Thursday, September 1, 2011

Them, I &Them....NO LOVE.....Nasio

"They talking about Love, yet they got no love at all, talking bout peace, yet all i see is war. You talk about this, you talk about that. Poor people just a suffer (are suffering) while you live out FAT" Ni maneno toka kwake Nasio Fontaine Mmoja wa wanamuziki wa Roots Reggae ambaye amesimama imara katika kutetea haki za wanyonge, kufumbua maovu ya viongozi na watawala na kufundisha njia m'badala za kujikomboa kwa tabaka likandamizwalo.
Namzungumzia Nasio na wimbo huu No Love Ijumaa hii kutokana na yale yaliyotokea wiki za karibuni na hata miezi kama sita iliyopita barani mwetu. Kuanzia "mapinduzi" ya viongozi wakongwe mpaka hali tete ya KUTOJALI wananchi nchini Tanzania. Tumeona viongozi wanavyosimama na kuzungumza kuhusu amani ambayo hawaonekani kuwa na nia ya kuisaka. Wanakwenda mikutanoni kuendesha vikao vya amani wakilipwa pesa nzuri na kuota vitambi wakati amani izungumziwayo haipo na wenye uhitaji wakiendelea kutaabika na machafuko hayo. Wengine bila hata aibu wanasema mapigano hayo wanayaleta kutaka kuleta Demokrasia nchini mwao na ndio maana Nasio kwenye wimbo huu akasema "you coming with your bribes and treachery to murder in the name of democracy. You living in your false pride and Luxury, while millions (are) dying in their poverty"
Wanapoomba kura (kwa wale wanaoomba kura) wanakuwa na ahadi mbalimbali zenye kuwapa matumaini watu. Wanaahidi yale ambayo hawawezi kutekeleza wakijua wazi kuwa maslahi yao yanatangulia mbele na ndio maana hawajali vifo na ukimbizi utokanao na yale wafanyayo. Hawajali mahitaji ya wananchi wao na hata MAENDELEO YAO. Tunaona mgao ukiendelea kila uchao, majengo ya gharama yakijengwa na waheshimiwa punde baada ya kuingia "mjengoni"na pia "biashara kama awali". Kwani kuna tofauti gani ya kiongozi anayeua wananchi wake kwa mtutu wa bunduki na yule anayesababisha vifo vyao kwa kutowapatia huduma muhimu kama za afya? Niliwahi kuandika kuwa "kama haya ndiyo mapenzi waliyonayo viongozi wa nchi zetu kwa nchi zao, kiasi kwamba wako tayari kuwaua ili waendelee kuwa madarakani, basi tuchague wanaozichukia nchi zao". Nalo hili Nasio aliliona aliposema "The wickedman ain't got no love for humanity, yet they got so much love for their vanity. Their need for way is rising high, while the sufferers are left to die (in starvation and hunger). Vote for me i'll set you free, are lies and hypocrices"
Nawasikiliza viongozi walivyoanza fitna na majungu ya kujifanya wanachukua kila hatua kusitisha machafuko yaendeleayo barani Afrika kwa kupanga safari nono za kwenda kujadili amani isiyopatikana. Hao NATO walitoa msaada wa silaha kwa "waasi" na sasa kunaanza pilika za kuzirejesha kwenye "mikono salama" kwani haijulikani mwenye nazo ana uwezo gani wa kufikiria yaliyo sahihi na kufanya yaliyo mema kwa "silaha hizo za misaada". Ni ipi TAFSIRI YA AMANI? Na ni vipi amani itarejea nchini Libya iwapo wenye silaha si watu wa kuaminika?
Kama alivyosema Nasio, nami ndivyo niaminivyo kuwa LOVE AND LOVE ALONE WILL CONQURE na sina shaka kuwa wenye kuanzisha haya kwa manufaa yao siku yao yaja.
Pole kwa wale wote ambao kwa tamaa za viongozi wao wamejikuta wakiwa wahanga wa machafuko ya namna moja ama nyingine.
Unaweza kujua mengi juu ya Nasio Fontaine kwa kubofya http://www.nasioreggae.com/main.html

**Them, I & Them ni kipengele kikujiacho kila Ijumaa kinachoelezea kazi za wasanii (Them) kulingana na maono yangu (I) kwa ajili na manufaa ya hadhira (Them)**
Kwa nyimbo zaidi ndani ya kipengele hiki bofya hapa.IJUMAA NJEMA

5 comments:

emu-three said...

