Sunday, August 5, 2012

Kizazi...Nini kipimo chake? Wakati, Mazingira ama Nyenzo?

Photo Credits: Jack Graham Blog
Labda wapo wanaoshangaa kuwa mtu na mzazi wake wanahesabika kuwa watu wa vizazi tofauti licha ya kwamba wote wako hai.
Wengine wanakubali kuwa wao na wazazi na wazazi wa wazazi wao ni vizazi tofauti licha ya kwamba wote wako hai.
Lakini wapo ambao pengine bila kufikiria wanaamini kuwa kila UZAO ni KIZAZI.
Na pia wapo ambao wanaamini kuwa yachukua miaka mingi kutoweka kwa kizazi kimoja kwenda kingine.
Kwani kila siku si tunasikia muziki huu wa "bongo flava" ukiitwa muziki wa kizazi kipya? Hata kama anayeuimba amevutiwa na muziki miaka michache iliyopita baada ya kumsikiliza "mkongwe" ambaye (kwa tafsiri "yao") si mtu wa kizazi chao?
Hujasikia wasanii wakirudia nyimbo za miaka kadhaa iliyopita na kusema wamezirudia katika MUZIKI WA KIZAZI kipya katika harakati za kutenga kizazi cha "remix" na MUZIKI HALISI?
ACHANA NA HAYA....
Juzi tukiwa shuleni katika kujadili KIJANA NA TEKNOLOJIA, binti mmoja akasimama na kuchangia akisema "maisha yangu yote sasa ni elektroniki. Ndio kalenda, kumbukumbu, miadi, barua, simu, sauti nk. Vyote nafanya kwenye simu yangu ya Iphone." Hapo mie nikawa natikisa kichwa kukubaliana naye. Kisha akasema KWA KIZAZI CHA SASA HUWEZI KUISHI BILA NYENZO KAMA IPHONE.
Hapoooooooooooooooo sasa....Sikusubiri "kunyoosha mkono"
Nikamuuliza kuwa anaamini kuwa kila pembe na mtu / kijana wa rika yake anaijua Iphone achilia mbali simu hata ya kukoroga?
Nikamuuliza anaposema KIZAZI CHA SASA anamaanisha katika nyumba, kijiji, mkoa ama jimbo analoishi ama anamaanisha ULIMWENGU MZIMA?Ni kweli kuwa binti huyu wa miaka 18 wa hapa Maryland yupo kwenye kizazi tofauti na binti ya jirani yetu mwenye miaka 18 pale Bushasha? Kama wana umri sawa, si wako kizazi kimoja? Lakini kama hawatumii nyenzo moja kutokana na mazingira, ina maana mazingira ni kigezo? Na je, ni kweli kuwa "Uncle" nanilii anayetumia kompyuta saana pale Bongo atakuwa katika kizazi sawa na haka kabinti ka hapa kwa kuwa nyenzo zainawaweka kwenye "usawa" wa matumizi?
Ndipo nilipopata wazo la kuja kuuliza hapa kwamba KIZAZI....KIPIMO CHAKE NI NINI? NI WAKATI, MAZINGIRA, AMA NYENZO?
Labda nikuonyeshe tu kuwa.....................Hawa hapa chini
Photo Credits: Broadcasting Corporation of China
Ni wanafunzi wa elimu ya awali kama ilivyo kwa hawa hapa chini.
JE!! Japo wanaweza kuwa na umri unaolingana ama kukaribiana, unaamini wako katika KIZAZI KIMOJA?
Kwani kizazi ni nini?
Innocent Galinoma aliuliza "what is life? Is life a gift, or a test, or a punishment for my people?"
MSIKILIZE

JUST THINKING OUT LOUD.
 NB: MARUDIO YA FEBRUARI 23, 2011

1 comment:

Ebou's said...

Mhh kaka hii nikuwana watunzi wamanenoambao hawafikiri ni nini maana halisi ya kizazi kimpya kama ni wakati, nyenzo au Mazingira, ambao hao watunzi wamesemo ya Kizazi kimpya nao pia wamekulia katika mazingira yenye nyezo zinazokwenda na wakati. hapo jibu ninaweza kusema Mazingira tafauti!