Friday, December 31, 2010

2010 - 2011......JAH GLORY

Mwaka ndio "unakatika" na kuna mengi yanayopaswa kuyatolea SIFA NA SHUKRANI kwa MUUMBA.
Kwanza kabisa ni UHAI wetu sote. Mimi niandikaye na wewe usomaye. Pili ni PUMZIKO JEMA kwa wote waliotutoka. Ni wengi ambao wanaondoka na (pengine) kuna unafuu kwa uondoka wao baada ya kazi ngumu na ya kuchosha wanayofanya hapa ulimwenguni na pia mateso na masumbuko wanayopitia ulimwenguni.
Wengi wetu husita kukubali hili kwa kuwa watu hawa hutufaa sana nasi twaona ugumu wa wao kwenda kupumzika wakituacha tukihaha na maisha yetu bila wao hata kama walituwezesha kuwa katika nafasi ya kujitegemea.
Binafsi namshukuru Mungu kwa mengi na wengi. Naweka sifa na shukrani kwa UHAI WANGU alionijaalia na namna anavyonijaalia kuutumia. Namshukuru kwa FAMILIA nzuuri alizonijaalia. Ameniwezesha kuishi kwa NDUGU, JAMAA na hata MARAFIKI ambao wamekuwa msaada chanya maishani mwangu.
Kisha akanijaalia kuwa na mke na mwana ambao mara kadhaa nimewatafsiri kama "STRESS BUSTERS" kwangu. WATU WEMA ZAIDI KUWA NAO KWA MWAKA HUU ULIOKUWA NA MAGUMU MENGI.
Lakini pia, mwaka huu nimebarikiwa na kujaaliwa KUEREVUKA. Kuerevuka kutokana na kusoma mengi mema toka kwa wale wema ambao waliamua kuweka maoni hapa na hata kwenye barua pepe. Heshima kwenu nyote.
Kama isemavyo "kauli mbiu" hapo juu, kumekuwa na mgongano chanya wa mawazo kuhusu namna tuonavyo tatizo, lakini mara zote mtazamo huo umekuwa ukielezwa kwa HESHIMA kwa pande zote. JAMBO NINALOJIVUNIA ZAIDI.
Siwezi kuzungumzia ku-blog bila kuwashukuru wenzangu wema ambao kwa wingi wao nahisi itakuwa vigumu kuwataja wote. Nilijaribu kuhusisha blogu zote nilizozijua KATIKA POST HII YA BLOGU KUTIMIZA MWAKA (irejee hapa) lakini sasa idadi ya washiriki wa blogu ni wengi na hata nikiwaza namna ya kuwaunganisha wote kwenye post, sitaweza.
Siwezi kuzungumzia maisha yangu bila kuzungumzia blogu na siwezi kusema blogu bila maoni. Vivyo hivyo siwezi taja maoni bila kumgusia Dada Mariam Yazawa. Mwanamaoni wa kwanza ndani ya changamotoyetu zaidi ya miaka miwili ilyopita. Na tangu hapo akafungua "mlango wa uelimishaji" toka kwa wanamaoni wengine wema. Leo najivunia mengi toka kwa wengi ambao kila uchao nawasiliana nao hapa na kwingine kwingi (mfano facebook na emails)
Shukrani tena kwa ndugu wasiopenda kuonekana ama kutambulika ambao licha ya kujua fika kuwa hakuna atakayewatambua (kwa urahisi) wameendelea kuwa na heshima barazani hapa.
Na tuapomaliza mwaka huu na kuanza mpya, napenda kuwatakia wote MAFANIKIO MEMA. Mafanikio ambayo si lazima yaje kwa njia ya "mteremko" kama alivyosema Orison Swett Marden alipotafsiri mafanikio akisema “Success is not measured by what you accomplish, but by the opposition you have encountered, and the courage with which you have maintained the struggle against overwhelming odds.”
Basi kwa kuwa ni Ijumaa, na ni siku ambayo huwa tunasindikiza maandishi yetu kwa muziki mwanana wa Reggae wenye "kushindilia" funzo la wiki, naomba nikuache na kibao chake Nasio Fontaine kiitwacho JAH GLORY.

Nami namshukuru Mwenyezi Mungu kwa uwepo wako wewe usomaye hapa, na natumai ushirikiano zaidi mwaka 2011 ambapo tutaweza kuisaidia jamii yetu kusonga mbele zaidi.
ASANTE KWA HESHIMA NA MUDA WAKO KUNISOMA MARA ZOTE ULIZONISOMA NA MARA ZOTE UTAKAZOENDELEA KUSOMA MAKALA HAPA
HERI YA MWAKA MPYA 2011

12 comments:

mumyhery said...

Heri ya Mwaka Mpya na kwako pia uwe wa mafanikio zaidi!!!

Fadhy Mtanga said...

kaka shukrani sana. nakutakieni heri ya mwaka mpya

Simon Kitururu said...

Kila la kheri Mkuu! Na asante sana kwa shule utupayo hapa kijiweni kwako ambayo kwangu imenifunza mengi tu!

Yasinta Ngonyani said...

Ahsante kwa mwaka huu, ahsante kwa kukufahamu, na kheri sana ya mwaka mpya wewe na familia yako. Tutaonana mwakani!!

Unknown said...

Ahsante sana mkuu kwa makala motomoto ulizotuanikia hapa jukwaani. Nawatakia kila la kheri na fanaka wewe na familia pia wapenzi wasomaji wa blog hii. Heri ya 2011

kashangaki said...

Hi my lovely nephew, Esther and my grand niece Paulina, how lovely to see you happy and we love you.
Well on our side the year is gone and 2011 is here, you will get it later but know we love you

then May I say

MAY 2011 be VERY VERY PROSPEROUS and then HAPPY NEW YEARRRRRRR

Mija Shija Sayi said...

Ubarikiwe kaka wewe na familia yako. Mungu awe nawe 2011. Amen.

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Muberwa;

Sina cha kuongezea isipokuwa kusema asante sana na Mungu Azidi kuibariki familia yako bila kuisahau ncha kali ya kalamu yako. Kila la heri sana sana!!!

Faith S Hilary said...

First of all can I say those pictures are AMAZING! Secondly, Happy New Year Bandio family :-)...that's it really...lol

PASSION4FASHION.TZ said...

Wow! a lovely people in da picture,Love you all and Happy new year my brother and your familiy!!
xxx.

Mbele said...

Kila la heri, Mkuu.

Rachel Siwa said...

Amani,upendo na baraka zitawale katika familiya yako!Kheri ya mwaka mpya!