Amani yupo, lakini inavyoonekana watu wanampenda Ubinafsi zaidi. Haki naye kila akitaka kuingia ndani , mkuu wa ulinzi Chuki anamzuia, sasa sijui kama tutafika.
Ujumbe wake ni safi sana kwa wenye kufikiri. Shukurani . Tupo pamoja

Simon Kitururu said...

Ijumaa njema Mkuu!

Maisara Wastara said...

Ni miezi kadhaa na masiku mengi tu sijaonekana katika tasnia hii ya blog.
leo nimerejea tena. Nawaahidi mambo mazuri, karibuni kibaraza cha Tegelezeni. Tupo Pamoja.

Unknown said...

Amani ni hali ya raha na salama bila ugomvi; ni kinyume cha fujo au vita.

Mara nyingi hali za amani ya nje na amani ya ndani hutofautishwa.

Amani ya kisiasa ni hasa kutokuwa na vita na mapigano kati ya nchi mbalimbali au kati ya vikundi ndani ya jamii.

Kama kuna mgongano kutokana na tofauti ya upendeleo juu ya jambo fulani amani inatunzwa kama pande zote zinafuata sheria au kanuni za jamii bila kutumia mabavu.

Mara nyingi maana kuu ya "amani" ni hali ya kutokuwa vita kati ya nchi kwa sababu vita huleta uharibifu mkubwa kushinda aina nyingine za ugomvi.

Amani inaweza kutaja pia tendo la kumaliza vita kwa njia ya mapatano kati ya washiriki wa vita au pia kati ya washindi na washindwa wakikubali kumaliza uadui. (linganisha Amani ya Westfalia).

Tangu vita kuu za dunia kulikuwa na majaribio mengi kuhakikisha amani kwa njia ya mapatano kati ya nchi zote za dunia.

Shirikisho la Mataifa lilianzishwa mwaka 1919 likashindwa kuzuia vita kuu ya pili ya dunia ikafuatwa na Umoja wa Mataifa ulio na shabaha ya kupunguza na kuzuia vita kwa njia ya ushirikiano.

Tangu kale watu waliona ya kwamba amani ya nje inaenda sambamba na amani ndani ya kila mtu. Penye hasira nyingi mioyoni mwa watu ni vigumu kutunza amani ya nje.

Kwa sababu hiyo amani imekuwa ni jambo muhimu katika dini na falsafa.

Dini mbalimbali zina ujumbe kuhusu amani:

* ndani ya roho wa mtu mwenyewe
* kati ya Mungu na mwanadamu
* kati ya watu

Maria said...

kwa kila kinachoendelea huko Libya, waasi kujidai kushangilia mitaani bila kujali waliouawa mpaka sasa, kuna wakati sielewi hao wanaoendelea kufa kwa sasa wakati waasi wanatamba wameshashinda wanauliwa na nani? as usual Africa lazima kuwe na machafuko..kukionekana kimya tu lazima vurugu zianze...nchi ngapi zina vurugu hatusikii NATO wako angani wakituliza..kwa mara ya kwanza nasikia waasi wanatetewa na kupewa silaha..the whole thing makes you wonder if it is really about democracy and peace or money, power and stealing...hao waasi wakato wenzao wako kwenye mapigano wao wako ndani ya ndege kutembelea mataifa makubwa (sijui kwa nini hawakwenda kwenye nchi za kiafrika)..kwamba wamechaguliwa na wenzao kuwawakilisha na kuomba kutambuliwa..nchi iko kwenye machafuko walikaa saa ngapi kuchaguliwa? as usual wanaume 30 utadhani nchi ina wanaume pekee au wanaume pekee ndo wenye akili na uwezo wa kutawala..