Saturday, April 23, 2011

Labda UTUPU kwetu watokana na U-TUPU wa fikra zetu.

Ni majuzi tu wakati napitia kibaraza cha Mzee wa Duh!!! Simon Kitururu nikakutana na "topiki" kwamba "....May be hakuna mtu Open Mided aisee (irejee hapa)" nami nikawaza kwanini awaze hayo? Kisha nikawaza labda kila anayeweza kujua kuwa kuna uwezekano wa kuwepo na kutokuwepo OPEN MINDS, huyo atakuwa na OPEN MIND japo anaweza kuitumia kuwaza kwamba HAKUNA ALIYE OPEN MINDED.Hiyo ikawa CHANGAMOTO kuwaza upya juu ya kile kilichopo nyuma ya pazia kwa mtu awazapo.
Ni kweli kwamba kuna kitu kibaya na kizuri ama ni mtazamo wa mtu juu ya ubaya na uzuri huo? Nimewaza jinsi watu walivyomuamini Mch ambaye alikuwa mlawiti wakati huo akiwa mtendaji wa hayo mabaya, halafu wakaja kumtenga baada ya kuwa ametubu na kuacha tabia hiyo.
Kwani hapa mtu huyu anatengwa kwa yale atendayo, ama yale yajulikanayo juu ya matendo yake? LABDA wasingejua wangeendelea kumuona kama MTAKATIFU, na sasa wamejua, na yeye kaumbuka na katubu na AMEKUWA MPYA tena, wao ndio wanamtenga.TUACHANE NAYE..............
Ukiitazama hii picha hapa chini unaona nini? Kwani ingekuwa ndani ya uwezo wako ungenunua? Na pengine unadhani ni USANII AMBAO UNGEWEZA KUU-SUPPORT?
Ukimaliza kujibu, angalia "making" yake HAPA iliyochukua masaa 24. Na baada ya kuona uhalisia wa kilichomo, unasemaje?
Kwani kuna kilichobadilika? Ahaaaaa...Yawezekana. na kama ndivyo, ni kwa kuwa fikra zako zimewekwa wazi, zimefunuliwa, zimeanuliwa, ZIMEWEKWA TUPU. Na kwa uTUPU huo umeweza kuona ambacho hukuona na sasa umekuwa na mawazo mengine.
Labda ni kweli kwamba UTUPU MAWAZONI KWETU UNATOKANA NA U-TUPU WA FIKRA ZETU.
Nawaza kwa sauti tuuu!!!!!

6 comments:

Ebou's said...

Yeahh inaonekana waziii dada wa2waliokamatwa mabega na dada alie mbele kaacha sehemu ya kopa yenye alama ya upendo wazi katika sehemu ya pua.. yani niliangali mpaka kuifahamu macho yameingia ndani kiasi flani...

Simon Kitururu said...

Mmmmh!

Yasinta Ngonyani said...

Wakati mwingine ni vizuri kuwaza kwa sauti..nimeangalia na naona taswira ya chui tu kwa kweli na mwisho macho yangu yameishia kutokwa na machozi kwa kuangalia mno....

Mzee wa Changamoto said...

Yasinta, sasa copy hii link kisha fungua utaona CHUI HUYO NI NANI

http://2sao.vn/p0c1052n20110421105147046/ve-tranh-3d-tren-co-the-nude.vnn

Rachel Siwa said...

Naona chui na sharubu zake tuu!

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Leo mimi niko "close-minded" na sitaki kufikiri mambo ya utupu wa fikra wala nini.

Nataka tu kuchukua nafasi hii kukutakia pasaka njema wewe pamoja na familia yako. Msalimie Ariana !!!