Wednesday, June 26, 2013

NELSON MANDELA pamoja NASI

Papaa Madiba..
Si lazima uwe NASI ili uwe NASI!
Ulikuwa NASI bila kuwa NASI na kwa miaka 27, ulikuwa NASI zaidi ya waliokuwa NASI.
Na sasa.....
Hauko karibu NASI lakini wengi walio kama sisi wanakuona wewe ukiwa NASI kuliko hata hawa walio wema na huku mitaani pamoja NASI.
Uliwekeza maisha yetu hata kwa kutengwa NASI. Ukatoka na kujiunga kusherehekea uhuru wako NASI.
 Tambua kuwa .....
Katika ulimwengu wa UKWELI, HESHIMA NA ROHO ulikuwa, upo na utaendelea kuwa NASI.
NASI sasa twafuatilia mwisho wa uwepo wako kimwili pamoja NASI
Lakini....
Utaendelea kuwa NASI kutokana na yale yote mema uliyotutendea.
Ikimpendeza Muumba utengane NASI kimwili, jua maishani mwetu (at least mwangu) utaendelea kuwa NASI
Love Love Madiba!!
ASANTE KWA UJUMBE HUU MKUU
Na sasa tusikilize makala hii maalum iliyozungumza ama kumkumbuka Mzee Mandela. Iliandaliwa na Peace Talk Radio

No comments: