Tuesday, September 29, 2015

Kipindi cha JUKWAA LANGU Sept 28 2015 (FULL)

Kipindi hiki hukujia kila JUMATATU, kujadili mambo mbalimbali na zaidi kuhusu UCHAGUZI MKUU WA TANZANIA 2015
Hiki ni kipindi kilichosikika Septemba 28, 2015
Kutoka Tanzania tuliungana na Liberatus Mwang'ombe. Mgombea ubunge jimbo la Mbarali kwa tiketi ya CHADEMA
Studioni alikuwepo Dj Luke Joe, na kwa njia ya simu tukaungana na wasikilizaji wengi ndani na nje ya Marekani
KARIBU

Thursday, September 24, 2015

TASWIRA ZA SALA YA EID AL-ADHW-HAA 2015 WAISLAM WASHINGTON DC

Baadhi ya waumini wa Tanzanian Muslim Community Washington DC wakipata picha ya pamoja baada ya kumaliza sala ya Eid Al-Adhw-haa iliosaliwa Siku ya Alhamis Sept 24, 2015 katika msikiti wa Islamic Center New Hampshire Maryland US.( Picha zote na swahilivilla.blogspot.com)
Waumini wa Tanzanian Muslim Community Washington DC wakipata picha ya pamoja baada ya kumaliza sala ya Eid Al-Adhw-haa iliosaliwa Siku ya Alhamis Sept 24, 2015 katika msikiti wa Islamic Center New Hampshire Maryland US.

DINNER ILIYOANDALIWA NA JUMUIYA YA WATANZANIA DALLAS KWA USHIRIKIANO WA DICOTA WAKIWEMO EAST AFRICA DIASPORA BUSINESS COUNCIL

 Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Wilson Masilingi akiongea na Watanzania na marafiki zao waliohudhuria chakula cha jioni kilichoandaliwa na Jumuiya ya Watanzania Dallas, Texas kwa ushirikiano wa DICOTA wakiwemo East Africa Diaspora Business Council ambao pia walitoa tuzo kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Kikwete.
Watatu toka kushoto ni Ndaga Mwakabuta Rais wa DICOTA akimkabidhi Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Wilson Masilingi tuzo ya Rais wa Jahmhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Kikwete siku ya Jumapili Septemba 20, 2015 wapili kulia ni Bwn. David Mureba ambaye ni Mwenyekiti wa East Africa Diaspora Business na wao ndio waliotoa tuzo hiyo kwa Mhe. Rais Jakaya Kikwete. Kulia ni Ben Kazora Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania Dallas, Texas na Rais wa EADBC(East Africa Diaspora Business Council)

Mhe. Wilson Masilingi akitoa shukurani kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Kikwete ambaye hakuweza kuhudhuria hafla hiyo.

Ben Kazora Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania Dallas, Texas na Rais wa EADBC(East Africa Diaspora Business Council) akiongea machache.

Tuesday, September 15, 2015

[AUDIO]: Kipindi cha JUKWAA LANGU Sept 14 2015

Kipindi hiki hukujia kila JUMATATU, kujadili mambo mbalimbali na zaidi kuhusu UCHAGUZI MKUU WA TANZANIA 2015
Hii ni sehemu ya pili ya kipindi kilichosikika Septemba 14, 2015
Kutoka Tanzania tuliungana na Jonathan Samiya na Nyakia, ambaye ni mmoja wa wakuu wa Itifaki wa kampeni za Dr Magufuli
Studioni alikuwepo Dj Luke Joe, Clare Ng'owo, Ali Badawy na Shamis Abdulla
Kwenye line tulikuwa na Jeff Msangi, Dr Patrick Nhigula na Arthur

Mgombea wa Ukawa Maulid Mtulila azindua kampeni ya ubunge jimboni Kinondoni!


Mgombea ubunge wa UKAWA kupitia chama cha CUF Maulid Salum Mtulia akihutubia mamia ya watu waliohudhria uzinduzi wa kampeni za ubunge jimbo la Kinondoni leo jioni.
Vyama vinavyounda Umoja wa katiba ya wananchi UKAWA leo hii vimezindua kampeni za ubunge kwa jimbo la Kinondoni ambapo mamia ya watu walihunduria katika viwanja vya Mapilau. Ukawa wameamua kusimamisha mgombea mmoja kwa kila jimbo toka vyama vya Chadema, CUF, NCCR Mageu na NLD ambapo kwa jimbo la Kinondoni Ukawa imemsimamisha Maulid Salum Mtulia.

