Tuesday, May 27, 2014

Kumbukumbu ya kifo cha Mangwea Mei 28, Samaki Samaki Morogoro


..Mastaa kibao kujumuika katika ‘LOVE CONCERT’
..Afande Selle, Belle 9, Samir na wengineo –Moro
P-Funky, Mswaki, Chemba Squad kutikisa

Na Andrew Chale
MASTAA mbalimbali nchini wakiwemo wanamuziki wanatarajiwa kushiriki kwenye tukio maalum la kumbukumbu ya mwaka mmoja tokea kifo cha marehemu Albert Mangwea ‘Ngwair’ , litakalofanyika ndani ya ukumbi wa Nyumbani Park (Samaki samaki Spot) , Kihonda Morogoro mjini Juni 28.
Akizungumza na mtando huu , Mratibu Mtendaji wa tamasha hilo, Kareeem Omary ‘KO’ alisema maandalizi ya tukio hilo litakalokuwa la kila mwaka, limepwa jina la ‘Love Concert - Kumbukumbu ya kifo cha Albert Mangwe’.
Kareem, aliwaomba wadau kujitokeza kwa wingi kuunga mkono kwenye tukio hilo kwani litakuwa la kipekee na la aina yake ambalo pia litatoa fursa kwa wakazi hao pia mikoa jirani na watu kutoka nje ya Tannzania ambao watauzulia.
“Nawaomba wadau kujitokeza kuonesha upendo wa pamoja. Kumbukumbu kwa mpendwa wetu kama ilivyo utamaduni wetu.” alisema Kareem.
Na kuongeza kuwa, siku hiyo Watu mbalimbali watapata kupiga picha na mastaa pamoja na mama mzazi wa Mangwea kama kumbukumbu.
Kareem aliwataja wasanii watakaotoa burundani, ni pamoja na kutoka kwa kundi la Wanachemba ambalo pia aliwahi kuwa nalo marehemu Ngwair, JSqueezer, P Funky Majani na Mswaki. Kwa upande wa wasanii kutoka Morogoro ni pamoja na Afande Sele, Team Racers, Mc Koba Chris wa Marya, Belle 9, Samir, Zombie, President Mirrow, Jordan wa Dejavu na wengine wengi.
Katika siku hiyo ya Juni 28, ambayo ndiyo siku aliyopatwa na umati marehemu, Kareem alisema kabla ya matukio ya shoo ukumbini, itatanguliwa na ibada mbili maalum ikiwemo ya Kanisani na ile ya nyumbani.
Aidha, Kareem alisema katika tukio hilo, ambalo linatarajia kuanza majira ya jioni ya saa 10 hadi saa 12 jioni, wametoa fursa kwa watoto kutoa burudani ikiwemo ya kuimba na nyinginezo na baadae usiku wa kuanzia saa 2 hadi majogoo wasanii hao mbalimbali watatawala jukwaa na burudani ya nguvu ya kumbukumbu.
Marehemu ‘Ngwair’ alifariki dunia akiwa nchini Afrika kusini, alijizolea umaarufu kwa nyimbo kama Mikasi na Nisikilize Mi na nyingine nyingi alizowahi shirikishwa na wasanii mbalimbali nchini wakiwemo Professa Jay, Nuru, TID, Chidi Benz na wengine wengi.

Nyumbani kwa Mama Mangwea 

No comments: