Friday, March 20, 2009

Them, I &Them. TANZANIA REGGAE FAMILY.........Hakuna

Marehemu Justine Kalikawe akiwa na moja kati ya tuzo alizowahi kushinda
Nikiwa na Ras Pompidou, Jah Kimbuteh, Ras Inno, Mjane wa Justine Kalikawe na Meneja wake wa kwanza katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo kuelezea tamasha la kumuenzi Justine ('03)
Mwaka 2003 ulikuwa na mambo mengi saana kwangu. Nakumbuka ndio mwaka ambao nikiwa na Dj Fax (wakati huo sote tukiwa 100.5 Times Fm) tulipanga mikakati ya kuwa na kipindi bora zaidi cha Reggae mjini Dar. Nakumbuka tulipanga kukutana na kushauriana na wadau mbalimbali wa Reggae nchini kuhusu namna tunavyoweza kushirikiana kuinyanyua muziki huo uliolenga katika KUELIMISHA, KUBURUDISHA na KUIKOMBOA AKILI YA JAMII ya wanyonywaji. Ni katika harakati hizo nilipoweza kuonana na kufanya mahojiano na wasanii kama Jah Kimbute, Ras Inno na nikakosa nafasi kuonana na Justine Kalikawe ambaye alikuwa akikosekana kutokana na ratiba yake ya kurekodi.
Bahati mbaya Justine aliondoka na kwenda nje ya nchi kwa zaiara ya kimuziki na aliporejea hakukaa muda mrefu akakutwa na mauti.
Ni katika kipindi kifupi saana tangu afariki, wasanii mbalimbali wa muziki wa Reggae Tanzania walikusanyika na kuandaa wimbo maalum (na baadae tamasha) kumuenzi mfalme huyo wa Reggae. Katika kutengeneza hilo, wasanii hao walitumia midundo ya nyimbo zake na mashairi toka katika nyimbo za Kalikawe toka katika albamu mbalimbali na kuunda wimbo HAKUNA.
Huu ni kati ya nyimbo bora za reggae kuwahi kuandikwa nchini Tanzania na ni kwa sababu mbalimbali zikiwemo.
1: Ulijumuisha wasanii nyota karibu wote wa muziki huo nchini akiwemo Inno Galinoma, Jah Kimbuteh, Ras Inno Nganyagwa, JhikoMan, Carola Kinasha, Athanas Sajula na wengine wengi.
2: Ulifanyiwa mazoezi kwa muda mfupi na kuimbwa kwa ufasaha.
3: Ulijumuisha midundo na mashairi ya Kalikawe ambayo yalikuwa yakisimuliwa na wasanii hawa
4: Ulionesha umoja wa wasanii wa Reggae nchini
Mbali ya hayo yote, pia uliweza kushinda tuzo na pia kutumika kwa muda mrefu zaidi.
Nami leo nawaletea kundi hili la Tanzania Reggae Family katika wimbo huu HAKUNA ambao ulikuwa maalum kumuenzi nyota wa Reggae nchini Tanzania Justine Kalikawe.
Kama alivyosema (Justine) na kama ilivyokaririwa na wanamuziki hawa, nami nawakilisha kwako kuwa "hakuna atakayekuja kukufanyia yale utakayo yafanyake, hakuna atakayekuja kukuletea, yale utakayo uyapate. Itabidi ufanye mwenyewe"
Swali kwa wana Tanzania Reggae Family ni kuwa mu-wapi na mbona hakuna kilichoendelea baada ya hapa? Watu walitoa nyimbo na albamu lakini hatuoni umoja uliooneshwa hapa na uliodhamiriwa kuendelezwa.


**Them, I & Them ni kipengele kikujiacho kila Ijumaa kinachoelezea kazi za wasanii (Them) kulingana na maono yangu (I) kwa ajili na manufaa ya hadhira (Them)**
Kwa nyimbo zaidi ndani ya kipengele hiki bofya hapa.
IJUMAA NJEMA

3 comments:

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

kalikawe bwana, namkumbuka akipita mitaa ya kwetu kwa miguu kwenda town ezi zile nakaa kwenye vilima vya kashula
kifo chake majamaa wanakiema mengi sijui kama ni kwli kwamba mshikaji alifanywa kuwa msukula na matajiri fulani?

Yasinta Ngonyani said...

Astareha kwa amani, Na pia nimekipenda kipande hiki kizuri cha reggae kwani ni miziki yangu. Ijumaa njema pia

Anonymous said...

hapa kuna mambo kadhaa.the system haipendi watu wajue au kusikiliza nyimbo za hisia badala yeke wanahamasisha nyimbo za mapenzi.

rasta hapa.

amani.