Wednesday, November 3, 2010

Kwanini nafurahia kushindwa kushinda kwa walioshindwa?????

Photo credit: GVLN Rao blog
Nani asiyejua kuwa "mwanzo halisi wa mlima ni mwisho halisi wa bonde"?
Ama ni nani anayesahau kuwa furaha ya sasa ni akiba ya huzuni ijayo?
Na kuna aliyesahau kuwa huzuni ya sasa ni akiba ya furaha ijayo?
Basi kwa "MANTIKI" hiyo hiyo.... kuna mengi ya kufurahia kwa wale walioshindwa.
Kuna mengi ya kujifunza na kuna mengi ya kusahihisha.
Kwa maana nyingine, ni kwamba ili walioshindwa sasa wahakikishe kuwa wanafanikiwa baadae, kuna ulazima wa waliofanikiwa sasa kushindwa baadae.
Sasa ni kwanini NIMEFURAHIA "kushindwa kushinda kwa walioshindwa"? Ntakwambia baadae. Malizia "kumeza" matokeo kisha nikueleze UTAMU wa UCHUNGU walionao wale walioshindwa wiki hii huko nyumbani Tanzania na hapa nyumbani.
PamoJAH

JICHO LA NDANI ni kipengele kinachozungumzia mambo mepesi na yaliyo ndani mwetu, ambayo yakiangaliwa vema na kwa tafsiri ama tafakari njema yanaweza ama ndio suluhisho kwa matatizo yetu. Kwa matoleo yaliyopita katika kipengele hiki, BOFYA HAPA

1 comment:

emu-three said...

Kama usemi usemao asiyekubali kushindwa sio mshidani, ingawaje kushindwa kunauma, ikizingatia kuwa mtu kajigharamia na hata kuvuka mpaka.
Lakini pia wahenmga walinena, kuwa kila jambo hutokea kwa wakati, na usiute na kulalama huenda ni kwa faida yako!
Aheri ya yule atakaye mshukuru mungu kwa kila jambo, kwani kwake heri ipo karibuni!
Cha muhimu ni subira, kwani subira huvuta heri!
Ni hayo tu mkuu!