Tuesday, July 9, 2013

Ramadhan njema kwenu nyote


Kwa siku kadhaa zilizopita, asilimia kubwa ya takribani watu Bilioni moja waumini wa dini ya Islamu wamekuwa wakijiandaa kwa mwezi mtukufu wa Ramadhani, mwezi wa tisa na MTUKUFU zaidi katika kalenda ya kiIslamu.
Mwezi huu uambatanao na mafunzo na njia sahihi za kuishi kiIMANI, na uwe nguzo ya maisha yetu hata baada ya kumalizika kwa mwezi huu
Yafunzwayo na kuhimizwa kwenye mfungo na mwezi mzima, ni mambo ambayo naweza kuyaita NJIA SAHIHI ZA KUISHI KATIKA JAMII na ninaamini yale yafunzwayo na maisha tuishiyo mwezi huu, tutayaendeleza maishani
Blogu ya CHANGAMOTO YETU yawatakia wale wote wafungao na kuamini katika mwezi huu, MWEZI NA MFUNGO MWEMA na kwa wale wote waishio na waamini, tunawatakia ushirikiano mwema kwa waaminio na kufunga katika mwezi huu
RAMADHAN KAREEM.

No comments: