Saturday, April 7, 2012

NIONAVYO MIMI...Habari za utafiti wa "Kikombe cha Babu" ni upotoshaji

ONYO:
Usisome hapa kama huna muda wa kutosha "kumeng'enyua" kiandikwacho

Siku tatu zilizopita, Gazeti la Serikali la Habari Leo liliripoti hapa kuwa "Waliopata ‘Kikombe cha Babu’ wafariki dunia".
Katika habari hiyo ambayo KICHWA CHA HABARI HAKIAKISI UHALISIA WA MAUDHUI YAKE, waandishi wamesema "Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ambayo sasa itatangaza matokeo ya utafiti wa tiba hiyo ya ‘Kikombe cha Babu’ imesema wengi ni wale wenye Ukimwi walioacha matumizi ya dawa za kurefusha maisha (ARVs).

Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Regina Kikuli, aliiambia Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) jana Dar es Salaam, kwamba hadi sasa Serikali inafanyia utafiti watu 206 ambao walipata kikombe hicho."
Ukisoma kichwa cha habari (Waliopata ‘Kikombe cha Babu’ wafariki dunia) kisha ukasoma kilichoandikwa ndani utagundua utata na mapungufu (kama sio upotoshaji wa makusudi) wa habari hii.
KWANZA.
Kwa mujibu wa Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Regina Kikuli aliyenukuliwa katika habari hiyo, "Serikali inafanyia utafiti watu 206 ambao walipata kikombe hicho". Na kisha, habari hiyo ikaongeza kuwa “Kwa sasa ni vigumu kusema dawa hiyo inaponya au haiponyi, tusubiri utafiti wa kitaalamu. Baada ya miezi miwili tutatangaza matokeo kwa umma,” alisema Kikuli na kuongeza kuwa utafiti huo unafanywa katika hospitali mbalimbali nchini chini ya usimamizi wa Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR).
Lakini uwiano huu ni wa watu 206 kati ya wangapi?

Taarifa hiyo imesema "Kaimu Mganga Mkuu wa Serikali, Donan Mmbando, alikiri kuwa wagonjwa wengi wa Ukimwi waliokwenda kupata tiba hiyo na kuachana na ARVs wamepoteza maisha."
Na hili linanipeleka kwenye swali langu la pili kuwa WALIFUATA MASHARTI YA TIBA YA BABU?
Mara kadhaa, Mch Mwasapile amekaririwa akisema kuwa WATU WASIACHE MADAWA WANAYOTUMIA KWA KUWA WAMEPATA KIKOMBE, na kwa maana hiyo, kama watu waliendelea kutumia dawa zao, na wakafa (hasa wale wa wanaofanyiwa uchunguzi), ni kipi kitakachoonyesha kuwa wasingeitumia wasingekufa ama wangeishi zaidi ya walivyoishi baada ya kunywa dawa hiyo?
Ukweli ni kuwa kama walikuwa wakitumia dawa zao za awali na ya Babu, basi hakuna ushahidi kuwa kilichowaua ni DAWA YA BABU, lakini pia kama waliacha kutumia dawa zao baada ya kutumia kikombe cha babu, basi WAMEKIUKA MASHARTI.
Lakini ni wangapi waliokufa baada ya kunywa kikombe hicho?
Idadi hiyo ni asilimia ngapi ya wote waliokunywa dawa yake?Walioenda kwa Babu wa Loliondo ni Mamia ya maelfu ya watu, na bado wanakwenda, kwa hiyo ningeomba ripoti hiyo itakayokuja ifanye kitu hicho hicho kwenye hizo hospitali za Bugando, Mwanza; Mbeya; Mount Meru, Arusha; Hydom, Manyara na KCMC, Kilimanjaro ambako uchunguzi huo unafanyika kwa kukusanya idadi ya watu sawa na wale waliokwenda kwa "Babu", kisha fuatilia kati ya hao watu, na ndani ya muda ambao "Babu" alikuwa akitoa matibabu Loliondo, ni wangapi walikufa (Hospitalini na nyumbani) kisha tujue kama ni kweli kuwa waliokufa kwa baada ya kutumia dawa ya "Babu" Loliondo ni wengi kuliko wale wanaokufa kwenye hospitali zetu "kubwa".
Tusisahau kuwa safari ya Loliondo ilihusisha wale ambao walishakata tamaa na walishatoka hospitali.
Kwa Maana nyingine, "Loliondo kwa Babu" kulikuwa kama HOSPITALI BAADA YA HOSPITALI YA RUFAA.

Lakini pia zi-wapi SHUHUDA KAMA HIZI za wale waliopona ama kupata nafuu baada ya kutumia dawa hii?
Ni kweli kuwa watu mia mbili na sita kati ya laki kadhaa walioenda kutibiwa (tena wenye maradhi sugu) watatoa "sample" sahihi juu ya matibabu haya? Dadangu Jestina George alipokuwa akichangia kwenye mjadala huu tuliokuwa nao jana kwenye ukurasa wa Facebook akatoa maoni ambayo naamini kama yatazingatiwa, italeta taswira nzuri zaidi kwenye mchakato huu. Alisema "Na vifo vingi vilitokana na hali ya jinsi ya kufika kule maana kulikuwa na tabu sana ya usafiri na pia ques were long. Mtu anatoa ndugu yake hospital aliye kuwa mahututi alitegemea nini? "
Bado naamini kuwa utafiti huu si makini na NIONAVYO MIMI......HABARI ZA UTAFITI WA KIKOMBE CHA BABU NI ZA UPOTOSHAJI

Na huu ni MTAZAMO wangu kwa namna nionavyo tatizo....
Labda namna nionavyo tatizo, ndio tatizo.

3 comments:

Anonymous said...

i have two relatives who went there and drink, but eventually all two died. this is not science,it is not a human wisdom which you can try to explain or please anyone, they die, and after that, all the questions die.. do youyr research...to get that link.. with your human wisdom..until the last day, i tel you...there is spiritual engagement which entangles them...the deaths a mysteriously presented,, after a fatal long illness.there after..

Anonymous said...

i have two relatives who went there and drink, but eventually all two died. this is not science,it is not a human wisdom which you can try to explain or please anyone, they die, and after that, all the questions die.. do youyr research...to get that link.. with your human wisdom..until the last day, i tel you...there is spiritual engagement which entangles them...the deaths a mysteriously presented,, after a fatal long illness.there after..

Mzee wa Changamoto said...

Thanks Dr Cosmas.
I really wish i understood what you were trying to say.
If you read carefully, i wrote " Ukisoma kichwa cha habari (Waliopata ‘Kikombe cha Babu’ wafariki dunia) kisha ukasoma kilichoandikwa ndani utagundua utata na mapungufu (kama sio upotoshaji wa makusudi) wa habari hii."

Let's debate points in details (if any) and not being VAGUE bout the whole issue.