Mh Iddi Azan azindua kampeni ya ubunge jimbo la Kinoindoni kwa kishindo!


Mh Iddi Azan akihutubia umti ulifurika katika viwanja vya CCM Mwinjuma, Mwananyamala jijini Dar leo jioni.
Mh Iddi Azan leo hii alizindua kampeni ya ubunge wa jimbo la Kinondoni ambapo yeye ndiye mgombea aliyeteuliwa na CCM kuiwakilisha katika uchguzi mkuu unaotarajiwa kufanyikwa tarehe 25 ya Mwezi Oktoba 2015.


 Katika uzinduzi huo uliofana ambapouliopambwa na bendi maarufu ya Twanga pepeta na wasanii luluki akiwemo Tunda Man toka TIP TOP connection na Bonge la nyau, Mh Azan alielezea maendeleo yaliyopatikana katika muda ambao yeye amekuwa mbunge wa jimbo hilo ni pamoja na miundo mbinu ya ya barabara na afya ambapo ameahidi kuwa iwapo atchaguliwa tena kuwa mbunge wa jimbo hilo atahakikisha barabara zote kubwa zinatiwa lami kwa kuwa pesa tayari zimeptikamna toka world bank na atahakikisha wodi za kina mama waja wazito zinaongezwa ili kupunguza msongamano katika wodi hizo.

Uzinduzi huo pia ulishuhudia wanachama wawili nguli wa Chama cha wananchi CUF wakirudisha kadi zao na kujiunga na CCM kitendo ambacho kiliamsha hamasa kubwa miongoni mwa wanchama na wapenzi wa CCM chama tawala.
Mwenekiti wa CCM wilaya ya Kinondoni akimnadi Mh Iddi Azan kwa maelfu ya watu waliohudhuria katika uzinduzi huo.
 Mstahiki meya wa wilaya ya Kinondoni Mh Yusuf Mwenda akiwapa vidonge Ukawa.

 Meya mstaafu wa Manispaa ya Kinondoni, Salum Londa akimwaga sera za CCM mbele ya umati wa wanachama wa chama hicho na wananchi waliofurika viwanjani hapo.

Sunday, September 13, 2015

UFAHAMU VYEMA MOYO WAKO "CARDIAC ARRHYTHMIA"

