Monday, December 13, 2010

Za Kale vs Maisha ya Sasa....KIFO

Wachambuzi Kaka Kaluse na Kaka Kamala wamezungumzia saana kuhusu Kifo. Wamezungumzia kuhusu majina na matukio na hata hisia zake na pia namna tunavyotakiwa kukichukulia. Mada zao juu ya hili hazikuwa rahisi kuzikubali hasa kama hukubaliani ama kuamini katika "maisha baada ya maisha". Lakini hapa sijiulizi juu ya tafsiri wala namna kijavyo, bali najiuliza kuwa endapo tungekuwa tunajua siku ya kufa kwetu, tungekuwa watu wa namna gani? Tungekuwa wema tukiamini kuwa tunamalizia siku zetu kwa wema zaidi? Tungekuwa wakatili hasa tukijua kuwa hakuna jema tunaloweza kufanya likatusaidia kuishi kuiona kesho? Tungekuwa na maandalizi mema kwa vizazi vijavyo kwa kupanga maandalizi ya kifo, msiba na gharama zote ama ingekuwaje?
Sijawahi kupata jibu la swali hili ambalo kwa namna moja ama nyingine mwimbaji Remmy Mtoro Ongala aliuliza alipokuwa "akikihoji" kifo kuhusu uwepo, uhalali na hata matendo yake kwa wanadamu. Ukimsikiliza kwa makini utasikia maandalizi anayosema anataka kuyafanya kuepusha matatizo yanayojitokeza kwa waroho wa mali za wafiwa akisema "sitakulaumu maana nitakuwa nimeacha msimamo nyuma yangu."
Swali ni kuwa tungekuwa binadamu wa namna gani leo, kama tungekuwa tukijua kuwa kifo chetu ni kesho?

Habari zilinizonifikia sasa hivi ni kuwa Dr Remmy amefariki dunia usiku wa kuamkia leo.
Kuna mengi ya kukumbuka kuhusu Dr Remmy, lakini kubwa ni uwezi wake wa kutunga nyimbo zilizogusa maisha halisi ya mTanzania MHITAJI mpaka kufikia hatua ya kuitwa SAUTI YA WANYONGE.
Ulale mahala panapostahili Dr Remmy
** Zilipendwa ni kipengele kinachokujia kila Jumatatu kukuletea muziki wa kale kuhusisha na maisha, muziki ama sanaa ya sasa katika nyanja mbalimbali. Unaweza kusikiliza nyimbo nyingine ndani ya kipengele hiki kwa kubofya hapa, ama mtandao shirika hapa**

8 comments:

malkiory said...

REST IN PEACE REMMY ONGALA.

Anonymous said...

Kaimba kuhusu kifo na sasa kimemchukua Rest in peace Remmy.

Simon Kitururu said...

R.I.P Dr Remmy!

Yasinta Ngonyani said...

USTAREHE KWA AMANI REMMY MTORO ONGALA.

emu-three said...

Tunachoweza kusema kwa sasa ni kumuombea safari hiyo, ambayo kashatangulia mbele, ...hayo ndiyo maisha, leo kwake kesho kwetu!

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

unafikiri hatujui kuwa tutakufa?

twajua tu na fanya utafiti kuna waliotuaga kuwa watakufa kabla ya kufa na wakafa akiwemo Munga tehenan na Kristo

Upepo Mwanana said...

Tunasikitika kumpoteza Remmy

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Pumziko jema Remmy.

Wakati nikianza kublogu (na kabla sijamwelewa Kamala vizuri) niliwahi kuandika makala hii kuhusu kifo:

http://matondo.blogspot.com/2009/01/tuzungumzie-kifo_28.html