Saturday, March 5, 2011

Weka maelezo yako.....

Maelezo ya Kaka Francis Godwin wa blogu ya MATUKIO DAIMA (mwenye hakimiliki ya picha hii) yanaeleza HAPA kuwa "Wazee wa wilaya ya Ludewa wakiwa katika maombi ya kumwombea mbunge wao na kuombea chakula kilichoandaliwa na mbunge huyo baada ya kumalizika kwa kikao cha kupokea mawazo ya wananchi juu ya vipaumbele vya jimbo hilo bungeni"
AMA KWELI PICHA MOJA YAELEZA MENGI. Kwa mimi ambaye ndio kwaanza nimemaliza darasa la Photography Appreciation, naona mengi "ya kuvutia"

Wewe waona nini na waonaje?

10 comments:

emu-three said...

Mhhh, kanzu, halafu bia...sijui kama ni `fashion' lakini nasikia kuna `pombe isiyo na kilevi'...lol

Mzee wa Changamoto said...

Ndugu.....
`pombe isiyo na kilevi'?
Mmmmmhhh!!!

Goodman Manyanya Phiri said...

Yako mawili. Wale wameoza. Au ni waungwana wasiyotaka kumwaibisha mwenye shughuli kusema : "Ondoa biya zako, Bwana!"

Rachel Siwa said...

Nimeishiwa maneno!!!!!vilaji na vinywaji na maombi!!!!!!!.

Simon Kitururu said...

Tukumbuke tu kuwa Yesu alikuwa anatengeneza MVINYO ambao kwa ukali ni zaidi ya mara mbili ya Bia walizo nazo !

Hau hamsomi BIBLIA mshangaao waombao wakati kuna bia mbele ?

Simon Kitururu said...

Nimerudi tena nje ya topiki:

Kuhusu ile quotation yako pale juu pembeni kwenye blogu yako ,....

...Hii : `` "There is NO IN-BETWEEN RIGHTEOUSNESS AND EVIL, so make your choice."
Jephter Washington McClymont (LUCIANO) ´´

Sijui kwanini inaniwazisha sana hasa kwa kuwa sijui kwanini sina uhakika na hilo!

Naendelea kuwaza !:-(

John Mwaipopo said...

natamani ningalikuwapo hapo maana hizo zimeombewa kabisaa, tofauti na zile tunazoagiza kaunta. au siyo simoni

Simon Kitururu said...

@Mr Mwaipopo: Si ndio hapooo!:-(

Unknown said...

Kumbe kweli mmetii kuweka maoni hapa. Nilichokiona hapo ni HAWAJUI WALITENDALO.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

ona yalivyofumba macho! chwekao kuli. nebinwa