Thursday, November 25, 2010

Nionavyo mimi....MAWAZIRI WAORODHESHE WATATENDA NINI, VIPI NA KUFIKIA LINI?


Hakuna ambaye hajasikia BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI lililotangazwa jana na Mhe Raisi Kikwete. Maoni juu ya baraza hilo ni mchanganyiko na wapo walioonekana "kulikubali" na pia waliolipinga ama kutoridhishwa nalo.
Wengi wa waliolikubali wameonekana kukubali zaidi uteuzi wa Mhe John Magufuli na Mhe Anna Tibaijuka katika wizara zao. Ni jambo la kufurahisha kuona BARAZA LINAUNGWA MKONO na wananchi. Kuna imani ama matarajio kwamba KUTAKUWA NA MAFANIKIO kutokana na kuungwa mkono kwa baraza hili. Hizi ni dalili njema.
LAKINI pia kuna walio na shaka. Wanaosema "wengi ni walewale" na wanahisi "ushikaji" umetawala uteuzi huu..
Wacha nami nianze kuweka yale nilonayo moyoni.
KWANZA niwapongeze wanaomuunga mkono Raisi (kwani hata bila kumuunga mkono baraza "litasonga"). Na pia wale wanaopongeza uteuzi wa Mama Tibaijuka niungane nao, lakini pia NIONYE AMA KUTAHADHARISHA kuwa Mama Tibaijuka ANAINGIA KWENYE MFUMO (pengine uliomomonyoka) AMBAO UNAWEZA KUWA KIGINGI KATIKA UTENDAJI WAKE. Bado naamini kuwa utendaji wa Umoja wa Mataifa ulikuwa na mazingira mazuri ya kazi yasiyo na mchanganyo na mkanganyo wa siasa kama ilivyo Tanzania yangu. Natumai watu watakaokuja kuangalia uongozi wake wataliweka hili katika fikra.
Ni hapa ninaporejea kwenye mada kamili kuwa
KABLA HAWAJAJITAMBULISHA KWETU KAMA MAWAZIRI, NINAPENDA WAJIPANGE NA KUANGALIA NI NINI WATATIMIZA KATIKA MIAKA MITANO IJAYO NA NI VIPI WATATIMIZA HAYO KWA KUFUATA ILANI YA CCM.
MAWAZIRI hawa wanalazimika kuwa na mipango kamili. Ninachukia kuona kila miaka mitano iishapo, tunalinganisha utendaji kazi wa mtu kwa kitu tusichokijua. Sasa watueleze ni nini tutarajie miaka mitano ijayo na kisha watupe mgawanyiko wa namna watakavyotimiza hayo kwa kufuata ilani za CCM. Wananchi WANA HAKI ya kujua utekelezaji wa AHADI HIZI ZA RAISI KIKWETE.
TOVUTI ZA WIZARA KUFAFANUA KAZI ZAO...Mhe. RAISI...ATI UMESEMA WIZARA YA MAHUSIANO NA URATIBU? Labda TOVUTI ZA WIZARA zitafafanua ni nini wizara inafanya ama inastahili kufanya. Hii Wizara ya Mahusiano na Uratibu ningependa kujua inahusika kuhusianisha na kuratibu nini? Pia "Mchanyato" wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo unatuelekeza wapi? Na katika TAARIFA YA MAREKEBISHO YA WIZARA KUTOKA MWANDISHI MSAIDIZI WA RAISI imesema "wizara ya vijana imehamishwa kutoka wizara ya kazi na kuihamishia wizara ya habari kwa sababu kuu mbili. Kwanza ni kushahabiana na michezo na utamaduni,...." NINAWAZA KUHUSU MSHAHABIANO HUU. Ni kweli kuwa katika yote yawafaayo na kuwahusu vijana, Ikulu imeona mshahabiano wao na Michezo na Utamaduni tu? Si Elimu, si Sayansi na Teknolojia, si Afya, Si Uwekezaji, Si Maendeleo ya Jamii, si Utawala Bora, si Uchumi, si Utalii, si Madini, si mafunzo ya jamii si, si, si ........?
Ningependa zaidi kujua zaidi kuhusu hili
AJALI ZA BARABARANI. Ni nani atakayechukua jukumu la kushughulikia kuzuia ajali na kuratibu usalama wa wananchi? Je! Ni Wizara ya Ujenzi (Barabara na Uwanja wa Ndege), Wizara ya Uchukuzi (Reli, Bandari, Usafiri Majini) ama Wizara ya Usalama wa Raia (ambayo hata sijui imekuwa "faded" ndani ya wizara ipi? Ama ni wizara gani?
WIZARA YA UCHUMI??? Nilipowasiliana Kaka Jeff Msangi na awaza kama wizara ya fedha ndiyo ishughulikayo na masuala ya uchumi. Ama mchakato wa uchumi ama uharibifu kutokana na madini utasimamiwa na Wizara ya Fedha, wizara ya Madini ama Wizara ya Mazingira?
Kuna mengi ya kuwaza na kuchangia kuhusu baraza hili ACHILIA MBALI KUWA NA WANAWAKE 9KATI YA BARAZA LA WATU 50.

