Thursday, November 18, 2010

Ni zipi athari za mitandao ya kijamii kwenye chaguzi zetu???

Credit: Simon Whatley
Nimewaza kwa kina namna ambavyo kusambaa kwa mitandao ya kijamii KUNAATHIRI michakato ya uchaguzi barani Afrika.
Hakuna ubishi kuwa mitandao hii imekuwa na ATHARI (zaweza kuwa nzuri ama mbaya) kwa jami zetu lakini bado nawaza NI IPI UIJUAYO?
Tunaona namna ambavyo wagombea wanatumia mitandao kama Facebook kukusanya uungwaji mkono, lakini kinachoweka shaka ni uelewa na uhalali wa waungaji mkono ambao wengine si halisi ama hawatumii majina na utambulisho halisi hivyo kutojua wako wapi na wanataka nini?
Lakini pia tumeona namna ambavyo matumizi ya mitandao kama YOUTUBE yanavyoweza kuepusha kero za polisi kwa kurekodi watendacho. Kakangu Chacha Ng'wanambiti aliandika kuwa kwa mara ya kwanza ameona Jeshi la Polisi likituliza ghasia bila kukiuka haki za binadamu, nami nikamjibu ni sababu ya Youtube..
Unadhani huyu kaka hapa chini angefanywaje kama kusingekuwa na video kamera? Si mnakumbuka "mbiringidhano" uliowakumba wa Zanzibar mpaka video zao "zikanyofolewa" kwenye mitandao ya kijamii?
Credit: The LHR
Na ndio maana nauliza kuwa NI ZIPI ATHARI (CHANYA NA HASI) ZA MITANDAO YA KIJAMII KATIKA CHAGUZI ZA AFRIKA???

5 comments:

Simon Kitururu said...

Ukizingatia ni watu wangapi kiidadi AFRIKA waguswao na TEKNOLOJIA hizi,...
.... nahisi its too early kuwa na HITIMISHO katika swala.


Angalizo:
Juzi juzi tu niliwahi kukutana na mwalimu wa chuo kikuu Dar-es Salaam ambaye ilibidi nielezee BLOG ni nini.

Sasa jiulize huko vijijini BONGO ambako wapiga kura ndio wengi zaidi ukianza kunukuu YOUTUBE sijui itakuwaje.

Ni mtazamo wangu tu!

Upepo Mwanana said...

Kitururu :-)
Nahisi teknolojia hii bado kabisa haijawafikia watu wengi.
Mitandao ya jamii inawanufaisha wachache tu, gharama ya internet ni kubwa huku kwetu Afrika, na hata wanaojua kuitumia, huklazimika kusoma wakiwa kazini tu. Wakiwa likizo hawapatikani tena. Na hata kama mtu ana uwezo wa kulipia, kuna sehemu akienda hawezi kupata network anaishia kukaa tu.
Bado tuna changamoto kubwa sana

Simon Kitururu said...

@Upepo Mwanana: Nakubaliana kabisa na ulosema!

Fadhy Mtanga said...

ukiyatazama matokeo ya uchaguzi mkuu uliomalizika hivi karibuni, utaelewa athari za mitandao hii.. ukitazama maeneo ambayo chadema imepata kura nyingi, utagundua ni yale maeneo ambayo watu wengi wana access na intaneti. hii ina maana kuwa sehemu kubwa iliyokubali mabadiliko ni ile ambayo wananchi wake wameweza kuwa na upatikanaji habari kwa kiwango kikubwa. kampeni zilizokuwa zikipigwa kwa njia ya intaneti, kwa mfano Mnyika pale Ubungo na Sugu pale Mbeya,Nyerere pale Musoma Mjini, (hawa ni wale niliofahamu walikuwa wakipiga kampeni pia kupitia mitandao hii) utagundua zimekuwa na mafanikio.
hatuwezi kusema kwa kuwa wananchi wengi hhawana access na mitandao basi mitandao hii haina athari. nikutazama uchaguzi wa 2005 kwa kuulinganisha na huu, ninayo kila sababu ya kukiri kuwa mitandao hii imekuwa na impact kubwa.
huu ni wangu mtazamo

Masangu Matondo Nzuzuzllima said...

Kama nilivyosema hapa:

http://matondo.blogspot.com/2010/11/hongereni-wanablogu-kwa-kazi-nzuri.html

Hebu tusiidogoshe nafasi ya mitandao hii zikiwemo blogu. Ukiangalia moto uliokuwa ukiwaka kule Jamii Forums, kwenye globu ya Jamii na kwingineko ni wazi kwamba blogu hizi zina athari kubwa. Hata kama zinasomwa na mtu mmoja haijalishi - huyo huyo mmoja anatosha. Mara nyingi falsafa kombozi huanzishwa/huenezwa na mtu mmoja.

Ni mwanzo mzuri sana na uchaguzi ujao mitandao hii itakuwa na athari kubwa zaidi.