Thursday, November 22, 2012

Ninashukuru kushukuru

Ndio..... 
Ninashukuru kushukuru kwa kuwa kila ashukuruye, yu-hai....
Ni siku nyingine ninayomshukuru Mungu kwa baraka za maisha tuliyonayo.
Na japo siku ya leo si tofauti sana na siku nyingine, lakini naungana na wale waliotenga siku ya leo katika kuifanya maalum kutoa shukrani hapa Marekani, yaani THANKSGIVING.
Nina kila sababu za kumshukuru Mungu kwa maisha yangu katika mwaka mzima tangu tarehe kama ya leo mwaka jana.
Ni mwaka ambao umekuwa na mengi na namshukuru Mungu yote yamepita na yote ni mema.
Kwanza namshukuru kwa maisha ya kila mmoja anizungukaye.
Ninyi mmekuwa sehemu ya MAENDELEO yangu. Iwe ni kwa "kunisukuma" kuelekea mafanikio ama "kunivuta" ili niongeze nguvu za kuyafuata mafanikio hayo.
Namshukuru Mungu kwa FAMILIA aliyonitunukia na zaidi nyongeza ya BINTI ambaye kaungana na Dadaye Paulina na kuleta faraja zaidi kwenye familia.
Natoa shukrani za ziada na pekee kwa Mama yao, ambaye amekuwa "NUSU NJEMA" kwangu.
Namshukuru Mungu kwa 
"Mshiko wa kwanza" wa Paulina kwa "Dada mdogo" Annalisa
Nimejaaliwa kuwa na familia nzuri na pana. Familia inayojumuisha NDUGU, JAMAA NA MARAFIKI ambao kwa hakika wamekuwa sio tu sehemu ya maisha yangu, bali BARAKA KWANGU. Mmekuwa nguzo kuu maishani mwangu. 
Nikiwa na Kaka-Rafiki Abou Shatry. Chief wa blog ya Swahilivilla na MPIGA PICHA MKUU WA JAMII PRODUCTION. Picha kwa hisani ya Swahilivilla Blog
Namshukuru Mungu kwa THAMANI ya kazi na maisha inayojidhihirisha miongoni mwa wengi sasa.
Shukrani na thamani kwa wale ambao wananipa nafasi ya kudhihirisha kilichomo ndani mwangu. Na kipekee kwa vituo vya Radio Pride Fm (Mtwara), Ebony FM (Iringa), Clouds FM na WAPO Fm (Dar) na kituo cha Chuo cha Howard hapa Marekani
Shukrani kwa TAASISI mbalimbali zilizoweza kuthamini michango mbalimbali iliyobarikiwa kukamilika mwaka huu kupitia kwangu.
Zaidi ni shukrani kwa Kanisa la The Way of the Cross Gospel Ministries ambao wamethamini mchango wetu wanahabarikama taswira hii hapa chini ilivyonyakwa na Kaka Luke Joe wa Vijimambo Blog
Nikitunukiwa cheti na Mch. Ferdnand Shideko kwa niaba ya Kanisa la The Way of the Cross Gospel Ministries. Hiki kilikuwa cheti cha kuthamini mchango wa uhabarishaji kwa wanahabari wa Washington DMV.
Pia kwawatu binafsi na makampuni ambayo yameendelea kuwa wawezeshaji wa harakati za maisha yetu ya kila siku pamoja na kufanikisha harakati za kusaka maisha kwa nia njema na aminifu.
Shukrani zaidi kwa Kampuni ya VIZION ONE ya hapa Washington DC kwa uwezeshaji mkubwa wa utendaji kazi wa Jamii Production.
Twaamini kuwa PUNDE tutaanza kuona matunda ya uwezeshaji huu.
Kitendea kazi kipya cha Jamii Production. Sehemu ya uwezeshwaji mkubwa wa kampuni ya VIZION ONE ya Washington DC
Nawashukuruwasomaji na wasikilizaji wa kazi zangu popote pale mlipo.
Nawashukuru WASHIRIKI WENZANGU katika kusaka, kutengeneza na kusambaza habari mbalimbali. Nanyi ni wengi mno na kwa hakika sitaweza kuwataja mmoja mmoja.
Lakini kwa umoja wenu, napenda mtambue kuwa ndio mnifanyao niwe nilivyo.
Nina mengi ya kushukuru. Na kwa hakika sitaweza kuyasema yote. Lakini napenda kusema kuwa NITAENDELEA KUTOA SHUKRANI KATIKA MAISHA YANGU kwa kuwa kila kitendekacho maishani kina sababu. Na kwa kuweka mtazamo chanya katika kile kikutokeacho, unaweza kujifunza jambo jema zaidi na kubadili kilio kuwa kicheko.
Na funzo la mwisho ni kuwa, kwa kuwa si rahisi kushukuru kila mtu kwa wakati mmoja, basi ni vema kumshukuru kila mmoja kwa wakati wake na kwa wakati akutendeapo jambo kwani hauna uhakika kuwa utapata nafasi ya kufanya hivyo pale utakapotaka kufanya hivyo.
Binafsi......NASHUKURU KUSHUKURU, KWA KUWA NI ISHARA KUWA NIKINGALI HAI
Give it all you've got...TODAY

ASANTENI.

2 comments:

Halil Mnzava said...

Nami nashukuru kwa kutushukuru.

Mungu akubariki wewe na familia yako.

Yasinta Ngonyani said...

Kweli nami nashema ahsante kwa kutushukuru nawe nakushukuru..