‘Cardiac Arrhythmia’ ni pale mtu anapokuwa na mapigo ya moyo yasiyo ya kawaida au yanayodunda sana. Mwili una mfumo asili wa umeme unaosaidia moyo kufanya kazi. Mfumo huu husababisha moyo kutanuka na kusinyaa ambapo husababisha damu kuingia na kutoka kwenye moyo; umeme kwa kawaida hufuata mkondo na mapigo ya moyo kwa kasi ya kawaida. Ingawa, kama mkondo wa kawaida wa umeme huu ukivurugwa moyo hushindwa kufanya kazi na kusababisha mapigo ya moyo ama kwenda taratibu sana, haraka sana au yasiyoimara.
Kuna aina kadhaa za ‘Arrhythmia’; Baadhi ni pamoja na zijulikanazo kitaalamu kama Supra-Ventricular Tachycardia, Ventricular Tachycardia, Ventricular Fibrillation, Atrial flutter and Atrial Fibrillation.
Mapigo ya moyo yasiyo imara hasa husababishwa na ugonjwa wa moyo na moyo kushindwa kufanya kazi. ‘Arrhythmia’ ndogo pia huweza kusababishwa na mtindo wa maisha usiozingatia afya bora ikiwa ni pamoja na uvutaji sigara uliopitiliza, Ulevi na kuzidisha matumizi ya kafeini au msongo wa mawazo.
Ingawa imegundulika hasa katika uchunguzi wa mara kwa mara wa matibabu dalili za ‘arrhythmia’ ni chache zinazoweza kuonekana ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa mapigo ya moyo, kupungua kwa mapigo ya moyo, maumivu ya kifua, kizunguzungu, kuchoka sana na kukosa pumzi.
‘Arrhythmia’ mara nyingi hutokea kwa nyakati tofauti tofauti. Hali ya kutotabiri kwa ‘arrhythmia’ na kutokea kwake kwa nyakati tofauti tofauti hufanya uchunguzi kuwa mgumu. Moja ya vifaa vitumikavyo zaidi kwa uchunguzi wake kitaalamu ni ‘electrophysiology (EP)’ na kinachukuliwa kuwa bora zaidi katika taaluma hii.
Utafiti wa EP hufanya kazi kwa kupima na kurekodi shughuli za umeme wa moyo na kuonesha njia za umeme. Inaonesha sababu na mahala penye tatizo la mapigo ya moyo. Matatizo yanayotokea katika utafiti wa EP ni machache sana kwa kuwa umekuwa ukifanyika salama kwa miaka mingi sasa.
Taarifa inaweza kuundwa katika namna mbili, ama kupitia ramani ya shughuli za umeme wa moyo kupitia kifaa maalumu kitaalamu ‘electrocardiogram (ECG)’ inayoonesha wapi ishara zisiyo za kawaida zinaanza kutokea ndani ya moyo.
Mfumo wa wa kitaalamu wa ‘Carto3’ ujulikanao kama ‘3D mapping’ ni teknolojia mpya inayotoa muonekano wa moyo kwa ukubwa mara tatu zaidi. Hii hupelekea kuboreshwa kwa usahihi wa vipimo na matibabu ya mgonjwa.
Kwa kesi ya kushuka kwa mapigo ya moyo, utafiti wa EP unatoa nafasi kutathmini haja ya vifaa kama vile ‘peacemaker’ au ‘defibrillator’ ambavyo husaidia kuzuia vifo vya ghafla vya magonjwa ya moyo.
Baada ya uchunguzi kupitia utafiti wa EP, mirija maalum ya ‘Radiofrequency (RF) catheter ablation’ huingizwa katika mishipa ya damu ambapo viwango vya juu na vya chini vya mzunguko wa nguvu ya umeme vinapokelewa katika tishu za moyo na kuharibu tishu zile zinazohusika na mapigo ya moyo ‘arrhythmia’. Baada ya matibabu kwa kawaida wagonjwa sasa huweza kikamilifu kupunguza matumizi ya dawa ambapo mgonjwa ataweza kupumua vizuri na mapigo ya moyo kwenda vizuri. 
kwa mujibu wa Dkt A M Karthigesan wa hospitali za Apollo baadhi ya ‘arrthythmia’ zilitibiwa kupitia kipimo maalumu kijulikanacho kitaalamu kama ‘RF Ablation’ ni ‘Supraventrical Tachycardia (SVT’; hii inatokea kwenye vyumba vya juu vya moyo na kwa ujumla inaelezewa kama moyo kupiga kwa kasi. Pingili za ‘Atirioventrikali (AVNRT)’, ‘atirioventrikali reentry (AVRT)’ na ‘focal atrial tachycardia’ ni baadhi ya aina nyingi za SVT.
Zaidi ‘Atrial Flutter (AFL)’ inaweza pia kutibiwa kwa upasuaji wa RF. AFL ni wakati atria inapopiga haraka sana kwa kiwango cha karibu mapigo 300 kwa dakika yanayotokea katika chumba cha juu cha moyo.
Arrhythmia nyingine maarufu inayotibiwa kwa RF ni ‘Atrial Fibrillation (AF)’. Hii ni wakati uwezo wa moyo kufanya kazi zake unapunguzwa kwa mapigo yasiyo na mpangilio ya chumba cha juu cha moyo. Ingawa ‘atrial fibrillation’ haitishii maisha, kuongezeka kwa mapigo ya moyo huweza kupelekea matatizo kama vile damu kuganda ambapo hatimaye inaweza kusababisha kiharusi.
Mwisho ‘Ventricular Tachycardia (VT)’ ambayo kama ikiachwa bila kutibiwa inaweza kuwa aina ya ‘Arrhythmia’ ya kuhatarisha maisha, hii hutokea wakati chumba cha chini cha moyo kikimpiga kwa kasi sana
Dkt. A M Karthigesan wa hospitali za Apollo anasema kuwa baadhi ya manufaa ya kufanyiwa tiba ya upasuaji kwa mirija ni kuwa mtu atarajie mabadiliko ya haraka katika ubora wa maisha sababu ya kuongezeka kwa uwezo wake wa kufanya kazi; Huduma ya matibabu iliyoboreshwa kwa jinsi mgonjwa anavyohitaji imeondoa upotevu wa muda; Kupungua kwa gharama za tiba na kuokoa maisha ambapo mgonjwa anapewa nafasi nyingine ya kuishi.

