Tuesday, June 11, 2013

VIDEO: Mahojiano na Mhe. Balozi Amina Salum Ali

Karibu katika sehemu ya kwanza kati ya mbili za mahojiano kati ya Jamii Production na Balozi wa Umoja wa Afrika (AU) nchini Marekani Mhe. Amina Salum Ali.
Katika sehemu hii, Mhe Amina ameeleza mengi ikiwemo...
1: Historia ya maisha yake.
2: Aliingia vipi kwenye kazi ya diplomasia?
3: Ni nini wajibu wake? Anawajibika kwa nchi ya Marekani ama na mashirika ya kimataifa kama IMF na World Bank?
4: Ni wapi ulipo mpaka kati ya majukumu ya mabalozi wa nchi wanachama wa AU na yeye anayewakilisha Umoja?
5: AU ina mikakati gani katika kufunda ama kuwalea viongozi wa afrika?
6: Kuna MAFANIKIO GANI ya Umoja wa Afrika hasa ukizingatia kuwa tangua kuanzishwa kwake tumeshuhudia nchi zikizidi kugawanyika badala ya kuungana kama Ethiopia na Eritrea na hata Sudan na Sudan ya Kusini?
7: Ni nini kinachokwamisha Umoja wa Afrika katika migogoro kama ya Kongo?
8: Nchi zetu ziko huru, zinajitawala, lakini ni kwa MANUFAA YA NANI?
9: Ni kweli kuwa Umoja wa Afrika unaendelea kuwepo si kwa mafanikio yake, bali kwa kukosekana kwa UMOJA M'BADALA?
10: Ni kweli kuwa kuna mamluki wanaokwamisha harakati za Umoja wa Afrika toka nje ya bara letu?
11: Tofauti ya mifumo ya utawala na nguvu za kijeshi na uchumi zinaathiri vipi UMOJA WA AFRIKA?
KARIBU UUNGANE NASI
Katika sehemu hii ya pili, Mhe. Balozi Amina amezungumza mengi ikiwa ni pamoja na....
1: Nafasi ya wanawake katika maamuzi na maendeleo ya Afrika. Je! Idadi kubwa ya wanawake tulionao katika nyadhifa barani Afrika ni ishara ya maendeleo ama ni "nafasi za upendeleo"?
2: Anaitafsiri vipi DEMOKRASIA YA AFRIKA na anaamini kipimo cha Demokrasia barani Afrika kingekuwa nini?
3: Ni nini anachoamini kuwa kingefanyika barani Afrika ili kuleta demokrasia ya kweli?
4: Anaamini Umoja wa Afrika umefanikiwa kwa kiasi gani katika madhumuni ya kuanzishwa kwake?
5: Je! Anaamini kuwa RUSHWA itaisha barani Afrika?
6: Yeye kama Mwanasiasa, Mwanadiplomasia na mTanzania, anazionaje siasa za Tanzania kuelekea 2015?
7: Anaishauri nini serikali katika kukabilaiana na ukuaji wa TEKNOLOJIA YA HABARI?
8: Kutokana na hali ilivyo Tanzania hivi sasa, anaionaje nafasi ya mwanamke katika kuongoza Tanzania?
9: Nini wito wake kwa wale wote wanaofuatilia mahojiano haya?
KARIBU UUNGANE NASI

No comments: