Saturday, March 7, 2015

KANISA ALILOTUMIA DR KING KATIKA HARAKATI ZA KUPINGA UBAGUZI

Kwa hisani ya mdau Dj Luke Joe

 Kanisa la Baptist lililopo jiji la Birmingham jimbo la Alabama kanisa alilokua akilitumia Dr. Martin Luther King miaka ya 1965 katika kuendeleza harakati za kupinga ubaguzi wa Wamarekani weusi mpaka kupelekea kanisa hili kupigwa bomu lililoua watoto wanne. Kanisa hili lipo barabara ya 16 N na barabara ya 6 N kwenye mji huo wa Birmingham.
Watu kutoka kila kona ikiwemo Vijimambo wakitengeneza historia ya kufika mahali ambapo Dr. Martin Luther King alipatumia kuendeleza harakati zake za kupinga ubaguzi wa Wamerekani weusi uliokua ukiendelea enzi hizo wazi wazi na hatimae kusikika Dunia nzima na kuungwa mkono na watu wengine ndani na nje ya Marekani.
 Watu wakipata ukodak moment wakiwa eneo la kanisa la Baptist lenye hstoria ya Dr. Martin Luther King katika harakati za kupinga ubaguzi kwa Wamarekani weusi ukiwemo na kutokupiga kura.
Watu mbalimbali wakiandika historia.

Eneo la maegesho ya magari

No comments: