Saturday, December 4, 2010

KOMBOLELA SHOW JUMAMOSI HII Desemba 4, 2010

Kama wewe ni mfuatiliaji wa mambo ya kisiasa, mojawapo wa mambo yametokea siku za karibuni ni uanzishaji wa matawi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) nje ya mipaka ya Tanzania kama vile India, Uingereza, n.k. Kujiunga na chama chochote ni haki ya kikatiba ya kila Mtanzania, kwa hiyo uanzishaji wa matawi ya chama chote chote cha siasa nje ya Tanzania sio kosa, hasa uanzishaji wa matawi unapokuwa hauvunji sheria ya nchi hizo za nje.

Tatizo, pengine ni hisia kwamba waanzishaji haya matawi ya chama nchi za nje, hasa ya CCM, ni wasaliti wa watanzania wengi ambao ni masikini. Hilo linatokana na matarajio kwamba Mtanzania ambaye amefanikiwa kutoka nje ya nchi amepanuka kimtazamo na kwamba mtu ambaye amepanuka kimtazamo na ana ujasiri, hawezi kukiunga mkono CCM, chama ambao kimekuwa madarakani muda mrefu bila kuleta maendeleo ya kweli kwa mtanzania masikini.

Radio Mbao kupitia Kombolela Show itakuwa na mahojiano na Maina Owino ambaye ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) tawi la Uingereza ili kufahamu mtazamo wake juu ya uanzishaji wa matawi ya CCM nchi za nje.

Jiunge nasi kwa kupitia hapa: http://www.radiombao.com/ ili usikose uhondo!
Kumbuka show yaenda hewani jumamosi saa 7 - mchana kwa Marekani ya Mashariki ama saa 3-4 usiku kwa saa za Afrika za Mashariki

Your Host
Metty

1 comment:

Anonymous said...

Mzee wa Changamoto,

Kuna kipindi nilikuwa na mawazo ya kuwa mtanzania akitoka nje ya nchi anaweza kuwa na mtazamo tofauti kuhusu siasa za nyumbani, kwa kifupi nilidhani "exposure" inaweza kufungua mishipa ya uelewe, lakini uzoefu mdogo nilioupata ni kuwa ni HAPANA! Waafrika kwa ujumla, wengi wetu tumetoka nje ya Afrika, tumetembea ulimwenguni, tumeona maendeleo ya Ulaya, Marekani, Japan, na kwingineko, lakini nini kimefungua mishipa ya ufahamu wetu hasa jinsi ya kutuondoa na balaa la umasikini unaotukukabili, Kwetu sisi haipendwi kwa ideology yake, kimekuwa ni chama cha washikaji! ukitaka mambo yake yaende uwe mwanachama wa Chama hicho, CCM sio ile ya wakulima na wafanyakazi, sasa hivi CCM inatangeneza super class, na ukitaka kuila keki ya nchi jitahidi kuwa mwanachama!kwa kifupi keki wanayotaka kuila ni ndogo mno! iko siku wataumana meno wao kwa wao! kama umeshindwa kupingana nao jiunge nao!

Kila la heri "orbi"