Imechangiwa na:
Dkt A M Karthigesan
Mshauri wa tiba ya umeme wa moyo
Hospitali za Apollo, Chennai

JUKWAA LA SANAA LAFANA, SALMA MOSHI AWALIPIA WASANII BIMA YA AFYA

-->Jukwaa La Sanaa la BASATA wiki hii lilipata wazungumzaji wa aina yake na kulifanya kuwa jukwaa lililochangamka na kuwa na mazungumzo ya zaidi ya masaa matano. Wasanii takriban 70 walikaa wakichambua maada mbalimbali kuhusu mustakhabari wa sanaa katika nchi yetu. Jambo ambalo liliingiza changamoto katika jukwaa hili, ni kuweko katika meza kuu wasanii wawili ambao walianza sanaa nchini na hatimae kuhamia ughaibuni ambako ndiko wanaishi kwa sasa.

Wasanii Salma Moshi aliyekuwa akijulikana kama Salma Nyoka, msanii wa kwanza wa kike kuchezea nyoka katika jukwaa, na ambaye alikuwa kiongozi wa vikundi vilivyotamba kama DDC Kibisa Cultural Troupe Super Mama Cultural Troupe na Ujamaa Cultural Troupe, na Abbu Omar, mwanamuziki aliyewahi kupigia bendi kama Urafiki na UDA Jazz ambae kwanza alihamia Kenya na kupiga na kurekodi na makundi kama Simba wa Nyika na Les Wanyika na pia kurekodi album kadhaa akiwa na kundi lake ambaye hatimae alihamia Japan ambako amekuwa akiishi kwa kupiga muziki na akiwa na waTanzania wengine kama Lista na Fresh Jumbe.

Mazungumzo yaligusia nyanja mbalimbali ikiwemo umuhimu wa kuwa na mikataba kabla ya kazi, kuboresha kazi ili kuweza kuuza nje, namna ya kujitambulisha duniani kwa kuwa na websites na blogs, na pia serikali kubadilika na kuweko mfumo wa uongozi wa sanaa kuanzia ngazi ya wilaya hadi Taifa. Katika mkutano huo, John Kitime Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanamuziki aliongelea fursa ya Bima ya Afya kwa wasanii, ambapo Salma Moshi alijitolea kuwalipia nusu ya ada wasanii wanne, na kumlipia bima kamili Mzee Kassim Mapili ambaye kwa sasa anasumbuliwa na moyo na figo. Abbu Omar pia aliamua kulipia Bima yake na kueleza kuwa katika nchi ya Japan ni lazima kila mwananchi kuwa na Bima ya Afya, kwani ugonjwa hauji kwa taarifa na matibabu ni gharama kubwa.

Mkutano huo ulianza saa tano na kulazimishwa kusimamishwa saa kumi, kwani wasanii bado walikuwa na mengi ya kuwauliza wasanii hawa nguli walioweza kuendeleza maisha ughaibuni kupitia sanaa
Baadhi ya wasanii wakimsikiliza Salma Moshi

Mwandishi maarufu Khadija Khalili (mwenye daftari) akifuatilia maada

Mwenyekiti wa CHAMRUMBA akiwa na Mzee Mapili


Francis Kaswahili mwenye kofia Mwenyekiti TAFOMUDEA





Abbu Omari mwanamuziki aishiye Japan

Salma Moshi na Mzee Mapili

Meza Kuu

Group Picture


Salma akiwa na baadhi ya wasanii aliowalipia sehemu ya Bima ya Afya
IMETAYARISHWA NA www.johnkitime.co.tz

