Thursday, January 27, 2011

Twachagua maongezi, maongezi yachagua mawazo na mawazo yatuchagulia jamii

Photo Credits: Workfromhome.com
Maongezi yanaweza kuwepo katika namna nyingi ikiwemo ile ya kuongea kwa sauti ama yale yaendeleayo kimyakimya akilini mwetu ambayo wengine wanayaita mawazo. Lakini ni mazungumzo haya ambayo huchukua jukumu kuubwa la kutambua mengi na kutambulisha mstakabali wetu. Ni haya yanayorekebisha mienendo yetu, maamuzi yetu, mawazo yetu, hisia zetu na hata matendo yetu. Ni mazungumzo haya yaendeleayo vichwani mwetu ambayo huanza bila hata ruhusa ya muwazaji, ambayo hupelekea matokeo ya aina mbalimbali. Fikiria mazungumzo yanayokuwepo ndani ya kichwa chako pale uonapo kitu upendacho (awe mtu, gari, nyumba, kazi ama chochote). Hili ndilo husababisha mtu kufuatilia ama kupuuzia kile aonacho. Kwa maana nyingine ni kwamba tuna kila uwezo wa kuchagua aina ya mazungumzo yanayoweza kuwa na ushindi ndani ya vichwa vyetu. Hili laweza kwa kuanza kuchagua watu wakuzungukao ambao kwa namna moja ama nyingine wanaathiri mazungumzo yetu ya nje kisha ya ndani. Pia waweza kuwa makini na namna maongezi ndani mwetu yanavyogawanya matukio na umuhimu wa yaliyopita, yaliyopo na yajayo. Lakini pia katika makundi hayo matatu kuna makundi mengine manne ndani mwake ambayo ni VITU, WATU WENGINE, SISI NA MAHUSIANO.
Watu wengi hujikita kwenye kuongelea vitu (kama magari, nyumba, safari, michezo nk) na watu wengine ( kama wanasiasa, watoto, waigizaji, majirani wafanyakazi wenza, watalaka nk) kuliko wanavyojizungumzia wenyewe na mahusiano yao.

Ukweli ni kwamba maongezi tuanzishayo kichwani huchagua nini tutaendelea kuwaza na hiyo hutufanya tuchague watu tunaopenda kushirikiana nao na hiyo yageuka kuwa jamii yetu.

JAMII YAKO NI IPI NA WAICHAGUA VIPI? Yangu ni pamoja na wewe unayemaliza kusoma hapa. Nimeamua kuishi na maisha ya mazungumzo chanya, mawazo chanya na hayo yatanifikisha kwenye jamii chanya. Kwa Ujumla naishi uchanya.
Msikilize Nasio hapa chini (ama bofya hapa) katika kibao LIVING IN THE POSITIVE anapozungumzia namna maisha yanavyoweza kuwa tofauti iwapo utaamua AKILINI kuwaza chanya.

1 comment:

Simon Kitururu said...

Na wasiwasi na uwezo wa kibinadamu kuchagua !:-(

Samahani kwa kuwaza hasi !:-(