Saturday, November 9, 2013

[AUDIO] DAKIKA 90 ZA DUNIA: Athari za vita baada ya kumalizika mapigano

Photo Credits:myptsd.com
Wakati vita ya Congo ikionekana kuelekea ukingoni, bado tunakumbushwa kuwa athari za vita katika nchi mbalimbali huendelea kuwaathiri wahusika na hasa wananchi wa nchi hizo kwa miaka mingi baada ya kumalizika kwa vita hivyo.
Baadhi ya athari huwa wazi sana. Mfano ni majengo yaliyoharibika wakati wa mapigano, watu wanaouawa wakati wa mapigano na hata uchumi unaozorota kutokana na watu kutofanya kazi wakati wa mapigano hayo.
Lakini pia kuna athari ambazo hazionekani ama kutopewa kipaumbele machoni mwa watu wengi baada ya vita hivyo.
Hivi karibuni, waMarekani wamekumbushwa kuhusu hili
Hii ni sehemu ya ripoti ya Jamii Production kwenye kipindi cha DAKIKA 90 ZA DUNIA kinachorushwa na kituo cha Radio cha Capital FM cha Dar Es Salaam Tanzania kila Jumamosi kuanzia saa moja na nusu asubuhi (7:30 AM).

Bahati Alex (L) Capital Radio Jijini Dar es Salaam na Mubelwa Bandio (R) wa Jamii Production Washington DC
Hii ilikuwa ripoti ya Novemba 9, 2013

No comments: