Sunday, March 9, 2014

Balozi Mulamula awapongeza Tano Ladies katika siku ya wanawake Duniani

Na Abou Shatry Washington DC
Katika sherehe ya kuadhimisha Siku ya kimataifa ya wanawake duniani, Mgeni rasmi Balozi wa Tanzania Marekani na Mexico Mhe. Liberata Mulamula amewapongeza Tano Ladies kwa uwezo wao mkubwa wa kufanikisha wito wao wa kuwaweka pamoja wanawake wa Tanzania pamoja na kusherehe International Women’s Day (IWD) siku ya March 8 inayosherehekewa kila mwaka ulimwenguni.
Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa nchi za Marekani na Mexico Mhe. Liberata Mulamula (watano kutoka kushoto waliosimama) katika picha ya pamoja na wajasirimali kwenye sherehe za wanawake duniani aliyoandaliwa rasmi na Tano Ladies (waliochuchumaa) siku ya Jumamosi Machi 8, 2014 ndani ya ukumbi wa Hampton Inn uliopo College Park Maryland Nchini Marekani 

Na pia kuweza kuwakusanya wanawake wajasirimali wa Tanzania kutoka sehemu mbalimbalina kwa kuweza kuonyesha ujuzi wao na kuweza kusherehekea sherehe hizo zinazofanyika kila Mwaka, March 8 duniani kote.
Balozi Liberata Mulamula aliaaza kwa kuwapongeza na kuwahamasisha kundi zima la Tano Lades kwa kazi nzuri waliofanya kwa ushirikiano na wanawake wenziwao wenye kuleta umoja na mshikamano katika kuendeleza maendeleo katika jamii ya waTanzania waliyopo hapa Amarekani.
Katika sherehe hizo Mhe Mulamula alikutana na wanawake wajasirimali mbali mbali waliweza kuweka meza zao ndani ya ukumbi na kutembelea meza moja baada ya moja na kupata maelezo ya kila mjasirimali katika biashara nazozifanya.
Balozi Mulamula liendelea kwa kuwasifu wanawake wajasirimali wakitanzania na kuwakabidhi vyeti katika siku hiyo adhimu ilioandaliwa rasmi na Tano Ladies.
Sherehe hizo zilitumbuizwa kwa nyimbo na wasichana waTanzania kutoka kwa Mama Jessica Kamala Mushala, pamoja na kundi zima la Taratibu Youth Association, kutoka Mount Rainier Maryland, na muimbaji Erica Lulakwa Glenn mTanzania kutoka San Francisco California, katika sherihe hizo zilizofanyika kwenye ukumbi wa Humton in College park Maryland nchini Marekani.
Balozi wa Tanzania Marekani na Mexico Mhe. Liberata Mulamula akipata maelezo mafupi  ya afya kutoka kwa Herriet Shangiraifupi wa Nesiwangu,bofya hapa kutembelea blog yake nesiwangu.blogs 
Mhe. Liberata Mulamula alipotembelea meza ya Nashona Bibie Lilian Danieli kutoka North Carolina
Mjasirimali Maria Mohamed alipokua kwenye meze yake ya Bahari Deco Crafts Style the Swahili way kwenye sherehe za wanawake duniani aliyoandaliwa rasmi na Tano Ledies Siku ya Jumamosi Murch 8, 2014 ndani ya ukumbi wa Hampton Inn uliopo College Park Maryland Nchini Marekani
Balozi wa Tanzania Marekani na Mexico Mhe. Liberata Mulamula akipata maelezo mafupi kutoka kwa mbunifu wa mishono ya Madira Salha Mwamende pamoja na familia yake siku ya kimataifa ya wanawake duniani.
Mtuzi wa kitabu cha Taste of Tanzania Miriam Rose Kinunda akiweka saini kwenye kitabu cha mteja alienunua kwenye maadhimisho ya Siku ya mwanamke duniani. 
Mtaalamu wa matatizo ya mitandoa (Computer Super Technician) Bi Mamina Yas akiwa katika utambulisho wa meza ya ujasirimali mwanamke anaweza kushuhulikia matatizo ya computer yako wakati wowote pale inapopatwa na matatizo ndani ya maeneo ya DMV unaweza kuwasiliana nae kama mkaazi wa maeneo haya. (Picha zote na swahilivilla.blogspot.com)

No comments: