Thursday, April 26, 2012

Pongezi za Muungano kutoka Ubalozi wa Tanzania Marekani

 
MIAKA 48 YA MUUNGANO 

PONGEZI KWA WATANZANIA WAISHIO MAREKANI NA MEXICO

 Nanapenda kuwapa pongezi Watanzania wenzangu waishio Marekani na Mexico tunaposherehekea miaka 48 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Kwa niaba yangu binafsi na kwa niaba ya wenzangu hapa Ubalozini nawatakia Watanzania wote heri na fanaka ya siku hii muhimu katika historia ya nchi yetu. Aidha, tunaposherehekea sikukuu hii, natoa wito kwa Watanzania wote kuendeleza udugu na mshikamano wetu, ili muungano wetu udumu na taifa la Tanzania lizidi kusonga mbele. 

Mwanaidi Sinare Maajar 
Balozi wa Tanzania Marekani na Mexico 
Washington, DC. 
April 25, 2012

No comments: