Sunday, March 1, 2015

Mhe. Ismail Jussa azungumzia Katiba Washington DC

Na Abou Shatry Washington DC
Mwakilishi wa jimbo la mji mkongwe ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa chama cha wananchi CUF Mhe: Ismail Jussa Ladhu amesema Tanzania inaelekea kusipotarajiwa na maoni ya wananchi waliyotoa maoni.
Mwakilishi wa jimbo la mji mkongwe Mhe: Ismail Jussa Ladhu akiongea na waTanzania wa DMV Siku ya Jumamosi Feb 28, 2015 kwenye ukumbi wa Tabeer Hall uliopo University Blvd East, Hyattsville, Maryland, Nchini Marekani. (Picha na swahilivilla)
Aidha amesema matarajio ya watanzania hayajatimizwa mbali ya kuwepo mijadala mingi juu ya rasimu ya Jaji Warioba ili kulipatia ufumbuzi wa kudumu katika Suala la katiba mpya.
Mhe. Jussa aliyasema hayo wakati akizungumza na Watanzania wa DMV siku ya Jumamosi Feb 28, 2015 kwenye ukumbi wa Tabeer Hall 1401 University Blvd East, Hyattsville, Maryland, Nchini Marekani.
Pia Mhe. Jussa ambaye pia ni mjumbe wa UKAWA amesema uamuzi wa UKAWA kususia na kujitoa katika bunge la katiba ni kwa sababu chama tawala CCM kimekwenda kutetea sera zake na kupinga mawazo ya wananchi ambayo yamewakilishwa katika rasimu ya Jaji Warioba.
Mkutano huo ulijumuisha Agenda kadhaaha ikiwemo Mchakato wa Katiba mpya, Ufafanuzi juu ya muundo wa serikali tatu, Uamuzi wa UKAWA kususia mchakato huo dhalimu na sababu ya maoni ya watu walio Diaspora kuhusu Uraia Pacha kutokutekelezwa kama walivyotarajia.
Video ya maswali na majibu utawajia hapo baadae
Watanzania waishio DMV(Washington DC, Maryland na Virginia) wakimsikiliza Mh Ismail Jussa alipohutubia katika mkutano uliondaliwa na Muungano wa Vyama vya CUF na CHADEMA Marekani.
Mwakilishi wa jimbo la mji mkongwe Mhe: Ismail Jussa Ladhu akiongea na waTanzania wa DMV, walioka meza kuu wakanza kushoto Katibu wa Tawi la Chadema DMV Liberatus "Libe" Mwangombe, akifuatiwa na Mwenyekiti wa Tawi la Chadema DMV Mhe. Kalley Pandukizi, Shamis Alkhatry CUF pamoja na Katibu Mkuu wa Baraza la kina mama CHADEMA DMV Bi Baybe Mgaza.

No comments: