Friday, March 25, 2011

Them, I & Them...BABYLON YOU DOOM....Nasio Fontaine

"Babylon you speak of peace yet you make more wars.You suppress the Innocent to deceive the Poor. Death and destruction hungry baby, mother breast run dry.Yet you plan more wars in your private sessions...." NASIO

Juma hili tumeshuhudia MAPIGANO YA KUSAKA AMANI huko nchini Libya ambayo leo yameingia siku ya saba. Ni mkanganyiko wa maneno na matendo ambao kwa hakika unaweza kumfanya asiyejua chanzo na uhakika ama uhalali wa habari kushindwa kujua nani wa kulaumu ama nani wa kushabikia.
Lakini yote juu ya yote, NIMEPENDA KULIANGALIA SUALA HILI KWA JICHO LA NDANI KIASI.
LABDA NI KWELI kuwa Mouamar Gadhafi ni kiongozi mkatili na utawala wake wa miaka 42 unamfanya ajisahau na kuwasahau wananchi wake.
Labda ni kweli kuwa Mouamar Gadhafi ameigeuza nchi kuwa mali yake (kama inavyosemwa) na kuwa analoamua ndilo linalofanyika. Kumekuwa na malalamiko kuwa Gadhafi amekuwa na maamuzi juu ya kila kitu kuhusu Libya. Inasemekana kuwa hawapi wananchi wake uhuru na wa aina yoyote. KAMA NI KWELI POLE KWAO.
Lakini ulipotokea mgogoro nchini humo, tumeshuhudia wale waitwa WAASI, ambao si kundi maalum na hawajulikani wanasimama katika itikadi gani, wameweza KUPATA SILAHA ZA KIVITA NA HATA KUWEZA KUTWAA BAADHI YA MIJI KUTOKA KATIKA MAJESHI YA SERIKALI.
Nawaza iwapo Gadhafi alikuwa akimiliki nchi kwa namna yake, na nina hakika kuwa silaha hizi hazikuwepo kabla ya UASI kuanza, ni nani anayewapa WAASI hizo silaha? Ni kwanini wakati wanafikiria kuweka MARUFUKU YA NDEGE KURUKA wasifikirie anayehusika kuwapa silaha WAASI wanaopigana na Kanali Gadhafi? Ulikuwa ni MKUTANO WA KUTAFUTA AMANI NA USALAMA WA RAIA HUKO LIBYA lakini mbona unaonekana kutokuwa na suluhisho la amani? Ni kweli kuwa silaha hizi zimepatikana kwa MSAADA? Na ni nani anayetoa "msaada wa silaha" kwa kundi ambalo mpaka sasa halijulikani?
Lakini si hiyo tu.....U-wapi UMOJA WA AFRIKA? Ni kwanini UMOJA WA AFRIKA haukuchukua / kupewa jukumu la kutekeleza ulinzi pale "KAKA MKUBWA" (Umoja wa Mataifa) alipotoa AMRI ya kuzuiwa kwa harakati za Kanali Gadhafi za kutumia ndege na vifaru kushambulia ngome za waasi? Na kwanini mpaka sasa hatusikii NGUVU HALISI ZA UMOJA HUO? Maamuzi kuhusu wana wa Afrika yanatolewa na Umoja wa Mataifa na kutekelezwa na NATO? Ninalosikia ni kuwa Umoja wa Afrika unapinga yaliyotokea, lakini hakuna la ziada.
Unapomsikiliza Gadhafi, anasema anapigana kuwaondoa Al Qaeda walioingia kuvuruga amani nchini mwake. Umoja wa Afrika haujachukua hatu katika hili licha ya kuwa raia na hasa watoto wasiojua hata tafasiri ya vita wako hatarini. Umoja wa Mataifa umesema na umepeleka ndege za kijeshi kutuliza ghasia na kuwalinda RAIA.
KILA UPANDE UNAZUNGUMZIA VITA KAMA NJIA YA KUPATA AMANI....Ni kweli?
Tumsikilize Nasio Fontaine HAPA na kibao chake BABYLON YOU DOOM kutoka katika ablamu ya REGGAE POWER

Intro:
Do, do, do, do, do, Tup tu doop
Yah, yah, yah, yah, yop tu doh pmm
Who uhh who wohh ohhy yea yea
Doobi, doobi, dopp tu doop
Hhbi, dooby, dooboop, hoh ohh ohh
Wuh uhh yea, yea, yea, yea, yea

Verse 1:
Babylon you speak bout peace yet you make more wars,
You suppress the Innocent to deceive the Poor.
Death and destruction hungry baby mother breast rum dry
Yet you plan more wars in your private sessions

Chorus:
Babylon you doom. You doom, doom, doom
Babylon you fail. Yes you fail ..x2

Verse 2:
You building more bombs and guns
Yet the babies are dying from hunger
We are the victims of your oppression
Blood of the Innocent that you slaughtered is upon your hands
You gave the guns, You set the fight,Then you sit aside
And watch the slaughter

Chorus:
Babylon you doom. You doom, doom, doom
Babylon you fail. Yes you fail
Babylon you doom
Your writings upon the wall, now
Babylon you fail. Yes you fail
Fire burn down Rome

Prrr, ra da da
Babylon you doom. You doom, doom, doom
Babylon you fail. Yes you fail
Babylon you doom
The writings upon the wall now, wohhy
Babylon you fail
Yes you fail

Bridge:
We are the victims of your oppression
And every day man another life, yeah
How many nations
How many lives you've taken
How many nations you destroyed
How many lives you've taken
Ou doom, doom, doom
Woh, uhh! Whohy you doom, doom, doom
So Babylon you doom doom, doom, doom
Who, uhh, who man you doom, doom, doom
So oppresser man you doom doom doom
Ohh! Mr. Wickedman you doom, doom, doom
See them running from their wickedness
Lord oh! Lord, Lord, Lord
See them running from their Filthiness, ohh! Ohh!
Numbered are your day Mr. Global sheriff
Where you gonna to
For shelter

**Them, I & Them ni kipengele kikujiacho kila Ijumaa kinachoelezea kazi za wasanii (Them) kulingana na maono yangu (I) kwa ajili na manufaa ya hadhira (Them)**
Kwa nyimbo zaidi ndani ya kipengele hiki bofya hapa.
IJUMAA NJEMA

1 comment:

emu-three said...

Akitoka gDafi nani...! Ni msururu uliopangwa kiutsadi, kwani nakumbuka tulijiuliza kuwa akitoka aliyekuwa raisi wa Iraq atafuata nani, tulitabiri labda ni huko Iran, kumbe kuna wengine...Hayo yametimia, swali akitoka Gadafi nani anafuata?
Kuna jamaa alisema sisi tukiwa tunahangaika kupiga kura wenzetu walishajua kuwa nani atakuwa raisi wetu kwasababu wametutawala katika kila nyanja, hata kifikira, wao ni kama waganga wa kienyeji, ikishindika `mtutu upo'...ndio hayo unayaona huko Libya!
Ipo siku wana Libya watamkumbuka Gadafi pamoja na `uroho wake wa madaraka'