Saturday, April 17, 2021

Reggae Time ya Kwanza Radio. Historia ya muziki wa Reggae

Muziki wa reggae ni mahadhi ambayo ni matokeo ya kutambulika na kuendelezwa kwa aina ama mitindo mingine ya muziki. Licha ya kwamba reggae inatambulika zaidi kutoka katika miziki ya Carribean yenye asili ya Afrika na miziki ya R&B toka Marekani, lakini reggae tunayoisikia sasa ni muendelezo wa midundo ya Rocksteady na Ska kuanzia miaka ya 1960 huko Jamaica. Katika miaka ya 1950, enzi ambazo wakazi wa visiwa vya Carribean walikuwa wapenzi wakubwa wa miondoko ya Calypso na wakati ambao waMarekani walikuwa akipenda zaidi miziki ya wasanii kama Harry Belafonte, wananchi wengi wa Jamaica walikuwa wakisikiliza zaidi miziki ya Rhythm and Blues (R&B) za kiMarekani. Miziki hiyo ilikuwa ikisikika zaidi kutoka miji ya Memphis, New Orleans na Miami na kuwa maarufu sana nchini Jamaica. Wanamuziki wa Jamaica wakachanganya miondoko hiyo ya R&B na miondoko ya Calypso ya Jamaika na kutengeneza muziki mpya wa SKA.

No comments: