Friday, October 3, 2014

Wajumbe wa DICOTA 2014 CONVETION wakutana kwenye cocktail party kwa utambulisho.

PICHA KWA HISANI YA VIJIMAMBO BLOG
 Bw. Lunda Asmani akielezea utaratibu utakavyokua kwenye DICOTA 2014 Convetion itakayoaanza muda si mrefu leo Ijumaa Oct 3, 2014 kwenye hafla ya Cocktail iliyofanyika Alhamisi jioni Oct 2, 2014 katika hotel ya Millennium Durham North Carolina. Bw. Lunda Asmani pia alitumia wasaa huo kuwatambulisha wageni mbalimbali akiwemo mgeni rasmi Katibu Mkuu kiongozi Mhe. Balozi Ombeni Sefue.
Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini Marekani Mhe. Liberatus Mulamula akiongea na wahudhuriaji waliofika Alhamisi ya Oct 2, 2014 kwenye DICOTA 2014 Convetion itakayoendelea leo Ijumaa Oct 3, 2014 katika hotel ya Millennium Durham, North Carolina nchini Marekani.

Bw. Mark toka Texas(kati) akiongea na wajumbe kwenye hafla ya Cocktail iliyofanyika Alhamisi jioni kulia ni Mhe. Liberata Mulamula na Lunda Asmani kushoto wakifuatilia kwa karibu.

Mgeni rasmi wa DICOTA 2014 Katibu Mkuu Kiongozi  Balozi Ombeni Sefue (kati) katika picha ya pamoja na wajumbe waliofika kwenye mkutano wa DICOTA Durham, North Carolina nchini Marekani akiwemo mkurugenzi mkuu wa Azania Bank Bw. Charles Singili.

Mhe. Liberata Mulamula akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wajumbe waliofika kwenye mkutano wa DICOTA 2014 Durham, North Carolina nchini Marekani.

Kutoka kushoto ni Gella Sambula, Bw. Alphano Kidata (permanent Secretary) na H. Taratibu (Asst Director of Planning & Budget wakifuatilia jambo walipojumuika na wajumbe kwenye hafla ya Cocktail iliyofanyika Alhamisi jioni katika hotel ya Millennium Durham, North Carolina nchini Marekani.

Mjumbe akipata picha ya kumbukumbu na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue
Wajumbe wakisikiliza utaratibu na mwongozo wa DICOTA 2014 Convetion kama ulivyokua ukitolewa na Bw. Lunda Asmani. Kwa picha zaidi bofya HAPA

No comments: