za kibinadamu.Ni muhimu tukajikumbusha hilo kila mara.