Sunday, April 26, 2015

Timu ya Zanzibar Diaspora USA yanyakua Kombe la Muungano Washington DC kwa Ushindi wa Mabao 7-1 dhidhi ya Tanganyika

Na Abou Shatry wa SwahiliVilla Blog
Katika shamrashamra za kusherehekea Miaka 51 kuungana Tanganyika na Zanzibar na kuwa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Timu ya Zanzibar Diaspora​ nchini Marekani imeifunga bao 7-1 jirani zake timu ya Tanganika USA.
Kocha wa timu ya Zanzibar Heroes Seif Ameir pamoja na Kapteni Deddy Rouba​ wakikabidhiwa Kombe la Muungano
Mechi hiyo ambayo imehudhuriwa na mgeni rasmi rais mstafu wa awamu ya pili wa Tanzania Mhe Alhajji Ali Hassan Mwinyi. ilifanyika katika viwanya vilivyopo Walker Mill Road District Heights Maryland, ambapo pia ilihudhuriwa na balozi wa Tanzania nchini Marekan Mhe. Liberata Mulamula.
Mechi hizo hufanyika kila mwaka kwaajili ya kusherehekea kuungana kati ya Tanganyika na Zanzibar April 26, 1964.
Rais mstafu wa awamu ya pili wa Tanzania Mhe Alhajji Ali Hassan Mwinyi baada ya kusalimiana na wachezaji wa timu zote mbili
Mapema Mhe Alhajji Ali Hassan Mwinyi aliwataka waTanzania kuungana kwa pamoja bila ya kujali tafauti zao
Wakati huo huo kabla ya mechi kuaza Alhajji Ali Hassan Mwinyi alisalimiana na timu zote mbili na kuupiga mpira kuashiria kuaza kwa mechi hiyo.

Kikosi kamili cha timu ya Zanzibar Diaspora
Mashindao hayo ambayo yaliwapa ushindi mnono Timu ya Zanzibar Heroes baada ya kichapo cha 7-1 dhidi ya Timu ya Tanganyika katika mechi ya kutafuta Bingwa wa Kombe la Muungano, bao la kwanza kwa timu ya Zanzibar lilifungwa kwa njia ya Penalti mfungaji wa bao hilo alikuwa Yahya Kheri na magoli mawili ya lifungwa na Wingi machachari Abdulla J. Somania, mbao hadi timu kipindi cha kwanza kumalizika Timu ya Tanganyika ilifungwa 3-0
Kipindi cha pili kuaza, Tanganyika waliingia kwa kasi, na katika mchezo waliocheza haukuwasumbua sana timu ya Zanzibar kutokana na udhibiti wa wachezaji wanne  ambao wazoefu wa zamani katika funi ya soka waliweza kuumiliki mchezo huo, mmoja wao alikuwa Captain Deddy Rouba​ ambae alikuwa Super Middlefield wa mchezo huo, aliposaidiana na Yussuf Mecca kutoka Columbus,Ohio,Yahya pamoja na Ally, ambao wametawala ngome ya timu ya Tanganika, bao la nne na la tano yalifungwa na Mshambuliaji hatari Lodi Mohammed, na bao la sita na  lasaba, lilifungwa na wingi hatari na mchezaji nyota ambae amechukua tunzo la mchezaji bora katika mchezo huo Abdulghan Ali Himid ambae baada ya mchezaji Yussuf Mecca kupata Redcard kwa kosa la kulalamika kwa goli la offside lilifungwa dakika ya 76 za mchezo huo na kujikuta timu ya Tanganyika kuambulia kipigo cha magoli 7-1, chini ya Kocha Seif Ameir wa Timu ya Zanzibar Diaspora Nchini Marekani.
 
Abdulghan Ali Himid akipokea tunzo la uchezaji bora 
Ally akishangilia Ushindi wa ZADIA
 
Mwenyekiti wa Zanzibar Diaspora Omar Ally
   
Kocha Seif Ameir wa Timu ya Zanzibar Diaspora Nchini Marekani wapili kushoto akipata picha na wachzaji wa Zanzibar Diaspora
 

No comments: