Monday, May 25, 2015

MINGURUMO YA PIKIPIKI YAPAMBA HEWA YA MJI MKUU

Na Abou Shatry Swahilivilla Blog Washington DC
 Kila ifikapo wikiendi ya Siku Ya Mashujaa nchini Marekani, maelfu ya mapikipiki na watazamaji humiminika katika barabara za jiji la Washington kushuhudia mtiririko wa ngurumo za mapikipiki katika kile waanadalizi wanachokiita kama na "Ride for Freedom" (Kuendesha kwa ajili ya Uhuru". Ada hii ilianzia mwaka 1988 ikiwa na lengo la kuwakumbuka na kuwaenzi mashujaa wa kijeshi waliohai na waliokufa au kupotea vitani.
Polisi wa Mji Mkuu Washington D.C wakifungua rasmi mwendo wa maelfu ya pikipiki kwaajili ya kutoa heshima  kwa wenzao waliofariki wakiwa  wanalihudumia  jeshi la nchi  hii,  katika sikukuu ya mashujaa yaani ‘Memorial Day’ (Picha zote na swahilivilla.blogspot.com)
Waendesha pikipiki hukusanyika asubuhi ya Jumaapili ya wikiendi hiyo katika eneo la Wizara ya Ulinzi ya Marekani, kisha huvuka Daraja la makumbusho wakati wa mchana, na ndirimo zao huelekea kwenye eneo la Mnara wa Makumbusho Ya Taifa.
Madereva wa magari ya kawaida hushauriwa kukaa kando au kuwa waangalifu wakati wa mapumziko ya wikiendi hiyo kutokana na idadi kubwa ya mapikipiki inayoingia katika eneo zima la Washington na vitongoji vyake, ambayo pia hupelekea barabara nyingi kufungwa.
 Washiriki wa msafara wa Pikipiki unaojulikana kama (Rolling Thunder) wakipita maeneo ya national mall, Jijini Washington DC katika sherehe za sikukuu ya Siku ya mashujaa ‘Memorial Day’.
Tukio hilo la kila mwaka la kuwaenzi mashujaa wa kijeshi, kwa mwaka huu lilianza saa moja asubuhi siku ya Jumapili ya tarehe 24 Mei kwenye eneo la Wizara ya Ulinzi ya Marekani (Pentagon).
Maandamano ya Rolling Thunder (Mtiririko wa Radi) yaliyopewa jina hilo kutokana na mtiriko wa sauti zitokanazo na injini za mapikipiki, yaliingia katika eneo la Washington kupitia Daraja la Makumbusho baada ya kuyajaza maeneo yote ya kuegeshea magari ya Kaskazini na Kusini mwa Pentagon kwa mapikipiki. Baadaye wapandaji waliendesha kulizunguka eneo la Mnara wa Makumbusho ya Taifa.
Dogo: Hudhaifa Shatry akipata burudani za msafara wa pikipiki  (Rolling Thunder) Siku ya Jumapili Mei 24, wakati yakipita  maeneo ya  national mall, jijini Washington DC 
Ingawa maandamano hayo kuchukua muda wa dakika takriban 20 tu tangu kuanza mpaka kumalizika, hata hvyo, makeke na wingi wa mapikipiki yanayoshiriki husababisha mabarabara kufungwa kwa karibuni masaa manne. Mwaka huu barabara zilifungwa kuanzia saa 5 asubuhi mpaka saa 9 alasiri.
Wikiendi Ya Siku Ya Mashujaa (Memorial Day Weekend), huadhimishwa mwishoni mwa Juma la mwisho la mwezi wa Mei kila mwaka nchini Marekani. 
Siku yenyewe khaswa ya Mashujaa ni Jumatatu ya mwisho ya Mei, lakini imepewa jina la "Memorial Day Weekend" kwa vile wafanyakazi wengi hupata nafasi ya kupumzika kwa siku tatu mfululuzi kuanzia Jumamosi hadi Jumatatu. Kwa Taswira  Zaidi Bofya Hapa

 Polisi wa Mji Mkuu Washington DC wakiwa katika funguzi za mwendo wa maelfu ya pikipiki katika sikukuu ya mashujaa yaani ‘Memorial Day’ 
Wakisalimiana na watazamaji waliokaa pembezoni mwabarabara wakati wakivuruisha gurumo za pikipiki zao hewani
 
Pikipiki la aina yake likiwa katika mwendo wa kuvurumisha ngurumo hewani katika sikukuu ya mashujaa yaani ‘Memorial Day’ Siku ya Jumapili Mei 24, 2015 Jijini Washington DC.  Picha zaidi Bofya HAPA
 

No comments: