Wednesday, December 1, 2010

Kutokomeza UKIMWI.....YES WE CAN!!!!!

Pengine yaweza kuonekana kama ndoto, na pengine yaweza kuonekana kama ni kitu kisichowezekana, lakini kwa hakika ni jambo linalowezekana. NAZUNGUMZIA KUTOKOMEZA UKIMWI NCHINI NA DUNIANI.
Japo ni kitu kiwezekanacho, lakini chahitaji jitihada za ziada.
Twahitaji malengo na pia utekelezaji wa nia.
Twahitaji kubadilika na kuacha kufanya ugonjwa huu kama mradi. Kisha kwa pamoja kuungana na walioathirika katika harakati zao za kuwa wazi. Wakiacha kunyanyapaliwa, wakapendwa, kuheshimika na kukubalika ndani ya jamii, watakuwa wazi zaidi kueleza namna tofauti walizopitia kufikia hali hiyo na kwa kufanya hivyo tutaepusha maambukizi mapya na kurefusha maisha ya wale wenye virusi hivyo. Japo idadi ya vifo vitokanavyo na ugonjwa huu vimeonekana kupungua kwa mwaka 2007 kwa mujibu wa TAKWIMU ZA W.H.O, bado tuna kazi ya ziada kuhakikisha tunawezesha namba ama takwimu hizi kufikia sifuri, yaani kuutokomeza ugonjwa huu.
Na hii ni CHANGAMOTO YETU sote.
Japokuwa kumekuwa na taarifa za awali kuonesha tumaini la kupatikana kwa KINGA na / ama TIBA ya ugonjwa huu, lakini KINGA HALISI NI KUJIEPUSHA NA USAMBAZAJI WA MAAMBUKIZI KWA KADRI YA UWEZO WETU
Kuutokomeza ugonjwa huu wa UKIMWI...... NDIO TWAWEZA
Tumwangalie dada huyu alivyoelezea namna alivyopokea matokeo ya vipimo vyake. Amekuwa muwazi juu ya hali yake, amekuwa mwelimishaji na mwanaharakati mwema kuhusu ugonjwa huu

Video yake kamilifu kuhusu biashara mbaya ya kuuza mwili pale UWANJA WA FISI waweza kuipata kwa kutembelea http://www.hyenasquare.org/
Basi tusikie wasanii nyota wa Uganda wanavyoungana kwenye mapambano haya muhimu juu ya gonjwa hili hatari.
"A little bit LOVE,
A little bit HOPE,
A little bit CAUTIONA IS ALL WE NEED.
A little bit WISER
A little bit SMARTER"


Ama twende CONGO ambako nao pia waliungana na kutoa kibao hiki kuhusu ugonjwa huu wa UKIMWI

KUTOKOMEZA UKIMWI NCHINI NA DUNIANI.....NDIO TWAWEZA

4 comments:

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

unaamin kweli kuna ukimwi kama ugonjwa ua siriha ya maangamizi ya Umma? ni swali

emu-three said...

Wakati mwingine najiuliza bila kukosa jibu. Kwa mfano nikitoka nje ya mada, kuna matangazo mengi yanayotoka kuhusiana na kupambana na malaria

`MALARIA HAIKUBALIKI...'
Na matangazo haya yamekita zaidi kwenye kutumia vyandarua...ukiangalia kwa makini zaidi utaona ni `matangazo ya kibisahara zaidi...labda kwa vile kuna vyandarua toka Marekani vya hati punguzo, lakini kama kwa ajili ya punguzo hilo vitanunuliwa kwa wingi kibiashara ni mafaniko makubwa!
Haya sasa ni matangazo ya kupambana na ukiwmi, na hapa naona ni matangazo ya kuuza kondomu kwa wingi..nasema hivi kwasababu kila tatizo lina chanzo chake, kwanini kwa mfani kwenye malaria hatupambani namzalia ya mbu?
Na huku kwenye UKIMWI, hatiangalii visababishii vya kuvutika katika ngono...tabia za kibinadamu zinaweza kuchangia, mfano mavazi, mfano mila, na mifani mingine ambayo inaweza kuwa nichanzo...lakini siku kama ya leo ni mtangazo ya kondomu...sio kwamba mengine hayapo, lakini yanayoonekana sana ndani ya runinga, ni nini...
Ngoja niishie hapa nisije nikatunga kisa ..

Simon Kitururu said...

Tukumbuke pia mambo kama BUG CHASING, GIFT GIVING, etc.......


``Bugchasing is a slang term for the practice of pursuing sex with HIV infected individuals in order to contract HIV. Bugchasers may seek HIV infection for a variety of reasons.

Bugchasers seek sexual partners who are HIV positive for the purpose of having unprotected sex and becoming HIV positive; giftgivers are HIV positive individuals who comply with the bugchaser's efforts to become infected with HIV.´´


Yote ni katika kujaribu tukumbuke kuna watu wanataka wenyewe kuambukizwa UKIMWI kisa wanajua hawana na wakifanyacho ni kujaribu kutafuta mwenye UKIMWI ili awaambukize.


Hii nikatika kuzidi kujaribu kusema ``DUNIANI KUNA MAMBO!`` na kuna mambo U THINK are the problem needing SOLUTION while others consider them ``LIFE with meaning´´.:-(


Kwa hiyo wakati tunaongelea kupiga vita UKIMWI tusisahau kuna watu UKIMWI ndio maisha yao KIMSHAHARA au hata mpaka kupata maana ya kwaninni WAKO HAI.


Nawaza tu kwa sauti!

Mzee wa Changamoto said...

Kaka KAMALA... Binafsi naamini hayo maangamizi ya UMMA kwa njia ya maradhi ndio ugonjwa wenyewe.
Naamini ni jibu tu. Lol

Mkuu EMU-THREE... Wala hujatoka nje ya mada, bali UMEIKUZA NA KUINYAMBULISHA ZAIDI. Tumejikita kwenye "kuzia" maradhi kwa namna imnufaishayo fulani badala ya kuiepusha jamii. Kinga ya ukimwi haielekezwi kwenye kuzuia vile viambukizavyo, bali kuuza vile viaminikavyo kuwa vizuia maambukizi. Umesema vyandarua, turejee kondomu na mengine.
Mtaka-TIFU KITURURU....Duh!!!
Natamani ningejua haya ili niandike mengine ama kivingine. Lakini umenipa changamoto nami nitaifanyia kazi
BLESSINGS