Monday, September 7, 2015

Bin'adam "TENA"....Na maisha KINYUMENYUME. Apumzikaye kusherehekea SIKU YA KAZI

Na Mubelwa Bandio
 Ni SIKU YA KAZI hapa Marekani. Ama niseme kuthamini kazi. Ama siku ya wafanyakazi. Lakini vyovyote iwavyo, ni siku ambayo wengi wetu hapa Marekani tunakuwa na "siku ya mapumziko". NDIO, DAY OFF katika kusherehekea SIKU YA KAZI.
Mmmmmhhh!!! Umeona eeee?
Nilishaandika kuhusu kinyumenyume cha Bin-adamu katika kutenda, kunena na kuwaza. Kuwa kwanini tuwazishwe vitu kwa namna nyingine?
Kwanini nchi nyingi Afrika zisherehekee UHURU kwa staili ya gwaride kama la WAKOLONI WALIOTUTAWALA?
Kwanini siku ya wakulima isherehekewe mjini, na wapatao "day off" ni wale wasio wakulima ilhali wakulima hawapati sherehe yoyote siku hiyo?
Ni kwenye muendelezo huu wa KWANINI, najikuta naleta MASWALI YAFUATAYO, ambayo nilitumiwa na rafiki yangu, na si mawazo yangu.
TUMUWAZE BIN'ADAM NA UNAFIKI WA MAWAZO YA KIMATENDO.
Soma kisha uwaze, "bin'adamu anawaza nini kutenda atendayo?" Japo nilitumiwa NICHEKE, lakini yaliniwazisha pia
-Why do supermarkets make the sick walk all the way to the back of the store to get their prescriptions while healthy people can buy cigarettes at the front?
-Why do people order double cheeseburgers, large fries, and a diet coke.
-Why do banks leave vault doors open and then chain the pens to the counters.
-Why do we leave cars worth thousands of dollars in our driveways and put our useless junk in the garage.

EVER WONDER .......
-Why the sun lightens our hair, but darkens our skin?
-Why can't women put on mascara with their mouth closed?
-Why don't you ever see the headline 'Psychic Wins Lottery'?
-Why is 'abbreviated' such a long word?
-Why is it that doctors call what they do 'practice'?
-Why is lemon juice made with artificial flavoring, and dish washing liquid made with real lemons?
-Why is the man who invests all your money called a broker?
-Why is the time of day with the slowest traffic called rush hour?
-Why isn't there mouse-flavored cat food?
-Why didn't Noah swat those two mosquitoes?
-Why do they sterilize the needle for lethal injections?
You know that indestructible black box that is used on airplanes? Why don't they make the whole plane out of that stuff?!
-Why don't sheep shrink when it rains?
-Why are they called apartments when they are all stuck together?
If flying is so safe, why do they call the airport the terminal?

HIVI TUNAWAZA NINI?

***"Waliwaza nini ni kipengele cha kuelimishana tukifurahia. Hiki kitakuwa kikikuletea habari za kweli na kushangaza kuhusu watu ambao wamefanya yale ambayo unaweza kujiuliza kuwa WALIWAZA NINI? wakati wanatenda haya. Kitakuwa na habari fupifupi kutoka ulimwenguni kote. Kwa habari zaidi kuhusu kipengele hiki BOFYA HAPA"***

Wimbo mpya wa UCHAGUZI toka kwa INNOCENT GALINOMA

Kuelekea uchaguzi mkuu nchini Tanzania, watu kupitia fani na kazi mbalimbali wamekuwa wakijaribu kuhamasisha wananchi kushiriki kufanya maamuzi yatakayolipeleka taifa letu mbele.
Innocent Galinoma, ni msanii mkongwe wa Reggae anayefanya kazi zake nchini Tanzania.
Naye ametunga wimbo maalum kwa ajili ya uchaguzi huu mkuu. Akisisitiza kuhusu kusikiliza na kuwahoji wagombea ili kujua fika wanalotaka kutufanyia katika kutatua kero zetu
Karibu usikilize kibao....UCHAGUZI

