Tuesday, November 2, 2010

Ni kweli Dk Shein kashinda..lakiniii..... labda Maalim Seif hajashindwa pia.

Septemba 3 mwaka jana niliandika makala yenye kichwa cha habari "Tunajidanganya wenyewe kudhani twawajali wengine (irejee hapa)" ambamo humo nilieleza kile ninachoamini kuwa UNAFIKI wa binadamu katika kudhani kuwa anampenda tu ilhali ukweli ni kuwa anapenda hisia anazokuwa nazo anapodhani anampenda mtu huyo. Nilisema (na hapa nanukuu) "Kuna ukweli ulioko 'nyuma ya pazia la akili zetu' kuwa, kila tufanyacho ni kwa manufaa yetu hata pale tuonekanapo ama kujitahidi kujifanya kuamini kuwa ni kwa manufaa ya tumfanyiaye." Ukweli huu umedhihirika hapo jana baada ya matokeo ya uRaisi huko Zainzibar kutangazwa ambapo mgombea wa CCM Dk Ali Mohamed Shein ametangazwa mshindi. Matokeo haya (ambayo blogu hii inayafurahia kuwa yamekwenda sawia bila vurugu kuu wala umwagaji damu), yalionesha kile ambacho wenye fikra chovu wameita UKOMAVU WA SIASA kwa kuwa mgombea wa chama cha upinzani Maalim SEIF SHARRIF HAMAD ameyakubali mara moja tofauti na chaguzi zilizopita. Hili lilizua mjadala na chuki kuubwa saana kwa wafuasi wengi walioamini kuwa kwa udogo wa tofauti za kura ni lazima kuna "uchakachuaji" uliojitokeza na hivyo kuamini kuwa Maalim Seif amewasaliti kuachia kiti hicho walichoamini kuwa "chao" kutwaliwa na Dr Shein.
Lakini wana haki ya kuwa hivyo maana wanaamini kuwa Maalim Seif ni "mpiganaji" wa kweli katika kutetea haki zao hasa wakikumbuka alivyosimma imara kupinga matokeo ya mwaka 1995, 2000, na 2005. Na hapo ndipo lijapo swali kuwa
MWAKA HUU KUMETOKEA NINI?
Ni kweli kuwa mwaka huu Maalim Seif ameshindwa "vibaya" kuliko awamu hizo tatu alizogombea? LA!
Ni kweli kuwa Maalim Seif ameona safari hii kuna ushindi wa dhahiri na ni kuwa ameshindwa kihalali??? Mmmmmmhhhh!!! SIJUI

Labda tuangalie takwimu hapa kule Zanzibar
JUMLA YA KURA ZILIZOPIGWA ni 364,924
KURA HALALI ni 358,815
KURA ZILIZOHARIBIKA ni 6109

DK ALI MOHAMMED SHEIN (CCM) amepata 179,809 sawa na 50.1%
MAALIM SEIF SHARIF HAMAD (CUF) amepata 176,338 sawa na 49.1%
SAID SOUD SAID (AFP) amepata 480
KASSIM ALI BAKARI (Jahazi Asilia) amepata 803
HAJI AMBAR KHAMIS (NCCR-Mageuzi) amepata 363
HAJI KHAMIS HAJI (NRA) amepata 525
JUMA ALI KHATIB amepata 497
Chanzo: http://www.wavuti.com/habari.html#axzz145HHz4Is

INA MAANA....tofauti kati ya kura za Dr Shein na Maalim Seif ni takribani nusu ya zilizoharibika. DUH!! BAHATI MBAYA SAANA HII

Ila ninalojua ni kuwa, katika huu mpango wa SERIKALI YA UMOJA WA KITAIFA, basi maalim Seif "atakuwa ndani" na kwa maana hiyo hakuna haja ya kuendelea kuburuzana.
Lakini swali jingine laja...
Kwani Maalim Seif alikuwa akigombea KWA MANUFAA YA NANI??????
Ya wale waliompigia kura na ambao waliendelea kutukana kwenye "chat rooms" baada ya yeye kukubali matokeo? Ama kwa ajili ya malahi yake binafsi?
HAPO NDIPO NINAPOTAKA UREJEE NUKUU HIYO HAPO JUU YENYE RANGI NYEKUNDU.
Na swali la ziada laja kuwa kama waliokuwa wakimpigia kura Maalim Seif walifanya hivyo ili aweze kuingia madarakani na kuwa mkombozi wao, si ataingia? Na akiingia si anaweza kuwa msaada kwao hata kama si Rasi? Tena kwa kuwa ameingia kwa "uhusiano mzuri na Raisi"?
Kwani waliyekuwa wakitaka akawatete si kakubali? Kwanini na wao wasikubali???
REJEA TENA NUKUU NYEKUNDU HAPO JUU
Labda nimalizie kwa kusema kile ambacho nilisema kwenye makala niliyoinukuu hapo juu kuwa
"Ukweli wa mambo ni kuwa HAKUNA JAMBO LOLOTE DUNIANI AMBALO ULIFANYA, UNAFANYA NA UNAWEZA KUFANYA NA LISIKUNUFAISHE AMA KUKUFAIDISHA KWA NAMNA YOYOTE. Ninalomaanisha ni kuwa kama itatokea ukapata faida ndooooog kuliko, ni ile ya kujua kuwa "hatimaye nimetekeleza" (wenyewe wanasema At least i did it) achilia mbali suala la kwanini umetekeleza.
Hakuna kisicho na faida maishani mwetu ambacho tunatenda.
Kama kuna ambaye anaamini kuwa alishatenda jambo lolote ambalo halikumnufaisha yeye, basi ajiulize mara mbili na kama hapati jibu la faida basi jiulize kama "uliridhika na yale mema uliyotenda?" Kama uliridhika na wema huo, basi faida yako ni hilo ridhiko."
YAWEZEKANA NI KWELI Dr SHEIN AMESHINDA URAISI WA ZANZIBAR.....LAKINI LABDA NA MAALIM SEIF NAYE HAJASHINDWA
Wakasirikao wamesahau "sig-out" ya Nguli wa habari za Africa SHAKA SSALI anayehodhi kipindi cha Staright Talk Africa
99;">Labda tuburudike na Nasio katika wimbo HYPOCRITES

NAWAZA KWA SAUTI TUUUUUUUU!!!!!!!!!!!!!!




Uchaguzi Tanzania ni "label" inayozungumzia namna niionavyo nchi yangu ya Tanzania ijiandaavyo na uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2010. Kwa maandishi mengine juu ya mada hii katika "label" hii BOFYA HAPA

1 comment:

emu-three said...

Nitapenda kuurejea usemi wake wenye busara aliousema jana kuwa `hakuna mshindi, bali washindi ni Wazanzibar..'
Unajua kila jambo lina mwisho wake, kama mtu mzima lazima ujiulize, haya yataisha lini, ni nini ninachokitafuta, je wananchi wanafaidika na hili, je hakuna njia mbadala.
Uongozi wa dhati ni kazi kubwa sana, hasa kuwatumikia wananchi. Na kwa yule anayeamua kwa dhati kuwa niwe kiongozi, hatalala kwa raha...wangapiwangapi wana moyo huo kama siokutafuta `kula'?!
Hongera sana Maalim, na kama ingelikuwa mimi natoa medali ningekuvika medali ya ushujaa, uvumilivu, hekima na busara!