Sunday, April 3, 2011

Baada ya HAPA, ungewaza nini?

Juma hili nimeona TUSHIRIKIANE kwenye KUWAZA ni nini ambayo wenzetu waliwaza baada ya KUNUSURIKA kwenye hali ama ajali kama hizi? Wengine walifanya UJINGA kwa "kujiegesha" na wengine "yaliwakuta" wakiwa kwenye habari nyingine. Tazama kisha WAZA kuwa baada ya hapa WALIWAZA NINI? Hasa huyo wa dk ya 2:21? Ama kweli KILA ROHO ITATOKA WAKATI WAKE UKIFIKA
Kisha tumuwaze "mtemi" huyu ambaye aliamini kuwa ni M'BABE kwa mwenzake. Lakini baada ya kupewa muda wa kuacha uovu aliokuwa akiufanya na kushindwa kufanya hivyo, akapewa FUNDISHO LA VITENDO
***"Waliwaza nini ni kipengele cha kuelimishana tukifurahia. Hiki kitakuwa kikikuletea habari za kweli na kushangaza kuhusu watu ambao wamefanya yale ambayo unaweza kujiuliza kuwa WALIWAZA NINI? wakati wanatenda haya. Kitakuwa na habari fupifupi kutoka ulimwenguni kote. Kwa habari zaidi kuhusu kipengele hiki BOFYA HAPA"***

1 comment:

Simon Kitururu said...

Atakayejibu WALIWAZA nini atakuwa anabunia tu hilo. AU?