Sunday, August 26, 2012

Matawi ya vyama vya siasa DIASPORA….DALILI NZURI, “MADENI” ZAIDI

Hatimaye ufunguzi wa tawi la CCM hapa Washington DC umefanyika Jumamosi ya Agosti 25 mwaka huu ikiwa ni siku 100 kamili tangu kufunguliwa kwa tawi la CHADEMA hapa.
Na kama ilivyoonekana kwenye taswira za ufunguzi wa matawi yote, IDADI YA WANACHAMA NI KUBWA.
Hiviii......Unaona UMATI MNENE kwenye uzinduzi wa tawi la CCM-DMV?
Photo Credits: Vijimambo Blog 
Na Je!!!...Uliona UMATI MNENE kwenye uzinduzi wa tawi la CHADEMA-DMV?
Photo Credits: Swahili Villa Blog 
Hii ni dalili nzuri sana.
Kwamba kuna namna nyingine ya kiITIKADI katika kuwaunganisha waTanzania wa jamii ya hapa Washington DC na vitongoji vyake. Na dalili iliyo nzuri zaidi, ni kuwa HAKUNA UHASAMA kati ya watu wa itikadi mbili hizi.
HONGERENI KWA HILO .
Na sasa tumeshuhudia uzinduzi wa matawi haya (kwa hapa DC na kwingineko) na kwa hakika tumeona IDADI ya kuridhisha kwa waliohudhuria uzinduzi wa vyama vyote, linalofuata (ama niseme LINALOTAKIWA KUFUATA) ndilo ninaloita DENI.
TANZANIA ina mahitaji mengi sana ambayo yanahitaji ushirikiano (hasa wa kimawazo) toka kwa watu wa “upande wa pili”. Ninaloamini ni kuwa IWAPO WATU WOTE HAWA KWENYE MIKUTANO YOTE HII WATAUNGANISHA NGUVU (HATA ZA MAWAZO) kusaidia matatizo ya Tanzania, TUTAFIKA MBALI.
Na hilo ndilo DENI KUU kwetu. Na ndio DENI KUU kwa viongozi wa matawi haya…KUUNGANISHA WANACHAMA WAO KUWEZA KUIJENGA TANZANIA YETU.
Nawatakia kila la kheri WANACHAMA NA VIONGOZI WOTE wa matawi ya vyama vya siasa katika DIASPORA.
Lakini nawakumbusha kuwa CHANGAMOTO YETU si kuwa na matawi mengi, ama wanachama wengi, bali kuwa sehemu ya suluhisho la matatizo yaliyoko nyumbani Tanzania na kwa kufanya hivyo, tutaona UMUHIMU WA MATAWI HAYA KATIKA DIASPORA.

Nawaza kwa sauti tuuuuuuuu!!!!!!!!! 

"POLITICS FIX" ni kipengele kinachozungumzia mambo ambayo blogu hii inaamini yanastahili kuwekwa vema katika siasa za nyumbani Tanzania, ama zinazoathiri Tanzania. Kusoma matoleo yaliyopita katika kipengele hiki BOFYA HAPA

1 comment:

emuthree said...

Tupo pamoja mkuu , twawatakia mafanikio mema, sisi huku sio matawi tu,tuna mpaka mashina, na huenda tukapata mti kamili, ila kufa hatufi cha moto tunakiona!