Monday, September 10, 2012

Ana kwa Ana na Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad


Mahojiano na Makamu wa kwanza wa Rais ZANZIBAR Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad.
Katika mahojiano haya, Mhe. Hamad anaeleza kile kilichomleta Marekani, hali ya kisiasa Zanzibar
Anajadili maridhiano ya mwaka 2009 na kufafanua ni kwanini alipigania kura za chaguzi za 1995, 200 na 2005 lakini sio 2010 ambapo wengi waliamini ameshinda ukilinganisha na chaguzi zilizopita?
Anazungumziaje dhana ya ukubwa wa serikali Zanzibar ukilinganisha na idadi ya watu wakena ni kwanini tuwe na Makamu wa Kwanza na Makamu wa Pili wa Zanzibar.
Nini kiini cha mgogoro wa sensa?
Na pia, kwa yeye kuwa sehemu ya serikali Zanzibar ilhali ni kiongozi wa chama cha upinzani Bara kunaleta mgongano wa maslahi?
Kwanini CUF inaonekana kupoteza mvuto nchini Tanzania?
Nini anazungumzia kuhusu mgogoro wake na Mhe. Hamad Rashid?
Zanzibar inakabiliana vipi na tatizo la ajira kwa vijana?
Je! Zanzibar ni nchi ya kijamaa ama kibepari?
Vipi anazungumzia tatizo la usafiri nchini Zanzibar?
 Elimu je?
Suala la Muungano lina utata gani?
Ni ipi tofauti ya Maalim Seif wa 1995 na huyu wa sasa?
Na mwisho nini wito wake kwa wote wamtazamao sasa?
Ungana nasi

1 comment:

Ebou's said...

Good job Mubelwa Bandio kama alivyosema Maalim Seif tatizo kubwa Zanzibar ni kuhusu ukosefu bora wa Elimu hata katika masomo ya Sayansi, hesabati, Engilsh, na Geografia, pamoja na uhaba wa walimu bora katika masomo hayo.

Vile vile ukosefu wa madawati, na mrundo wa mkusanyiko wa wanafunzi katika darasa moja, na tatizo la baadhi ya vifaa vya elimu ambalo nitatizo kubwa Zanzibar kwa hivi sasa.

Swali kwa Zanzibar Diaspora. Je Mtaisaidia vipi Zanzibar kwenye suali zima la Elimu ya Zanzibar ......?