Monday, November 4, 2013

Balozi Mulamula na Kjell Berg washiriki Ibada ya Mavuno, Usharika wa Kikristu wa Kiswahili Minnesota

Kwa hisani ya Mindi Kasiga
 Mhe. Liberata Mulamula akiwasili kwenye Ibada ya Mavuno Usharika wa Kikristu wa Kiswahili Minneapolis, Minnesota na kupokelewana Mchungaji wa Usharika huo Andrea Mwalilino. Katikati ni mshereheshaji wa shughuli ya Mavuno Bw. Gracious Msuya. Ibada hiyo ilifanyika Jumapili tarehe 3 Novemba 2013
Mchungaji Mwalilino na sehemu ya waumini akiongoza wimbo wakati wa Ibada ya Mavuno ya usharika huo.
Mhe. Kjell Berg, Balozi wa Heshima wa Tanzania Jimboni Minnesota akiwasalimia Watanzania wakati wa sherehe za mavuno kwenye kanisa la Usharika wa Kikristu wa Kiswahili, Minneapolis Minnesota.

Mhe. Liberata Mulamula akizungumza na waumini wa usharika huo ambao wengi wao ni Watanzania waliofurika kwa wingi wakati wa sherehe hizo za mavuno tarehe 3 Novemba 2013.

 
Blanketi likiuzwa kwenye mnada wakati wa sherehe za mavuno usharikani hapo ambapo ahadi na makusanyo ya mavuno yaliyopatikana ilikua jumla ya dola za kimarekani 2,500.
Muendeshaji wa mnada huo Smart Baitani akipita kusalimia meza kuu baada ya kufunga mnada rasmi.
Balozi Mulamula aliyeambatana na mumewe Bw. George Mulamula  wakiagana na Mhe. Kjell Berg baada ya sherehe hizo za mavuno kukamilika.
Watanzania na Marafiki wa Tanzania waliokusayika kwenye hafla ya chakula cha usiku nyumbani kwa Bw. Meshak Balira New Hope, MN kwenye picha ya pamoja na Mhe. Balozi Liberata na Bw. George Mulamula baada ya chakula na maongezi.
Josiah Kibira mtayarishaji wa Filamu za Kiswahili za BongoLand I,II, III na IV akimzawadia Balozi Mulamula filamu hizo ambazo alisema zimesambazwa Vyuo Vikuu vinavyofundisha Kiswahili nchini Marekani na nje ya Marekani.

No comments: