Sunday, November 24, 2013

Thanksgiving Parade ya 2013 yafana Silver Spring Nchini Marekani


Mamia ya wananchi walikusanyika jana hapa Silver Spring Maryland kwenye gwaride la Siku ya shukrani (Thanksgiving).
Washiriki wengi wamevaa nguo za utamaduni za nyakati za kale za (Miaka ya 1600 hadi sasa.)
Asili ya kusherehekea Thanksgiving imianza katika miaka ya 1613 na wananchi wengi walijitokeza kuangalia Parade hiyo licha ya kuwa na hali ya baridi, ambayo inafanyika kila mwaka.
Askari wa mji wa Montgomery wakipita na pikipiki  katika maonyesho ya ufunguzi wa ufunguzi wa Thanksgiving Parade iliofanyika Siku ya Jumamosi 23, 2013 katika Mji wa Silver Spring Maryland. (Picha zote  na swahilivilla.blogspot.com)
Montgomery county police wakiwa katika ufunguzi rasmi wa Thanksgiving Parade iliofanyika Siku ya Jumamosi 23, 2013 katika Mji wa Silver Spring Maryland.
Vijana waliovalia mitindo ya mavazi ya asili  wakipita na bango la kukaribisha sikukuu ya  Thanksgiving itakayofanyika rasmi siku ya Alhamis Nov 28 nchini Marekani
Police wa jimbo (State Police) wa Maryland wakipita na bendera katika Thanksgiving Parade iliofanyika Siku ya Jumamosi 23, 2013 kwenye mtaa wa Fenton, Georgia Avenue, na kumalizikia Silver Spring Avenue.
Wanafunzi wa  Springbrook  High School wakipita na Band katika Thanksgiving Parade wakiwa katika mwendo wa burudani
Wanafunzi wa Bowie State University pia walikuwepo wakitoa burudani ndani ya Parade hiyo
Wanafunzi wa Bowie State University wakiburushisha kwa Bandi mbele ya halaiki ya mamia ya watu waliokusanyika kuangalia burudani hiyo.
Warembo wa Kilatino akiwa amevalia mavazi ya kitamaduni kusherehekea Thanksgiving Parade iliofanyika siku ya Jumamosi Nov 23,  2013 ndani ya Jiji la Silver Spring Maryland Nchini Marekani!
Mbunge wa kata ya Montgomery County, Philip M. Andrews akipita katika  Thanksgiving Parade iliofanyika siku ya Jumamosi Nov 2,  2012 ndani ya Jiji la Silver Spring Maryland Nchini Marekani!
Baadhi ya watazamaji wengi walio pembezoni wakiangalia burudani ya Thanksgiving Parade
Fulan Dafa wenye asili ya kiChina wakitoa burudani katika sherehe ya Thanksgiving Parade
Wachina wa Fulan Dafa wakimzungusha Yellow Dragon katika kusheherekea Thanksgiving Parade
Wasichana warembo waliovaa mitindo ya mavazi ya aina yake wakitoa burudani  kwenye Thanksgiving Parade iliofanyika Jumamosi 23, 2013 katika Mji wa Silver Spring Maryland.
Wasichana warembo waliovaa mitindo ya mavazi ya aina yake wakipita kwenye Thanksgiving Parade iliofanyika Jumamosi 23, 2013 katika Mji wa Silver Spring Maryland.

No comments: