Kwa wasomaji wote wa Changamoto yetu (na blog nyingine)
Nimeamshwa na taarifa juu ya malalamiko ya MMK MEDIA kwenye vyombo vya habari kuhusu ubalozi na / ama afisa balozi wake Binafsi napenda kugusia mambo mawili kuhusiana na lalamiko lao KWA NAMNA AMBAVYO NIMEHUSISHWA / TUMEHUSISHWA (kama Jamii Production)
Katika malalamiko hayo, MMK MEDIA imeambatanisha BARUA YANGU ambayo ilikuwa ni BARUA BINAFSI KWA KAIMU BALOZI (kwa wakati huo) Mama Lilly Munanka.
Barua hiyo (kama nilivyosema hapo awali) ilikuwa ni BARUA BINAFSI na haikupaswa kuchapishwa kwenye blogu kama ilivyotokea. Niliiandika kwa Mama Munanka kama barua ya awali ya malalamiko kwake na haikuwa barua ya kuchapisha kwenye blogu kama ilivyotokea (kwa bahati mbaya) kwa wale niliowaambatanisha.
KAMA INGEKUWA NI YA KUCHAPISHWA KWENYE BLOGU, BASI INGEKUWA KWENYE BLOGU YANGU KABLA YA KWINGINE KOKOTE
Hata hivyo, punde baada ya kuchapishwa niliwasiliana na wanahabari wenzangu (ambao niliwaambatanisha katika barua hiyo) na kuwaeleza kuwa ile ilikuwa NAKALA KWAO NA SIO CHAPISHO LA BLOG.
Nilifanya hivyo kwa kuwa ilikuwa ni mara yangu ya kwanza kuwasiliana na Mama Munanka na hivyo halikuwa jambo sahihi kuchapisha barua hiyo bloguni.
Lakini pia, katika lalamiko la sasa, MMK MEDIA wameandika kuwa "Baada ya tukio hafla hiyo kubwa kupita bila kusita niliandika masikitiko yangu kwa niaba ya MMK MEDIA GROUP wamiliki wa Swahili TV online, Swahili Radio Online na Blog ya Swahilitv.blogspot.com kuhusiana na yaliyojitokeza ubalozini."
Ni kweli kuwa nami niliyaona malalamiko hayo ambayo pia kwa kiasi fulani yalinisikitisha
Katika malalamiko hayo, MMK MEDIA iliandika kuwa "afisa huyu alikimbia vyombo vya habari rasmi na kualika video production company inayofanya shughuli za harusi kuwa mwakilishi wa Swahili Tv, Swahili Radio, Swahilitv Blog, na vyombo vingine vinavyoheshimika hapa DMV" (tazama screenshot hapa chini)
Hilo lilinisikitisha kwa kuwa NI DHAHIRI KUWA TUMEKUWA TUKIFANYA HABARI KABLA NA ZAIDI YA MMK MEDIA
Tumekuwa tukishirikiana HABARI (sio matukio na taswira tuu) na vyombo vingi vya habari nchini Tanzania KABLA YA KUZALIWA KWA MMK MEDIA.
Na katika hili, ushahidi upo wazi kwani sote tunaweka kazi zetu online, hivyo ni rahisi kwa wewe msomaji kuLINGANISHA UBORA WA HABARI katika KAZI ZETU ZA SAUTI (hapa) NA KAZI ZAO (hizi hapa) ama KAZI ZETU ZA VIDEO (hapa) na KAZI ZAO (hapa)
Kwa kumalizia tu, niseme kuwa SIPINGI HAKI YA MMK MEDIA KULALAMIKA, ila nasikitika kuwa WAMETUMIA BARUA YANGU BINAFSI KUJAZIA MALALAMIKO YAO HADHARANI, na pia wameshindwa kuwa wawazi kuhusu malalamiko yao ya awali ambayo kwa namna moja ama nyingine YALIPOTOSHA KUHUSU JAMII PRODUCTION NA KAZI ZAKE.
Lakini bado (BILA IDHINI) wametumia nakala ya barua yangu kutimiza lengo lao.
Katika hili nimesikitishwa na ningependa NILIWEKE HILO WAZI.
Mubelwa T Bandio
MTAYARISHAJI / MTANGAZAJI
JAMII PRODUCTION
1 comment:
Wameghafirika.Sikuwa nafuatilia matangazo yenu mara kwa mara.Hongera sana kwa kazi nzuri kaka.
Post a Comment