Monday, December 20, 2010

Tunapofunga mwaka, tujali UHAI kuliko pesa.

Ni MSIMU mwingine ambao tunajua kuwa wengi hurejea nyumbani kwa mapumziko ya Krismas na Mwaka Mpya. Na mara zote huwa ni furaha saana msimu huu ufikapo, lakini kama Lucky Dube alivyoimba kuwa "where there's a pleasure, there's always a danger" nami nakumbusha kuwa ule "uroho" wa pesa wa kupandisha nauli, kuongeza safari za mabasi na vyombo vingine vya usafiri bila kujali matengenezo na ukarabati wa vyombo hivyo, mashindano ya "nani atafika wa kwanza" baina ya vyombo hivyo na pia kutenda kazi kwa muda mrefu bila kupumzika kwa waongoza usafiri huo kumekuwa kukizua vilio kila mwaka na hata wale wasiopoteza maisha wanabaki na maumivu ama vilema vya Maisha.
Kuna raha wakati huu wa sikukuu na kuna pesa pia kwa kuwa watu wana uhitaji wa kwenda kujumuika na familia zao, lakini kama wamiliki hawatakuwa makini, basi kutaendelea kuwa na karaha kwa wale ambao licha ya kulipa pesa nyingi, bado wanaweza kutofika waendako, ama kufika wakiwa na maumivu ama mapungufu na kibaya zaidi wasipate malipo yoyote kukidhi matibabu yao kama ilvyotokea kwa baadhi yetu miaka 11 iliyopita.
Tukumbuke kuwa katika kila raha tuisakayo wakati huu wa sikuku, kuna uwezekano wa karaha kuambatana nayo. Na tuwe waangalifu na wajalifun na waheshimifu kwetu na kwa wenzetu.
Amani, Upendo na Usalama kwenu nyote nyakati hizi.

3 comments:

emu-three said...

Na uishe kwa amani na uje mpya kwa amani!

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Usemayo kaka ni kweli tupu. Ndugu zangu wa Kishumundu hasa wanapaswa kuzingatia maana kwao ndiyo wakati wa kwenda kufanya ibada zote halali na haramu.
Tuwe waangalifu jamani. Kwani maisha matamu hata kama magumu.

Faith S Hilary said...

Happy Holidays bro together with your family! I just hope people (or should I say we? I don't do anything anyway lol) will enjoy the holidays responsibly, too much of everything is always harmful