Sunday, January 1, 2012

Steina Mrema aagwa.

Watanzania na jamii zao kutoka miji ya karibu na Washington DC leo wamejumuika kwa wingi katika ibada ya kumuaga ndugu, rafiki na mpendwa wetu Steina Mrema.
Ibada hiyo ilifanyika katika kanisa la Cathedral Of Praise lililopo mji wa Lanham, jimbo la Maryland. Mtoto wa Marehemu akiwa na Mama yake wakitoa heshima kwa Marehemu Steiner. Baada ya hapo, ndugu, jamaa na marafiki walipita kutoa heshima zao za mwisho. Rashidi Mkakile, Stephano Mhina na George Mwasaliba wakitoa heshima zao za mwisho kuuaga mwili wa marehemu Steina Mrema.Sunday Shomari, akitoa heshima za mwisho kwa Marehemu Steina Mrema.

Baada ya mwili kuondoka, ulifuata wakati wa chakula na mazungumzo, nami nikabahatika kumpata rafiki wa muda mrefu na wa karibu wa Marehemu Steina Mrema ambaye alinieleza machache kuhusu Marehemu. Karibu umsikilize

SHUKRANI KWA WOTE WALIOSHIRIKI KATIKA KUFANIKISHA HILI.
MUNGU AWATANGULIE NDUGU WATAKAOSINDIKIZA MWILI KWA MAZIKO NYUMBANI TANZANIA.

2 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Bwana alitoa bawana ametwaa. Marehemu astarehe kwa amani.

Rachel Siwa said...

Poleni sana wafiwa, Mungu awatie nguvu kwa wakati huu mgumu kwenu.Mwanga wa Milele umwangazie eeBwana.....