Thursday, April 19, 2012

Alex Kajumulo.....Nabii asiyekubalika kwao?

Alex Kajumulo akiwa studioni kurekodi moja ya kazi zake.
Ni kati ya watu wanaofahamika kwa michezo zaidi. Wengine wanamfahamu kama mfanyabiashara / mjasiriamali, lakini HESHIMA ya Alex Kajumulo duniani ipo zaidi kwenye fani ambayo wengi wa waTanzania hawamtambui kwayo.......MUZIKI.
Akiwa na bendi yake ya BUSHMAN, Alex, aliyeanza kupenda muziki akiwa "bwana mdogo" kijijini Bukoba sasa anafanya vema katika anga za muziki dunia nzima na kuwa msanii wa kwanza toka barani Afrika kusikika katika vituo vinavyopiga mahadhi yote.
Lakini si hilo tu, Alex Kajumulo ameweza kuingia katika fainali za shindano la kimataifa la watunzi wa nyimbo duniani linalojulikana kama International Songwriting Competition.
Unaweza kuona jina lake KWENYE MAHADHI YA "WORLD" KWENYE ORODHA HII ambapo ni yeye pekee aliyeingia fainali kutoka barani Afrika.
Katika shindano hilo ambalo washindi watatangazwa mwishoni mwa mwezi huu ama mwanzoni mwa mwezi ujao, wasikilizaji wanaweza kupiga kura kwa kupitia ukurasa huu wa Facebook
Hivi karibuni nilipata bahati ya kuhojiana na Alex akiwa nyumbani kwake Seattle Washington na kujadili suala la muziki tuu. Na HAPA anaeleza safari yake kimuziki, mashindano aliyowahi kushiriki, mafanikio na hata mafanikio yake.
Unaweza kutembelea TOVUTI YAKE HAPA
Karibu usikilize mahojiano yetu

3 comments:

Alpha Ferries. said...

Safin sana Babukaju!

emuthree said...

Mkuu tupo pamoja,nimeipata hiyo

Unknown said...

Ahsante sana mzee wa changamoto yetu.