Manny Pacquiao akisherehekea mkanda wake katika uzito wa Super Walter baada ya kumshinda mpinzani wake "mgumu" Antonio Margarito.
Photo Credit: Getty Images via Yahoo Sports!
Hili ndilo limfanyalo Manny Pacquiao aitwe KING OF POUND FOR POUND. Yaani kwa tafsiri isiyo rasmi ni MFALME WA UZITO MBALIMBALI. Usiku wa kuamkia leo ameweza "kumvuruga" mpinzani wake Anthonio Margarito katika pambano la kugombea mkanda wa World Boxing Council super welterweight katika pambano lililofanyika mbele ya mashabiki 41,734 waliojitokeza ndani ya uwanja wa Cowboy. Hili lilionekana kuwa kati ya mapambano magumu zaidi kwa Pac-Man ambaye wengi walisema hajawahi pambana na "kichwa ngumu" kama Margarito ambaye jana aliingia uwanjani akiwa na "faida ya urefu wa inci 5 na pia paundi 17 zaidi ya Manny.
Paquiao ameshakuwa bingwa wa dunia katika uzito wa paundi 112, 122, 126, 130, 135, 140, 147 na usiku wa kuamkia leo akatwaa taji la uzito wa Paundi 154
Na hizi hapa chini ni dodoso za pambano hilo toka Yahoo Sports
Kisha msikilize alipohojiwa na ESPN baada ya pambano
NA SASA TUNAJUA KWANINI FLOYD MAYWEATHER ANAMKIMBIA BONDIA-MWANASIASA HUYU WA UFILIPINO
Sunday, November 14, 2010
Manny Pacquiao.......mkanda wa 8, katika uzito wa 8 tofauti
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
1 comment:
Huu ndiyo mchezo wangu na leo sijalala. Nilikuwa na wasiwasi kwamba pengine Manny angeweza kudundwa. Nampenda huyu kijana wa Kifilipino kutokana na historia ya maisha yake hasa utotoni ilivyo ngumu; na jinsi asivyo na makuu wala kujidai pamoja na kwamba sasa ameshakifikia kilele.
Margarito, kwa upande mwingine, ni jeuri na sikufurahishwa na jinsi alivyomfanyia Miguel Cotto - huku watu wengi wakiamini kwamba pengine alitumia ule mchezo wake mchafu wa "kurundika mawe" kwenye bandeji zake. Ndiyo maana nilifurahi sana alipotwangwa kisawasawa na Sugar Shane Moseley.
Pambano la jana ilikuwa ni Manny katika kilele chake. Ilikuwa ni kama ule mtindo wa mfalme mwenyewe "I dance like a butterfly, I sting like a bee" na hilo jicho la kulia la Margarito sijui kama litaona mwanga tena. Halafu kama kawaida katika mahojiano ya mwisho wa pambano, Manny alionyesha ubinadamu wake kwa kusema kwamba hakutaka tu kumtandika "knockout" huyu jemedari wa Kimeksiko na katika raundi ya 11 alikuwa anamtaka refa asimamishe pambano kwani hakutaka kuendelea kumtwanga mpizani wake aliyekuwa amelewa masumbwi.
Ni wazi kwamba Manny wa jana atamchakaza Floyd "Money" Mayweather bila wasiwasi wo wote. Ndiyo maana anakimbia na nadhani kukimbia huku pengine ndiko kunamfanya asiwe "stable" kiasi cha kufanya mambo ya ajabu ajabu yanayomletea matatizo mara kwa mara. Ni mtu mwenye "ego" kubwa na anaumia anaposikia watu wakimsifia Manny na kumwacha yeye. Pengine akiishiwa na pesa ndipo atakubali kupambana na Manny - na hapo ndipo atakapochakazwa kwa mara ya kwanza - na kustaafu moja kwa moja!
Ndondi ni mchezo ambao unamwonyesha binadamu kama alivyo - mnyama - achana na hii michezo mingine ambapo binadamu anajifanya eti mstaarabu na mwenye mbwembwe tele!
Post a Comment