Saturday, September 5, 2015

Reggae Time ya Pride FM......Justin Kalikawe


Ni zaidi ya miaka 12 sasa tangu kuondokewa na mwanamuziki mahiri wa Reggae kutoka nchini Tanzania, Justine Kalikawe.
Kwangu ni kumbukumbu “mbichi” ya kuondoka kwake, kwa kuwa alifariki tukiwa kwenye mkakati wa kufufua hamasa na umuhimu wa muziki wa reggae nchini.
Nakumbuka ilikuwa ni mwaka 2003. Mwaka ambao ulikuwa na mambo mengi saana kwangu. Ndio mwaka ambao nikiwa na Dj Fax (wakati huo sote tukiwa 100.5 Times Fm) tulipanga mikakati ya kuwa na kipindi bora zaidi cha Reggae jijini Dar (ambako radio hiyo ilikuwa ikisikika).
Na nakumbuka tulipanga kukutana na kushauriana na wadau mbalimbali wa Reggae nchini kuhusu namna tunavyoweza kushirikiana kuunyanyua muziki huo uliolenga katika KUELIMISHA, KUBURUDISHA na KUIKOMBOA AKILI YA JAMII ya wanyonywaji. Ni katika harakati hizo nilipoweza kuonana na kufanya mahojiano na wasanii kama Jah Kimbute, Ras Inno na nikakosa nafasi kuonana na Justine Kalikawe ambaye alikuwa akikosekana kutokana na ratiba yake ya kurekodi. Hivyo nikawa "namvizia" ili kujua muda ambao hashiriki kurekodi nimpate naye aweze kuizungumzia tasnia ya Reggae nchini Tanzania.
Bahati mbaya Justine aliondoka na kwenda nje ya nchi kwa zaiara ya kimuziki na aliporejea hakukaa muda mrefu akakutwa na mauti. Huo ndio ukawa mwisho wa ushiriki wake katika mkakati huo.
Lakini wakati anafariki, nilikuwa likizo Bukoba, hivyo siku hiyohiyo nilipata taarifa zilizonishtua sana, lakini nikazikubali na kuanza mikakati ya kushiriki mazishi yake, jambo ambalo nililifanikisha.
Lakini….
Justin Kalikawe ni nani?

MWANAMITINDO JOCKTAN MAKEKE KUWAKILISHA TANZANIA KWENYE MASHINDANO YA TDWFS NCHINI AFRKA KUSINI

 Msanii wa mitindo ya kiafrika kutoka Tanzania JOCKTAN WA MAKEKE AFRIKA ambaye amekuwa tishio katika mitindo ya asili ya mwafrika ameendelea kuiwakilisha vyema Tanzania katika majukwaa mbalimbali ndani na nje ya nchi , kama unakumbuka mwezi wa saba alituwakilisha vyema Jijini Nairobi na kuonekana mwanamitindo bora sasa.
  Msanii huyu ambaye ndio mwanzilishi ya kampuni ya MAKEKE AFRIKA CO.  LTD atapanda tena jukwaani mwezi huu nchini Afrika Kusini kufanya maajabu kwa mara nyingine katika shindano hili kubwa la mitindo nchini Afrika kusini, JOCKTAN WA MAKEKE AFRIKA amesema kuwa sasa anakuja na collection nyingine mpya inayokwenda kwa jina la TABID - THE AFRICAN BEAUTY IN THE DARKNESS  ambayo itaonekana katika jukwaa hilo la TDWFS - the designers walk fashion show hivi karibuni.
       ABOUT  THE DESIGNERS WALK FASHION SHOW
This is an event, hosted by Auriginal PTY.(LTD), that brings together aspiring models and designers to compete and showcase their talents and innovation.
The Designers Walk fashion show is an event founded to serve as a platform for rising models and designers. By means of a competition, we have the judges and the people to evaluate the best. However, the decision of who the best doesn't end ones opportunities. 
aside from models and designers, we have rising entertainers coming to the table, to expand their horizon and to keep you on your toes during the event. With interested people, their opportunities can also expand.

UZINDUZI WA KAVASHA CLUB NA KITABU CHA JIFUNZE LINGALA MTUNZI TCHIMANGA ASSOSSA


Uzinduzi wa Dar Kavasha Club pamoja na uzinduzi wa kitabu cha kujifunza Kilingala utafanyika leo tarehe 05-Sep-2015 kuanzia saa 12 jioni katika ukumbi wa MRC Mikocheni, ukumbi ulio nyuma ya Shopperz Plaza. Uzinduzi huo utasindikizwa na burudani  kutoka kwa wana Bana Marquis bendi inayoongozwa na mwanamuziki Tshimanga Kalala Assosa, ambaye pamoja na kuwa ni kati ya wanamuziki waliokuweko katika enzi ya uanzishwaji na ukuaji wa mtindo wa Kavasha, akiwa mwanamuziki wa bendi kama Negro Success, Lipualipua, Orchestra kamale, na Orchestra Fuka fuka.
Uzinduzi huu ulikuwa ufanyike mwezi wa 5 lakini ukaahirishwa kutokana na mvua kubwa iliyonyesha siku ambapo uzinduzi huo ulipangwa kufanyika.
Kiingilio cha onyesho hili ni BURE. Na hakika tukio hili ni la aina yake katika tasnia ya muziki wa dansi

A+E NETWORKS(R) KURUSHA DOKUMENTARI YA OJ SIMPSON

A&E_0005
Mkuu wa vipindi channel ya A & E Networks, Racheal Job akizungumza na waandishi wa habari kutoka nchi za Afrika waliokusanyika kwenye jukwaa kubwa la kuonesha vitu mbalimbali vinavyoburudisha katika chaneli za DStv na GoTv kupitia MultiChoice nchini Mauritius. Katikati ni Mkurugenzi wa Kanda channel ya A & E Networks, Anthea Petersen na kushoto ni Mkuu wa Mawasiliano channel ya A & E Networks, Sarah Williams-Robbins.
A&E_0038
Mkuu wa Mawasiliano channel ya A & E Networks, Sarah Williams-Robbins akifafanua jambo kwenye jukwaa lililowakutanisha waandishi wa habari (hawapo pichani) kutoka nchi mbalimbali za Afrika nchini Mauritius.
A&E_0045
Ebenezer Donkoh kutoka YFM Ghana akiuliza swali katika mkutano wa waandishi wa habari ulionadaliwa na MultiChoice Africa.

Serikali ya Awamua ya Tano ni ya Viwanda - Samia Suluhu

Baadhi ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wananchi wakiwa katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa kiti cha urais Bi. Samia Suluhu Jimbo la Kawe Kata ya Msasani kwenye viwanja vya Namanga jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wananchi wakiwa katika mkutano wa kampeni wa mgombea mwenza wa kiti cha urais Bi. Samia Suluhu Jimbo la Kawe Kata ya Msasani kwenye viwanja vya Namanga jijini Dar es Salaam.
Mgombea mwenza wa kiti cha urais, Bi. Samia Suluhu akizungumza na wanaCCM na wapenzi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika mkutano wa kampeni wa kwenye Viwanja vya Namanga jijini Dar es Salaam. Mgombea mwenza wa kiti cha urais, Bi. Samia Suluhu akizungumza na wanaCCM na wapenzi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika mkutano wa kampeni wa kwenye Viwanja vya Namanga jijini Dar es Salaam.
Mgombea mwenza wa kiti cha urais, Bi. Samia Suluhu akimtambulisha mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM Jimbo la Kawe, Kippi Warioba (kushoto) katika mkutano wa kampeni wa kwenye Viwanja vya Namanga jijini Dar es Salaam.  
Mgombea mwenza wa kiti cha urais, Bi. Samia Suluhu akimtambulisha mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM Jimbo la Kawe, Kippi Warioba (kushoto) katika mkutano wa kampeni wa kwenye Viwanja vya Namanga jijini Dar es Salaam.

Thursday, September 3, 2015

MULTICHOICE AFRICA KICKS OFF THE BIGGEST CONTENT SHOWCASE IN AFRICA

D3A_2835
MC's during the official opening of MultiChoice Africa Content Showcase Extravaganza, IK (right) and Eku at the Outrigger Beach Resort in Mauritius.(Photos by MultiChoice and Zainul Mzige of Modewjiblog).
It was a magical night filled with #OnlyTheBest of African entertainment when MultiChoice Africa kicked off its second #OnlyTheBest Content Showcase Extravaganza in spectacular style at the Outrigger Resort.
The star-studded guestlist read like the who's who of Africa's entertainment and media.
The guests walked down the African media Walk of Fame onto a red-carpet that opened up to a sensational night of dazzling entertainment. The event, dubbed 'Night of a Thousand Stars' saw all the glitz and glamour of Hollywood, Bollywood and Nollywood come to life on the island paradise, as guests that include Genevieve Nnaji, Rita Dominic, Desmond Elliot and Ramsey Nuoah were given the full movie-star treatment. Flavour, Stonebwoy and The Mavins kept the guests on their feet with their popular hits while the night's MCs IK and Eku kept the glamorous proceedings running smoothly.
Guest also experienced host IK who also brought his popular show, 'High Lites with IK', to the stage in Mauritius with a delightful interview with Nigerian crooner Banky W alongside music by DJ Sousa.
D3B_6272
Red carpet treatment for the guest #OnlyTheBest.
MultiChoice Africa's CEO Tim Jacobs also took to the stage to welcome guests with a promise that the video entertainment service provider will do all it can to make only the best content available to its subscribers on any platform, on any device and at any time.
“We believe television is an extremely powerful tool that can educate, entertain and inform. The evolution of this medium has become fast and furious and as a business we are constantly evolving to stay ahead,” said Jacobs at a glittering ‘Night of a Thousand Stars’ event. “MultiChoice’s business is built around three key pillars: people; content - in the form of great entertainment, news and sport - and the latest cutting-edge technology. Our mission is to ensure that our subscribers do not miss out on any of the stories, events or moments that are shaping our future.”
Jacobs lauded the success of MultiChoice’s GOtv DTT (Digital Terrestrial Television) offering, which currently operates in 8 countries, bringing low-cost digital television to homes and supporting governments in freeing up vital broadcast spectrum by switching from analogue to digital signal.
He also acknowledged the challenges which the business faces. “Our growth over the last 20 years has been a result of massive investments we have made in people, content and technology – but as with any business, not all of these investments or changes have hit the spot…. so we have from time to time re-evaluated our position and made changes to our strategies. At the end of the day however it is really our subscribers we have to thank for staying with us, trusting us to deliver the best television experience and customer service to make their experience world class,” said Jacobs.
D3B_6293
M-Net Regional Director West Africa, Wangi Mba-Uzoukwu (right) and Eku the MC flanked by another guest.
M-Net Regional Director West Africa, Wangi Mba-Uzoukwu, reminded guests that M-Net has a near 30-year history on the continent, where it started with a daily 12-hour broadcast on a single channel. Now, having changed the way television is viewed across the continent, the broadcaster leads the way in producing, acquiring and showcasing the best entertainment content in Africa. “Our first broadcast in 1986 led to other firsts like the launch of SuperSport and the Mzansi Magic, Zambezi Magic, Jango Magic and Africa Magic channels; and with the creation of exciting, genre-defining and iconic content like Carte Blanche and Tinsel, M-Net continues to shape cultures, build bridges and empower talent across Africa even as we remain synonymous with all things entertainment on the continent,” said Mba-Uzoukwu.
She echoed Jacobs’ sentiments about the need for constant evolution, to stay ahead of the video entertainment service provision field. “We are launching and redefining channels and we continue to expand our content offerings to viewers across the continent. Our ongoing and significant investments in local productions have positioned Africa on the entertainment global arena and with new technology we continue to reach even more people, ensuring that no one ever misses the M-Net Magic. Our investment drive remains geared not only towards the industries in which we play, but also in the people who power them,” said Mba-Uzoukwu.
The MultiChoice Africa Content Showcase is a dynamic 5-day content extravaganza, which sees a host of DStv’s biggest channels, including Sony, SuperSport, Zee TV, A+E, Disney, MTV Base, BET, Comedy Central, BBC and M-Net previewing their latest and greatest content, soon to be seen across the video entertainment services provider’s platforms. To keep track of happenings at the MultiChoice Africa Content Showcase, follow @multichoice_africa on Instagram, @mcashowcase on Twitter, or via #OnlyTheBest.