Saturday, May 12, 2012

Kwenu kinamama wema.....

ASANTENI......MAISHANI MWANGU, hakuna asiye na umuhimu. Na kila mtu anawajibika kwa namna moja ama nyingine katika ukuaji wangu japo umuhimu na ukuaji huo waweza kuwa ama kuja kwa aina na malengo tofauti. Vyovyote iwavyo, na vyovyote ijavyo, "mwisho wa siku" nakuwa nimejifunza kitu / vitu na kuerevuka zaidi ya nilivyokuwa kabla.
NDIVYO NIFAHAMUVYO KUHUSU MAISHA.
Lakini pia lazima nikiri kuwa maisha yangu ya kila siku yamekuwa zao na endelezo la KINAMAMA ambao katika ngazi na matukio mbalimbali maishani, wamekuwa sehemu kubwa ya suluhisho. Simaanishi kuwa kinababa hawapo (kwani kinamama hawa wamekuwa walivyo kutokana na kinababa walio upande wao. Lol), lakini kwa kuwa leo ni siku ya kinamama hapa Marekani (naamini haiadhimishwi pamoja duniani kote), naomba nizungumzie nafasi yao maishani mwetu.
Tarehe 5 Aprili, 2009 niliandika makala yenye kichwa cha habari Ni mbegu ndogo iletayo mazao makubwa (irejee hapa)
Na habari hiyo iliyomhusu Daktari bingwa wa upasuaji ulimwenguni Dr Benjamin Carson. Katika makala hiyo, nilieleza kile nilichosikia na kusoma katika toleo la kipengele cha THIS I BELIEVE kipindi cha Morning Edition kirushwacho na Radio ya jamii hapa Marekani ya NPR. Unaweza kusikiliza alichokisema katika kipindi hicho kwa ku-bofya hapa.
Post hiyo iliandikwa miezi sita na siku tisa kabla nami sijawa mhanga wa kazi ama shughuli hii nzuri ya ulezi.
Licha ya kuwa mlelewa na kuona njia njema za malezi toka kwa wazazi na walezi wangu, haikuwa sawasawa mpaka nami nilipoingia jukumu lisilo la hiari la ulezi. Na hapo ndipo nilipoona uzuri, ugumu na ama umuhimu wa malezi bora kwa yule umleaye.
Nakumbuka katika Salaam zangu za siku ya kinamama duniani (hapa) niligusia umuhimu wa kinamama. Natambua malezi si ya mwanamke pekee kwani nasi kinababa tunaongeza heshima na thamani ya wanawake kwa kile wanachotubariki nacho, ina maana tunaongeza mapenzi na msaada kwao na kujishughulisha zaidi katika malezi. Ina maana kwa kuamua kumuona mwanamke kwa namna iliyo bora zaidi, tunaongeza msaada wa malezi kwao na kuboresha malezi kwa mtoto.
Wapo waliotangulia wakasema "harder the battle, tougher the fight, sweeter the victory". Na naamini mchakato mzima wa malezi ndio UTAMU WAKE na kwa waliofanikisha suala la malezi wanaweza kuamini kuwa katika KUWEKEZA KWENYE MALEZI, TUNASAIDIA KUKUZA MWANA NA KIJANA / BINTI ALIYE MWEMA AMBAYE NDIYE ATAKAYEKUJA KUWA MSAADA KWA JAMII.
Na kwa kuwa wanajamii wote wanaanzia utotoni, basi lazima tujue kuwa UZAZI NA MALEZI ni KAZI BORA ZAIDI na ni msaada mkubwa kwa jamii ijayo.
WAKATI NATHAMINI KAZI KUBWA IWEKAYO HADHI YA U-MAMA KWA KINAMAMA WEMA na hasa rafiki zangu sana na "mama wapya" Msia na Elinita, naomba uungane naye kusikiliza kibao hiki mwanana cha Darius Rucker kuhusu makuzi na malezi na yanavyopita. Anaonesha ama kueleza namna ambavyo kile tunachoona ni karaha katika malezi ya sasa tutakavyokumbuka baada ya muda mfupi. 
Na hili ni jingine linalofanya MALEZI KUWA KAZI BORA SAANA MAISHANI
HAPPY MOTHERS'DAY
He didn't have to wake up
He'd been up all night
Layin’ there in bed listenin’
To his new born baby cry
He makes a pot of coffee
He splashes water on his face
His wife gives him a kiss and says
It gonna be OK

It won’t be like this for long
One day we'll look back laughin’
At the week we brought her home
This phase is gonna fly by
So baby just hold on
‘Cause it won't be like this for long

Four years later ‘bout 4:30
She's crawling in their bed
And when he drops her off at preschool
She's clinging to his leg
The teacher peels her off of him
He says what can I do
She says now don't you worry
This’ll only last a week or two

It won’t be like this for long
One day soon you'll drop her off
And she won’t even know you're gone
This phase is gonna fly by
If you can just hold on
It won’t be like this for long

Some day soon she'll be a teenager
And at times he'll think she hates him
Then he'll walk her down the aisle
And he'll raise her veil
But right now she's up and cryin’
And the truth is that he don't mind
As he kisses her good night
And she says her prayers

He lays down there beside her
‘Til her eyes are finally closed
And just watchin’ her it breaks his heart
Cause he already knows

It won’t be like this for long
One day soon that little girl is gonna be
All grown up and gone
Yeah, this phase is gonna fly by
So, he's tryin’ to hold on

‘Cause it won’t be like this for long

It won’t be like this for long

It won’t be like this for long

2 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Akina mama wote HONGERENI SANA na Asanteni sana. Mnafanya kazi nzuri sana na kumbukeni tunaweza kuliko tunavyoamini. Akina mama OYEEEEEEEEEEEEEE

emuthree said...

Mkuu tupo pamoja, ndio hata mimi nikakumbuka kila kisa cha nani kama mama; http://miram3.blogspot.com/2011/01/nani-kama-mama-1.html