Friday, February 4, 2011

Them, I & Them.....RISE UP....Nasio Fontaine

"Hey! Rise up people Rise up, don’t make them fool you no more......
Wake up people wake up, can’t make them fool you no more.....
Yeah! Power to the people set the captives Free
Freedom is a must, come on and up with the people’s movement
And the people Rise and Say, LIBERATION IS TODAY
And the people Rise and Say POLITICIANS MUST OBEY"
Ni juma jingine ambalo ULIMWENGU umeshuhudia NGUVU YA WANANCHI inavyoendelea kuisumbua dunia. Kama anavyoimba Nasio kwenye wimbo huu kuwa "Power to the people set the captives free", tumeshuhudia namna ambavyo WATU WALIOCHOKA na ambao wanahisi WAMEFIKISHWA MWISHO WA UVUMILIVU wakiamua kulazimisha mabadiliko. Wameamua kuamka na kudai kile kilicho chao. HAKI YAO.
Japo katika kudai haki kuna "wasio haki" wanaotaka kuingia kwa haki za watu ili kuwanyima haki hizo, lakini bado tunaona NGUVU YA UMMA.
Hili si geni. Hili halijaanza kuonekana na kusemwa leo. Kwenye ukurasa ama "label" hii ya I & THEM tumeandika kuhusu UKWELI ULIOPO KWENYE ROOTS REGGAE katika kueleza matatizo ya watu. Ukweli ambao unaendelea kubaki na kweli yake miaka mingi baadae kwa kuwa MATATIZO BADO YAPO. Ukifuatilia kipengele hiki utatambua nisemalo.
Lakini leo turejee yanayotokea Misri, Tunisia, Yemen, Jordan na kwingine ambako watu wameamua (ama pengine kuamulishwa ama kusaidiwa kuamua) kuondoa UTAWALA uliopo na kuleta mwingine kwa tumaini la kuwa \utakuwa na manufaa kwao.
Basi Ijumaa hii nisiwe na maneno mengi, natambua kama (hata kwa bahati mbaya) umefuatilia habari, utajua ninalozungumzia. Je! Wanasiasa wata"OBEY" kulingana na haya yanayotokea?
Msikilize Nasio Fontaine na kibao chake RISE UP kutoka albamu ya LIVING IN THE POSITIVE ya mwaka 2003.

Kwa wale msomeao kwenye mitandao isiyoonyesha "player", BOFYA HAPA kuusikiliza kutoka nilipouhifadhi.
Yeah! Rise up ye Mighty people
We gonna Rise up uhh
We gonna Wise up, yeah!
We gonna Wake up
Come on! You Mighty people

Hey, Rise up people Rise up, don’t make them fool you no more
Nuh, no, no, no, no, no, no, no, no
Wake up people, Wake up come on!
Can’t make them fool you more more. Nuh,
Liberation is a must
Yeah! Power to the people set the captives Free
Freedom is a must.
Come on and up with the people’s movement
And the people Rise and Say, liberation is today.
And the people Rise and Say, FREEDOM IS TODAY

We gonna Rise up come on!
We gonna Wise up, uuhh!
We gonna Wake up
Rise up Mighty people
We gonna Shake up
Pah dap, pah, pah, pah, pah, dap, pah

Hey! Rise up people Rise up, don’t make them fool you no more
No, no, no, no, no, no, no, no, no, no, no
Wise up people wise up, can’t make them fool you no more
People are rising up fighting for freedom
Force of the people is on the rise.

Hey, Rise up people Rise up, don’t make them fool you no more
Nuh, no, no, no, no, no, no, no, no
Wake up people, Wake up!
Can’t make them fool you more more. Nuh,
Yea! Break the Chains things must be rearranged
Up you Mighty race accomplish what you will
And the people Rise and Say LIBERATION IS TODAY
And the people Rise and Say Politicians must obey

We gonna Rise up, come on ye mighty people
We gonna Wise up, liberation is a must
We gonna wake up huhh, come on, come on
We gonna Shake up,
Cause you’ve been kept down for so long, yeah,
And the people Rebel, we’re gonna Win now
And the people Rebel. Revolution time
And the people Rebel, Lord, Lord, Lord
Yes the people Rebel, yes and the people rebel
Yeah! And the people rebel, Ras Tafari Live


**Them, I & Them ni kipengele kikujiacho kila Ijumaa kinachoelezea kazi za wasanii (Them) kulingana na maono yangu (I) kwa ajili na manufaa ya hadhira (Them)**
Kwa nyimbo zaidi ndani ya kipengele hiki bofya hapa.
IJUMAA NJEMA

7 comments:

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

nguvu ya umma, na iheshimiwe

Triple S said...

Watu wakichoka lolote laweza kutokea hasa wakiona wanafnywa wajinga.

Simon Kitururu said...

Mmmh!

Ijumaa njema MHESHIMIWA!

Unknown said...

Ni umbali gani umebaki ili tufike mahali pa urithi wetu?

emu-three said...

Kweli `nguvu ya umma ' iheshimiwe na mabavu sasa yamepitwa na wakati..`suluhu, mjadala na kuridhiana' tukubali sote ni binadamu, na tunataka `mkate' wetu wa kila siku, lakini je mkate huo `unaupataje' ukizingatia kuupata kwako ni kuwaibu kwa `dhamana' uliyopewa!
Mhhh, labda muda umefika wa `umma' kujua kuwa wao ndio waliowaajiri viongozi wao wa siasa, sasa kwanini `tuwaogope' wafanyakazi wetu?

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Ukiwafikisha watu kwenye "liwalo na liwe" hata ungekuwa na silaha kali na jeshi kubwa na katili namna gani ni kazi bure. Historia imejaa mifano tele ya aina hii. Ndiyo maana watawala wengi hukazania zaidi katika kuudanganya na kuuengaenga umma na kuhakikisha kwamba unabakia katika kunguku. Kama alivyosema Kamala:

"nguvu ya umma, na iheshimiwe" DAIMA!!!

Ndugu Nkwazi N Mhango said...

Bahati mbaya ni kwamba watawala wetu wanaona yanayotokea huko yatokeako kama hayawahusu wakati yanawahusu sana kuliko hata waliokwishaonja joto ya jiwe.