"Wacha niachie" hapa, naamini nawe utaona la kuongeza katika kuisaidia TANZANIA YANGU ISONGE MBELE
Tuonane "Next Ijayo"

3 comments:

Koero Mkundi said...

Hapo umenena na lau kama wangefuata ushauri wako basi tungewapima kulingana na kile walichoahidi kutenda kwa miaka mitano. kwa upande wa Rais ahadi zake nimeziorodhesha kama kumbukumbu pale kibarazani kwangu na itasaidia sana baada ya miaka mitano kufanya tathmini na kuangalia kama ametekeleza au alitudanyanya?

emu-three said...

Uchapakazi wa mtu upimwe kwa kile anachokifanya kwa jamii, ndani ya wizara yake. Mimi nitamwangalia sana yule atakayeshughulikia wizara ya miundo mbinu, barabara hasa kilio hiki cha foleni za magari, pia maswala ya umeme! Tutajiajirije kama hakuna `nguvu ya kuendeshea mitambo' na wengi twategemea umeme...!
Angalieni sana vitu muhimu vya kumkomboa mtu wa chini, umeme ni muhimu sana, kama yalivyo mafuta(petrol)!
Muda mwingi sasa unapotelea njiani kwenye madaldala...muda huo ungefanya jambo kubwa sana...

Anonymous said...

Binafsi ninapata hasira sana pale ambapo mbunge anapopewa uwaziri wakati jimboni kwake kwa miaka kadhaa hakuna alichokifanya.
Sielewi kama Raisi huwa analizingatia hili kwa wabunge wazoefu. Mtu ameshindwa kusimamia vizuri jimbo lake, huo uwaziri anapewa wa nini? Cyril Chami binafsi sina ambacho naweza kujivunia nacho kuwa alikifanya cha maendeleo kule Moshi Vijijini na sijui mtu huyu alishinda vp ubunge ktk uchaguzi wa mwezi jana.
Habari zinadokeza kuwa mbunge huyu wakati wa kipindi cha uchaguzi wa serikali za mitaa, mbunge huyu alikiri kuwa hajafanya lolote ktk kipindi cha miaka mitano iliyopita na baadhi ya vijiji alikimbizwa, watu hawakumtaka kwa sababu hakuna alichofanya. Raisi anayaangalia mambo kama haya kabla ya kumpa mtu ridhaa ya kuiongoza wizara au ni vigezo gani anatumia? Ukongwe wa kuongoza wizara, au ufanisi? Je wananchi wa Moshi vijijini watakuwa na imani nae katika kuongoza wizara wakati hawaridhishwi na utendaji wake jimboni? Au waamini kuwa anamudu vyema wizara kuliko jimbo?