Thursday, September 24, 2015

DINNER ILIYOANDALIWA NA JUMUIYA YA WATANZANIA DALLAS KWA USHIRIKIANO WA DICOTA WAKIWEMO EAST AFRICA DIASPORA BUSINESS COUNCIL

 Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Wilson Masilingi akiongea na Watanzania na marafiki zao waliohudhuria chakula cha jioni kilichoandaliwa na Jumuiya ya Watanzania Dallas, Texas kwa ushirikiano wa DICOTA wakiwemo East Africa Diaspora Business Council ambao pia walitoa tuzo kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Kikwete.
Watatu toka kushoto ni Ndaga Mwakabuta Rais wa DICOTA akimkabidhi Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Wilson Masilingi tuzo ya Rais wa Jahmhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Kikwete siku ya Jumapili Septemba 20, 2015 wapili kulia ni Bwn. David Mureba ambaye ni Mwenyekiti wa East Africa Diaspora Business na wao ndio waliotoa tuzo hiyo kwa Mhe. Rais Jakaya Kikwete. Kulia ni Ben Kazora Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania Dallas, Texas na Rais wa EADBC(East Africa Diaspora Business Council)

Mhe. Wilson Masilingi akitoa shukurani kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Kikwete ambaye hakuweza kuhudhuria hafla hiyo.

Ben Kazora Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania Dallas, Texas na Rais wa EADBC(East Africa Diaspora Business Council) akiongea machache.


No comments: