Tuesday, April 28, 2015

ZADIA kuendeleza umoja na mshikamano wa waZanzibari nchini Marekani

Na Abou Shatry Washington DC
Jumuiya ya Wazanzibari waishio nchini Marekani  Zanzibar Diaspora Association (ZADIA) imesisitiza azma yake ya kendeleza umoja na mshikamano wa Wazanzibari ndani na nje ya Zanzibar.
Mwenyekiti wa  Zanzibar Diaspora Association (ZADIA) ndugu Omar Haji Ally, akitoa maelezo ya utambuisho pamoja na kumkaribisha Mhe. Ali Hassan Mwinyi kwenye mazungumzo na dinner, ilioandaliwa rasmi na uongozi mzima wa (ZADIA) Siku ya Jumapili April, 26, 2015, katika ukumbi wa Tabeer Hall, iliopo Hyattsville, Maryland Nchini Marekani. (Picha zote na swahilivilla.Blog)
Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa ZADIA Ndugu Omar Haji Ally, alipokuwa akitoa maelezo mafupi ya kumkaribisha Rais wa zamani wa Zanzibar Mheshimiwa Alhajj Ali Hassan Mwinyi kwenye chakula cha usiku kilichoandaliwa rasmi na Uongozi mzima wa Zanzibar Diaspora Association (ZADIA) Siku ya Jumapili April, 26, 2015, kwenye ukumbi wa Tabeer Hall uliopo Maryland Nchini  Marekani.
"Hii ni jumuiya ambayo inapambana kuhakikisha kuwa Wazanzibari wanakuwa wamoja", alisema Bwana  Omar Haji Ally, na kuongeza kwamba kama ni watoto, basi wanajumuiya hiyo wanajisikia kuwa na bahati kubwa kuwa na mama Zanzibar.
Katika hafla hiyo ambayo mgeni rasmi aliambatana na ujumbe anaofuatana nao, Maofisa wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani na wanachama wa ZADIA, Bwana Ally alisema kuwa, mbali na kuendeleza umoja wa Wazanzibari, Jumuiya hiyo imejidhatiti katika harakati za kusaidia kuleta maendeleo katika nyanja mbali mbali Visiwani Zanzibar.
Akitoa mfano wa hayo, mwenyekiti huyo aligusia juu ya juhudi zilizofanywa na jumuiya yake katika kuwasiliana na shirika la "Pure Ultrasound' la nchini Marekani ambalo tayari limeshakubali kutuma vifaa vya Ultasounds na wataalamu wake kuwafundisha madaktari wote wa Zanzibar kuvitumia vifaa hivyo.
Rais mstafu wa awamu ya pili wa Tanzania Mheshimiwa Alhaj Ali Hassan Mwinyi akiwahutubia waZanzibar katika hafla ya Chakula cha Usiku, kilichoandaliwa na Zanzibar Diaspora Association (ZADIA) Siku ya Jumapili April, 26, 2015, katika ukumbi wa  Tabeer Hall iliopo Maryland, Nchini Marekani.
Alhajj Mwinyi atakumbukwa kwa msemo wake maarufu alioutoa wakati akiwa rais wa Zanzibar kuanzia 1984-1985 wa "Zanzibar ni njema atakaye aje".
Katika kipindi hicho kifupi, akiwa na Waziri Kiongozi wake Maalim Seif Sharif Hamad, Zanzibar ilipata maendeleo mazuri ya kiuchumi.
Akitoa maelezo kwa niaba ya Wana diaspora wa ZADIA, ndugu Ally, alielezea matumaini yake kuwa Mzee Mwinyi atatumia ushawishi wake kisiasa kuhakikisha kuwa Zanzibar itaendelea kuwa njema katika kipindi kinachokuja cha uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika baadaye mwaka huu na hata baada ya uchaguzi.  
Sikiliza Hotuba ya Mzee Mwinyi 

 Mzee Mwinyi akiwa na Mwenyekiti wa  Zanzibar Diaspora Association (ZADIA) ndugu Omar Haji Ally.
 
Baadhi ya waalikwa wakiwa katika Dinner, ilioandaliwa rasmi na Zanzibar Diaspora Association (ZADIA) Siku ya Jumapili April, 26, 2015 katika ukumbi wa Tabeer Hall, iliopo Hyattsville. Maryland, nchini Marekani.

Mzee Mwingi akiwa na Mkewe Mama Siti Mwinyi katika Dinner, ilioandaliwa rasmi na Zanzibar Diaspora Association (ZADIA) Siku ya Jumapili April, 26, 2015 katika ukumbi wa Tabeer Hall, iliopo Hyattsville, Maryland Nchini Marekani. 

No comments: