Saturday, February 2, 2013

Anna Mwalagho na wimbo wake mpya...WOMEN OF THE WORLD

Punde baada ya mahojiano humu ndani ya Asparagus Media Studios. Takoma Park, MD. U.S.A
Msanii mshairi maarufu mwenye asili ya Kenya Anna Mwalagho ametoa video yake ya kwanza.
Katika wimbo video hiyo, Anna ambaye amekuwa akishiriki katika maonyesho mengi hapa Marekani, amezungumzia masuala ya wanawake na namna ambavyo ni waJASIRI kuliko wanavyoamini.
Ameeleza kuhusu harakati zao na THAMANI YAO HALISI kupitia wimbo huu wa WOMEN OF THE WORLD.
Karibu uungane naye katika BURUDANI ELIMISHI hii.
SISITIZO: SIKILIZA UJUMBE MZITO ULIOMO KWENYE WIMBO HUU

JAMII PRODUCTION ILIPATA FURSA YA KUFANYA MAHOJIANO NA ANNA MWALAGHO Mwezi Machi 2012
Na haya hapa chini na maelezo ya post kuhusu mahojiano hayo, na mahojiano yenyewe. KARIBU
Kazi yetu ni kutunza kumbukumbu za wale ambao wanathamini mawazo, fikra, na mbinu zao kwa manufaa ya wengine au vizazi vipya.
Msikilize kwa makini Muigizaji, Mchezaji, Mshairi, msimulizi wa hadithi na mwimbaji Anna Mwalagho akieleza mengi kuhusu maisha yake.
Ameeleza alivyoanza mpaka alipofikia, waliomvutia, mafanikio katika kazi na mengine mengi.
Msikilize kwenye mahojiano haya aliyofanya nasi ndani ya studio za Asparagus zilizopo Takoma Park, jimbo la Maryland nchini Marekani

Pia nilimuuliza kilichomsukuma / kusababisha kuandika wimbo wa I REMEMBER ambao binafsi naupenda sana.
Haya hapa chini ni maelezo niliyounganisha na wimbo wenyewe.
Enjoy

Punde baada ya mahojianao wakania IMPROMPTU ACT na Abou.
Hahahahaaaaaaa

Shukrani za pekee kwa Abou Shatry wa Swahilivilla Blog kwa kufanikisha hili

No comments: