Wavuna umati wa washabiki wa kimataifa
Bendi maarufu ya muziki wa dansi barani Ulaya Ngoma
Africa almaarufu FFU ughaibuni,usiku tarehe 23 Novemba 2013 walifanikiwa
kwa mara nyingine kuliteka jiji la Bremen nchini Ujerumani. Kiongozi wa bendi hiyo
kamanda Ras Makunja wa FFU alikiongoza jukwaani kikosi kazi chake katika
jumba la Übersee-Museum akiwa na matumaini kuwa wanaenda kutumbuiza
washabiki "high class" (wenye hadhi ya kibwanyenye) lakini mziki ulipoanza
mdundo uliwachanganya washabiki na kila mmoja
alijimwaga uwanjani !
Ngoma Africa Band walijikuta wapo katika kibarua kama kawaida yao
cha kushambulia kwa virungu vya muziki na kufanikiwa kuupanua wigo
wake kwa kuwanasa mashabiki wengi wa kimataifa.
Bendi hiyo iliyojiimarisha na kujenga himaya ya kimataifa kwa kutumia muziki wake, imekuwa ikitajwa kama bendi bora ya kiAfrika barani ulaya.
Bendi
ya Ngoma Africa inafanananishwa sawa na kikosi maalumu cha kuzuia
ghasia FFU, lakini pia ina majina mengi ya utani na kiusanii kama vile Viumbe
wa ajabu "Anunnaki Elien" n.k ambayo imepewa na washabiki au wapenzi
wake.
Kiongozi wake pia ana majina kama vile kamanda Ras Makunja wa
FFU ,mtawala wa Anunnaki Empire.
Ngoma Africa band wanasikika kupitia www.ngoma-africa.com
No comments:
Post a Comment