Monday, July 16, 2012

Anarejea...

Ni mmoja wa watangazaji waliopata kunivutia sana.
Kwa lugha fasaha na hata "mtindo" wa utangazaji. Nikiwa mtangazaji "mchanga" (mwanzoni mwa miaka ya 2000), alikuwa akinguruma kituo cha Clouds FM na hakuna anayebisha kuwa alikuwa akishirikiana vema na timu yake "kukimbiza" vipindi.
Akaondoka "hewani", lakini baada ya kimya cha muda mrefu, anasema ANAREJEA.
Namzungumzia Fina Mango.
Anarejea ndani ya MAGIC FM kuanzia Agosti 4.
Natamani kumsikia, kujua kama kweli...KIMYA KINGI KINA MSHINDO MKUU.

Karibu Dada, karibu TENA.
Na naamini utadhihirisha ukomavu wako "hewani"

No comments: